Ijumaa, 11 Aprili 2014

ULIMPOKEA ROHO MTAKATIFU ULIPOAMINI?


(Mtendo 19:1–3)
“Ikiwa Apolo alipokuwa Korintho, Paulo, akiisha kupita kati ya nchi za juu alifika Efeso, akakutana na Wanafunzi kadhaa wa kadha huko akawauliza Je, mlimpokea Roho Mtakatifu mlipo amini? Wakajibu la, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia. Akawauliza basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema kwa ubatizo wa Yohana.”
Aina gani ya Injili Paulo alihubiri? Alihubiri Injili ya ubatizo wa Yesu na damu yake. Matendo 19:1-2 inasema “Ikiwa, Apolo alipokuwa Korintho, Paulo akiisha kupita kati ya nchi za juu akafika Efeso, akakutana na Wanafunzi kadhaa wa kadha huko akawauliza, Je, mlimpokea Roho Mtakatifu mlipoamini?”
Hata hivyo watu hawa walikuwa wamekwisha mwamini Yesu huku wakiwa wameweka kando maana ya ubatizo wa Yesu. Hawakujua juu ya Injili njema ambayo hupelekea kumpokea Roho Mtakatifu ndani. Na hii kupelekea Paulo kuuliza “Je, mlimpokea Roho Mtakatifu mlipoamini?” lilikuwa swali geni kwa baadhi ya wafuasi. Watu wengine wangeliweza kuuliza “Je, una mwamini Yesu?” Lakini Paulo aliuliza swali katika njia isiyokuwa ya kawaida ili kwamba waweze kumpokea Roho Mtakatifu, ndani yao kwa kufanya upya imani zao katika Injili njema. Huduma ya Paulo ilikuwa ni kuhubiri Injili njema ya ubatizo wa Yesu kwa Yohana Mbatizaji. 
Hebu tuone ushuhuda wa Mitume katika Injili ya ubatizo. Kwanza Paulo alishuhudia “Hasha sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi? Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?” (Warumi 6:2-3). “Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo” (Wagalatia 3:27).
 Mtume Petro naye pia alishuhudia Injili ya ubatizo wa Yesu katika 1 Petro 3:21–22 akisema “Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unawaokoa ninyi pia siku hizi (siyo kuweka mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamira safi mbele za Mungu) kwa kufufuka kwake Yesu Kristo. Naye yupo mkono wa kuume wa Mungu amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zikiisha kutiishwa chini yake.”
Mtume Yohana pia alishuhudia hii Injili njema katika 1 Yohana 5:5-9 “Mwenye kuushinda ulimwenguni ni nani isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni mwana wa Mungu? Huyu ndiye aliye kuja kwa maji na damu. Naye Roho ndiye ashuhudiaye kwa sababu Roho ndiye kweli. Kwa maana wako watatu washuhudiao mbinguni Baba na Neno na Roho Mtakatifu na watatu hawa ni umoja. Kisha wako watatu washuhudiao duniani, Roho na maji na damu na watatu hawa hupatana kwa habari moja”.
Yohana Mbatizaji alichukua nafasi muhimu, katika kukamilisha Injili njema. Biblia inazungumzia yafuatayo juu ya Yohana Mbatizaji katika Malaki 3:1-3 na Mathayo 11:10-11.
Yohana Mbatizaji alikuwa mwakilishi wa wanadamu na alikuwa ni nabii Eliya ajaye kama alivyoandikwa katika Agano la Kale. Katika Agano la Kale, sadaka ya dhambi ilichinjwa ili kumwaga damu baada ya kubeba dhambi za mtu kwa tendo la kuwekewa mikono. Katika Agano Jipya, hata hivyo Yesu ndiye aliyesimama kama sadaka ya dhambi kwa kubeba dhambi ya ulimwengu kwa njia ya ubatizo na kifo chake Msalabani kulipa mshahara wa dhambi. Ubatizo wa Yesu kwa Yohana Mbatizaji pale Yordani ndiyo uliokoa wanadamu wote.
Mungu alipanga aina mbili za matukio ili kuweza kuwaokoa wanadamu tokana na dhambi zao na kuweza kutimiza haki yote. Tukio la kwanza lilikuwa ni kumfanya Yesu aje ulimwenguni kupitia mwili wa mwanamwali Bikira Mariam, na kuwezesha abatizwe na kusulubiwa ili kuondoa dhambi za ulimwengu. Tukio la pili ni kuwepo kwa Yohana Mbatizaji duniani kupitia Elizabeti mama yake. Mungu alisababisha matukio haya mawili yatokee ili wanadamu waweze kuokolewa kwa dhambi zao zote. 
Hii ni kazi ambayo Mungu aliipanga katika utatu. Mungu alimtuma Yohana Mbatizaji ulimwenguni miezi sita kabla ya Yesu, ndipo akatumwa Yesu Kristo mwokozi wa wanadamu hapa duniani kuwaweka huru wanadamu tokana na hukumu ya dhambi zao.
Yesu alishuhudia juu ya Yohana Mbatizaji katika Mathayo 11:9 “Lakini kwa nini mlitoka? Ni kuona Nabii? Naam, nawaambia na aliye mkuu zaidi ya Nabii”. Zaidi ya yote, pale Yohana Mbatizaji aliyemtwika dhambi zote za ulimwengu Yesu, alipo mwona tena siku aliyofuata yeye mwenyewe alishuhudia kwa kusema “Tazama! mwana kondoo aichukuaye dhambi ya ulimwengu” (Yohana 1:29).
Biblia ina taarifa nyingi za Yohana, aliye mbatiza Yesu na inatupasa kupekuwa na kutafuta ili kuweza kuwa na ufahamu mzuri juu yake. Yohana Mbatizaji alikuja ulimwenguni kabla ya
Yesu jukumu lake likiwa kutimiza Injili njema ambayo ndiyo mpango wa Mungu. Biblia inasema kwamba Yesu alikubali dhambi zote za ulimwengu juu yake toka kwaYohana, naye Yohana alimtwika dhambi hizo juu yake ili kutimiza mapenzi ya Mungu.
Tunamwita kuwa ni Yohana Mbatizaji kwa sababu alimbatiza Yesu. Ubatizo wa Yesu una maana gani? Neno “ubatizo” linamaanisha “kuoshwa” kwa kuwa dhambi zote zimekwisha kutwikwa juu ya Yesu kwa kupitia ubatizo wake, hivyo basi zimekwisha kuoshwa. Ubatizo wa Yesu una maana sawa na tendo la “kuwekea mikono” ambalo ile sadaka ya dhambi ilipokea katika Agano la Kale. Maana ya kiroho ya tendo la ubatizo ni “kutwika, kuoshwa au kuzikwa”. Ubatizo wa Yesu kwa Yohana ulikuwa ni tendo la ukombozi katika kuondoa dhambi zote za watu wa ulimwengu.
Ubatizo wa Yesu unaumuhimu sawa kama ilivyo tendo la kuwekea mikono, ambapo ni njia ya kutwika dhambi juu ya sadaka ya dhambi katika Agano la Kale. Kwa maneno mengine,
watu wa Israeli walitwika dhambi zao za mwaka mzima juu ya sadaka ya dhambi katika siku ya Upatanisho kwa kupitia tendo la kuwekea mikono ya kuhani mkuu. Sadaka hii katika Agano la Kale ilikuwa na dhambi sawa na ubatizo wa Yesu na kifo chake msalabani.
Mungu aliiteuwa siku ya Upatanisho kuwa ni muda wa kuondoa dhambi za wana wa Israeli. Katika siku ya kumi ya mwezi wa saba, kuhani mkuu alitwika dhambi za mwaka za watu wake juu ya kichwa cha sadaka ya dhambi kwa kuwekea mikono juu ya sadaka kwa upatanisho wa dhambi za watu. Na huu ndio mpangilio wa utoaji wa sadaka ambao Mungu aliuweka. Ilikuwa ndio njia pekee katika kutwika dhambi za watu juu ya sadaka ya dhambi na alifanya hivyo kwa tendo la kuwekea mikono ambalo ndiyo sheria ya milele Mungu aliyoweka.
“Na Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai, na kuungama juu yake uovu wote wa wana wa Israeli na makosa yao, naam dhambi zao zote, naye
ataziweka juu ya kichwa chake yule mbuzi kisha atampeleka aende jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari na yule mbuzi atachukua juu yake uovu wao wote, mpaka nchi isiyo watu, naye atamwacha mbuzi jangwani” (Walawi 16:21-22).
Katika Agano la Kale, mwenye dhambi aliweka mikono juu ya kichwa cha sadaka ya dhambi na kutwika dhambi zake juu yake ili aweze kusamehewa. Na siku ya Upatanisho Haruni Kuhani Mkuu akiwa mwakilishi wa Waisrael wote, aliweka mikono yake juu ya kichwa cha sadaka ya dhambi ili kutwikwa sadaka hiyo dhambi zote za Waisraeli. Ndipo sadaka hiyo huchinjwa baada ya kubeba dhambi hizo.
Tendo hilo linamaana sawa ya kiroho kwa ubatizo (“Baptisma” ni Kigiriki, maana yake “kusafisha kuzikwa kutwikwa”) ambapo Yesu aliupokea toka kwa Yohana katika Agano Jipya. Kama alivyokuwa Kuhani Mkuu katika Agano la Kale alipoweka mikono yake juu ya sadaka ya dhambi ili kutwika dhambi za watu wa Israel, ndivyo hivyo dhambi zote za wanadamu zilitwikwa juu ya Yesu kupitia ubatizo wake na Yohana Mbatizaji. Ndivyo Yesu alivyokufa Msalabani katika kutupatanisha kwa dhambi zetu.
Hii ni Injili njema. Kama ilivyo Haruni kuhani Mkuu alivyotoa sadaka ya Upatanisho kwa niaba ya watu wa Israeli, Yohana Mbatizaji naye aliye uzao wa Kuhani Haruni alichukua jukumu hilo akiwa mwakilishi wa wanadamu juu yake Yesu. Mungu anaeleza mpango huu ulio mzuri wa ajabu kuhusiana na upendo wake katika Biblia kama ifuatavyo katika kitabu cha Zaburi 50:4-5 “Ataziita mbingu zilizo juu na Nchi pia wahukumu watu wake. Nikusanyieni wacha Mungu wangu waliofanya Agano nami kwa dhabihu” Amen, Haleluyah.
Historia ya Kanisa inasema kwamba hapakuwepo na Krismasi kwa karne mbili za mwanzo katika kuanzishwa kwake. Kanisa la Wakristo wa mwanzo pamoja na Mitume wa Yesu
waliadhimisha January 6 kama “Siku ya Ubatizo wa Yesu” tu, uliofanyika katika mto Yordani na Yohana Mbatizaji. Kwa nini waliweka msisitizo zaidi katika hilo, yaani ubatizo wa Yesu katika imani yao? Jibu lake ndilo ufunguo halisi wa Ukristo wadesturi ya Kitume.
Lakini natumaini hamtochanganya ubatizo wa waumini na ule ubatizo wa Yesu. Ubatizo wa waumini kama ilivyo siku hizi una maana tofauti na ule ubatizo wa Yesu alioupokea katika mto Yordani. Hivyo imetupasa sisi sote kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu kwa kuamini ubatizo wa Yesu Kristo ambao alioupokea toka kwa Yohana na pia damu yake Msalabani. Ikiwa mtazamo wa Kanisa la kwanza uliweka kipaumbele juu ya hili kuwa ndilo Sakramenti muhimu, basi hili kwao waliona ndiyo egemeo la imani katika ubatizo wa Yesu na hivyo hata sisi leo hii tuchukulie ubatizo wa Yesu kwa Yohana kuwa ni sehemu isisyo epukika katika wokovu wetu.
Zaidi ya yote ni lazima tuufikie na kuikumbatia imani iliyo sahihi yenye ufahamu kamili ambayo husema kwamba Yesu ilimbidi asulubiwe kutokana na kubatizwa kwake na Yohana. Imetupasa
kuelewa kwamba Roho Mtakatifu huanza kuweka makazi ndani yetu pale tu tunapoamini ubatizo wa Yesu, kufa kwake msalabani na kufufuka kwake ili awe Mwokozi wetu. Ubatizo wa Yesu kwa Yohana na damu yake msalabani vyote vinamaana ya pakee katika Injili njema.
Njia ya tahadhari kwako katika kumpokea Roho Mtakatifu ni kuamini Injili njema ya ubatizo wa Yesu na damu yake. Ubatizo wa Yesu ulitakasa dhambi zote za wanadamu mara moja. Ulikuwa ni ubatizo wa ukombozi uliopelekea kwetu kumpokea Roho Mtakatifu. Kwa kuwa baadhi ya watu hawajagundua nguvu iliyomo katika ubatizo wa Yesu, basi wao huelewa hili kuwa ni kama sherehe ya kawaida.
Ubatizo wa Yesu hufanya sehemu muhimu katika Injili njema ambayo hutueleza namna ile Yesu alivyobeba dhambi zote za ulimwengu juu yake na hata kuikubali hukumu yake kwa kumwaga damu yake msalabani. Yeyote anayeamini maneno ya Injili hii iliyo njema hufanywa kuwa msharika wa Kanisa ambalo linamilikiwa na Bwana, na kufurahiya baraka ya Roho Mtakatifu.
Roho Mtakatifu ni karama toka kwa Mungu kwa wale wote waliokwisha kusamehewa dhambi zao. Kwa ubatizo wake, Yesu alikuwa “Mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu” kwa namna iliyotosha (Yohana 1:29). Katika Yohana 1:6-7 inasema “Palitokea mtu
ametumwa kutoka kwa Mungu jina lake Yohana. Huyo alikuja kwa ushuhuda ili ashuhudie ile nuru, wote wapate kuamini kwa yeye”. Ili kumwamini Yesu kuwa ni mwokozi wetu aliyechukua
dhambi zetu zote ni lazima tuelewe juu ya huduma ya Yohana na ushuhuda kama ilivyo andikwa katika Biblia. Ndipo tutaweza kumwamini Yesu Kristo kama Mwokozi wetu. Ili kuweza kumpokea Roho Mtakatifu pia tunahitajika kuwa na imani madhubuti iliyoshuhudiwa moyoni.
Hivyo kukamilisha Injili ya kweli iliyo njema ni lazima kuamini ubatizo wa Yesu kwa
Yohana na damu yake pale msalabani. Katika Mathayo 11:12 imeandikwa “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa Ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu na wenye nguvu wauteka”. Kifungu hiki husemekana kuwa ndicho kifungu kigumu kueleweka kati ya vifungu kadha katika Biblia. Hata hivyo imetupasa kuwa makini kwa sehemu isemayo “Tangu siku za Yohana Mbatizaji”. Hakika hapa inatangaza kwamba huduma ya Yohana ilikuwa iimeunganika moja kwa moja na huduma ya Yesu kwa wokovu wetu.
Yesu anatuhitaji tuingie katika Ufalme kwa ujasiri wa imani kama ulivyo ujasiri wa mwenye nguvu. Tunatenda dhambi kila leo, sisi ni dhaifu lakini ameruhusu tuweze kuingia katika Ufalme wake kwa imani, kifua mbele bila ya kujali udhaifu wetu. Hivyo kifungu hiki kina maana kwamba watu wataweza kuuteka Ufalme wa mbingu kwa imani katika Injili njema isemayo kwamba Yesu amefuta dhambi zote za ulimwengu kwa kupitia ubatizo wake kwa Yohana na damu yake msalabani. Kwa maneno mengine ina maana kwamba mbingu inawezwa kutekwa kwa imani madhubuti katika Injili hii njema ya ubatizo wa Yesu na damu yake.
Ubatizo wa Yesu ndiyo uliobeba dhambi zote na imani yetu juu yake hatupa uhakika kwamba tutapokea uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yetu. Lazima tuhubiri Injili hii kwa majirani zetu, ndugu zetu, wapendwa wetu na kwa yeyote Yule ulimwenguni. Lazima tuwe na imani katika Injili njema ambayo inasema kwamba dhambi zetu zote ulimwenguni zilitwikwa kwake Yesu kupitia ubatizo wake. Kwa kupitia imani yetu ndipo basi tutaweza kupokea tulizo la ukombozi na uwepo wa Roho Mtakatifu ndani. Kila mtu ataweza kuwa mwana wa Bwana ambamo ndani yake Roho Mtakatifu atakaa, kuwa moja kati ya kaka na dada kwa kuamini Injili njema ya maji na Roho. Ni lazima muwe na imani sawa katika Injili njema kama aliyokuwa nayo Paulo. Namshukuru Bwana kwa kutupa Injili njema na kumsifu yeye. Ameni.

Jumatatu, 7 Aprili 2014

WATU WA VIPAWA HUTENDA KAZI KWA KUWEKEA MIKONO!


Yatupasa kuwa mbali na imani ya aina hii. Baadhi ya watu siku hizi wanaimani potofu kwamba wataweza kumpokea Roho Mtakatifu ikiwa watawekewa mikono na wale waliokwisha kupokea nguvu hizo. Wao hudhani kwamba kwa kuwa maandiko yanasema kuwa watu wengi walimpokea Roho Mtakatifu waliposhuhudia kuwekewa mikono na Mtume, hivyo nao wataweza kufanya namna hiyo pia. Baadhi yao wanajisingizia kwa imani potofu za aina hii, wanadhani kuwa wataweza kuwapa wengine Roho Mtakatifu kwa kupitia kuwawekea mikono juu yao. Yatupasa kuwa makini na kuwepo kwa watu wa aina hii.
Hata hivyo yatupasa kuweka akilini kwamba imani za watu hawa zinautofauti mkubwa na zile za Mitume wakati wa kipindi cha Kanisa la mwanzo. Siku hizi jambo kuu lenye kuleta ubishani mkali katika imani za baadhi ya Wakristo ni kwasababu hawana imani katika Injili ya kweli ya maji na Roho kati yao. Wengi husema kwamba wanamwamini Mungu lakini hawakumweshimu na hivyo badala yake hujidanganya nafsi zao na zawenzao. Hata hivyo wenye dhambi kamwe hawatowezea kudanganya swala la kumpokea Roho Mtakatifu au hata kufanya wengine wadanganyike. Ikiwa mtu fulani atasema kwamba Roho amekuja juu yake yeye mwenye dhambi basi roho huyo hakuwa ni yule Roho Matakatifu kweli, bali badala yake ni roho wa shetani ajifanyaye kuwa Roho wa kweli.
Mitume wakati wa Kanisa la mwanzo walikuwa ni watu waliomjua na kumuamini Yesu Kristo kuwa ndiye mwokozi aliyechukua dhambi zote za wanadamu kupitia ubatizo wake alioupokea kwa Yohana na kifo chake msalabani. Waliweza kupokea Roho Mtakatifu kwa sababu waliamini ukweli juu ya ubatizo wa Yesu na damu yake pale msalabani. Pia walihubiri Injili ya maji na Roho kwa wengine hivyo kuweza kuwasaidia katika kuwaongoza kumpokea Roho Mtakatifu.
Lakini siku hizi Wakristo wengi wamempokea katika imani za kishabiki. Je ni kweli mwenye dhambi katika nyakati hizi ataweza kumpokea Roho Mtakatifu kupitia kuwekewa mikono
toka kwa mhudumu mwingine aliye na dhambi? Hakika hili halifikiriki. Wapo watu wanaosema kwamba ingawa wanadhambi moyoni, wamempokea Roho Mtakatifu ndani yao.
Hata ikiwa mtu anaonekana ni mchungaji mzuri machoni pa kundi lake kamwe hawawezi kumsababisha yeyote kumpokea Roho Mtakatifu  ikiwa yeye mwenyewe anadhambi moyoni.
Hii ndiyo sababu Manabii wengi wa uongo wameweza kuwaongoza watu kuelekea motoni. Yakupasa uelewe ukweli kwamba wale wote wenye kufundisha aina hii ya imani ni manabii wa uongo. Hawa ni watu ambao tayari wameshikiliwa na mapepo. Ikiwa mtu anadhambi moyoni, je, Roho Mtakatifu ataweza kukaa ndani yake? Jibu ni hapana. Jingine, je, itawezekana kwa mtu aliye na dhambi kuweza kusababisha mtu mwingine aweze kupokea Roho Mtakatifu? Kwa mara nyingine jibu ni hapana. Sasa basi nini kinacho sababisha watu wanao semekana kuwa na vipawa (karismatiki) katika nyakati hizi kuweza kufanya miujiza na maajabu katika ukristo huku wakiwa bado wanadhambi moyoni mwanao? Mapepo au roho chafu hufanya hivyo. Roho Mtakatifu kamwe hawezi kuishi ndani ya mwenye dhambi.
Yeye hukaa ndani ya wale tu walio na imani katika Injili ya maji na Roho. Je? wewe nawe unauhakika roho aliye ndani yako ni Roho Mtakatifu? Katika Yohana 3:5 Yesu alisema “Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia ufalme wa Mungu.” Kwa namna hii basi Roho Mtakatifu kuweka makazi ndani kutawezekana kwa wale tu watakao amini injili ya maji na
Roho. Kosa ambalo wakristo wengi wafanyalo nyakati hizi nikwamba, huamini kwamba mtu ataweza pia kumpokea Roho Mtakatifu ndani yake kwa kuwekewa mikono na mtumishi
mwenye dhambi. Hili nikosa kubwa na la hatari. Nyakati hizi, wakristo wengi na watumishi wao wanaimani na dhamiri zao kwamba, kuwa na Roho Mtakatifu ndani ya mtu huja kwa kupitia kuwekewa mikono.
Uhusiano kati ya ondoleo la dhambi la kweli na tendo la kuwekea mikono.
“Kuwekea mikono” ni namna ambayo mtu huweza kutwikwa au kutoa kitu alicho nacho juu ya kitu kingine. Kwa mfano, ikiwa tutazungumza katika kipaza sauti, sauti hiyo husafiri kupitia waya toka kipaza sauti na kutokea upande wa pili kwa sauti kubwa zaidi katika spika ili kila mtu aweze kusikia. Ndivyo pia katika Agano la kale pale mwenye dhambi alipoweka mikono yake juu kichwa cha mnyama wa sadaka na hivyo kusamehewa. Kwanjia hiyo pia, nguvu ya Mungu
huwekwa juu ya mtu kwa mtu kwa tendo la kuwekewa mikono toka kwa mtumishi wake. Hivyo tendo la kuwekea mikono limechukua maana ya “kuhamisha, kutwika”.
Watu wanaojiita ni wenye vipawa (wanakarismatiki) hawawezi kamwe kusababisha mtu kuweza kuwa na Roho Mtakatifu ndani yake kwa njia ya kuwekea mikono, badala yake kusababisha watu hao kupokea roho chafu. Lazima ukumbuke kwamba mtu aliye na nguvu za roho chafu huamisha roho hizo kwa wengine kupitia tendo la kuwekea mikono. Mtu aliye tawaliwa na mapepo anapoweka mikono juu ya kichwa cha mwingine, pepo lililomo ndani yake huingia ndani ya mtu huyo kwa sababu shetani hutenda kazi kupitia wenye dhambi.
Kwasababu hiyo basi kila mtu imemlazimu kuamini injili ya maji na Roho ikiwa anataka kupokea Roho Mtakatifu ndani yake. Shetani hutawala wale wote walio na dhambi hata ikiwa
wanamwamini Yesu, huku wakiwa wameshindwa kupokea ondoleo la dhambi.
Ikiwa mtu atapokea tendo la kuwekewa mikono toka kwa mtu aliye na mapepo, mapepo hayo yatahamia juu yake mtu huyo, hivyo naye pia moja kwa moja ataweza kufanya miujiza ya uongo. Yatupasa kujua kwamba mapepo huja na kufanya makazi ndani ya mtu kwa kupitia tendo la kuwekewa mikono.
Na kumpokea Roho Mtakatifu ndani huwezakana tu kwa imani katika injili ya maji na Roho.
Tendo la kuwekea mikono ni njia mahususi iliyo wekwa na Mungu katika kutwika kitu juu ya kingine. Lakini shetani husababisha watu wengi kupokea roho chafu kwa kupitia tendo hilo. Ukweli ni kwamba watu wengi nyakati hizi hujaribu kununua nguvu za Roho Mtakatifu kwa fedha na hivyo kufanya tatizo hili kuwa kubwa zaidi.
Wakristo wengi wanaufahamu wa kimakosa juu ya ukweli wa kuwa na Roho Mtakatifu ndani. Tulipouliza kwa namna gani wataweza kumpokea Roho Mtakatifu ndani yao, wengi wa watu
hujibu kwamba inawezekana kwa kupitia sala za toba na kufunga. Hili si kweli kabisa. Je, nikweli Roho Mtakatifu huja juu yako pale unapo fanya maombi maalumu kwa Mungu?
Hapana kuweza kuwa na Roho Mtakatifu ndani yako huja kwa wale tu wanao amini injili ya maji na Roho. Kwa kuwa Mungu ni kweli ameweka sheria kwa ajili ya kuweza kupokea Roho Mtakatifu ndani. Je, Roho Mtakatifu ataweza kuwa ndani ya mtu aliye na dhambi moyoni? Jibu bila shaka hapana. Mtu hawezi kumpokea Roho Mtakatifu kupitia tendo la kuwekewa mikono. Hata ikiwa mtu atahudhuria mikutano ya uamsho na maombi ya uchungu kwa Mungu ili aweze kupokea nguvu ya Roho Mtakatifu, Roho Mtakatifu atabaki kuwa mbali naye. Wenye dhambi hakika hawatoweza kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu ndani yao. Wenye dhambi wataweza kupokea kipawa hicho cha Roho Mtakatifu ikiwa tu watapokea ondoleo la dhambi kwa kuamini Injili ya maji na Roho.
Yeyote asiyefahamu injili ya maji na Roho, kamwe hatoweza kumpokea Roho Mtakatifu. Siku hizi injili ya maji na Roho imeenea kwa kasi kupitia vitabu, mikutano ya makanisa, tovuti na hata vitabu vya kielectronikali ulimwenguni pote. Hivyo, yeyote anayetafuta ukweli wa injili, ataweza kuamini hili na kuweza kumpokea Roho Mtakatifu ndani yake. Ikiwa bado hujampokea, yakupasa uelewe kwamba ili uweze kumpokea ni lazima uamini injili ya maji na Roho.

JE, INAWEZEKANA MTU KUMNUNUA ROHO MTAKATIFU KWA UWEZO WAKE?


(Metendo 8:14–24 )
“Na Mitume waliokuwako Yesuramu, waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu wakawaombea wampokee Roho Makatifu kwa maana bado hawajawashukia
hata mmoja wao ila wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu. Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho Mtakatifu. Hata Simoni alipoona ya kuwa watu wanapewa Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono ya Mitume akataka kuwapa fedha akisema, nipeni na mimi uwezo huu ili kila mtu nitakaye mwekea mikono yangu apokee Roho Mtakatifu. Lakini Petro akamwambia fedha na ipotelee mbali pamoja nawe kwa kuwa umedhania ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali. Huna fungu wala huna sehemu katika jambo hili, kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele za Mungu. Basi, tubia uovu wako huu ukamwombe Bwana ili kama yamkini usamehewe fikira hii ya moyo wako. Kwa maana nakuona u katika uchungu kama nyongo, na tena u katika kifungo cha uovu. Simon akajibu akasema, niombeeni ninyi kwa Bwana yasinifike mambo haya mliosema hata moja.”

Husika na somo kuu katika kifungu hiki, napenda kuleta ujumbe huu iwapo “mtu anaweza kumpokea Roho Mtakatifu ndani yake kwa kupitia juhudi binafsi”. Mitume katika nyakati
hizo za Kanisa la kwanza waliweza kupokea nguvu toka kwa Mungu na kutumwa sehemu kadhaa naye. Yapo matendo ya miujiza kadhaa katika Kitabu cha Matendo, mojawapo likiwa
kushuka kwa Roho Mtakatifu juu ya waumini pale Mitume walipowawekea mikono. Biblia inasema “Mitume walipowawekea mikono wale ambao hawakuwa wamempokea
Roho Mtakatifu ingawa walikwisha mwamini Yesu, walipokea Roho Mtakatifu.”

Sasa basi, ni kwa namna gani walimpokea Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono? Kwa wakati huo maneno ya Mungu bado yalikuwa yakiendelea kuandikwa na hivyo basi kazi ilikuwa bado haijakamilika hivyo Mungu aliwapa Mitume nguvu za pekee kuweza kufanya kazi zake. Alikuwa pamoja na Mitume na kuweza kuleta miujiza mingi na maajabu kupitia kwao. Kilikuwa ni kipindi pekee, wakati Mungu alipofanya maajabu na miujiza ambayo iliweza kuonekana kwa macho ya wanadamu ili kuweza kuwafanya watu waweze kumwamini Yesu Kristo kuwa kweli ni mwana wa Mungu na ndiye mwokozi. Palikuwepo na umuhimu kwa Mungu pamoja na
Mitume kwa nguvu za ajabu kuweza kuonyesha kazi ya Roho Mtakatifu ili kuthibitisha kwamba Yesu Kristo ndiye Mungu na kwamba ndiye Mwana wa Mungu Mwokozi. Ikiwa Roho Mtakatifu asingefanya kazi kupitia miujiza na maajabu kwa nyakati hizo za kanisa la kwanza hakika pasingekuwepo na yeyote awezaye kumwamini Yesu kuwa ni Mwokozi.

Hata hivyo hakuna umuhimu tena kwetu sisi leo hii kumpokea Roho Mtakatifu kupitia miujiza na maajabu ya kuonekana kwa macho ya kawaida kwa sababu Biblia imekamilika. Badala yake sasa, kuwa na Roho Mtakatifu ndani yetu kunategemea imani zetu zaidi. Kwa maneno mengine ni kuamini Injili ya kweli. Mungu ametupatia Roho Mtakatifu awe ndani yetu kwa wale tu watakao kuwa na imani ya Injili ya kweli mbele ya Mungu. Kuwa na Roho Mtakatifu ndani hutokea kwa wale tu wanao amini maneno ya Mungu kama ilivyo timia kwa kuja kwake Yesu hapa ulimwenguni na kwa ubatizo wake na damu yake.

Nyakati hizi wachungaji wengi hufundisha waumini wao kwamba matendo yasiyo ya kawaida yawezayo kuonekana kwa macho ndiyo ishara tosha ya kuwa na Roho Mtakatifu. Hivyo
kuwaongoza waumini kumpokea Roho Mtakatifu kwa njia hiyo. Huwapotosha watu kwa kuwapa mafundisho ya uongo kama yale ya kunena kwa lugha kuwa ndiyo ishara ya kushukiwa na Roho
Mtakatifu. Wachungaji hawa hujiona kuwa wao ndiyo mitume watendao miujiza na maajabu makuu na hivyo kuvutia washabiki wa kidini ambao hutaka kumjua Mungu kwa hisia zao.

Ushabiki huu umeenea kwa Wakristo walio wengi duniani pote na wengi wao hufuata imani hizo na hatimaye kupatwa na roho za kishetani kwa kupitia njia za nguvu za giza. Hata leo, watu hao waliokumbwa na ushabiki wa aina hii hudhani kuwa nao wataweza kuwafanya wenzao kuweza kumpokea Roho Mtakatifu kupitia kuwekewa mikono.

Hata hivyo kwa jinsi Simoni alivyo potoka, nao huwa kama wachawi wanaonekana katika kifungu hicho. Wameharibiwa kwa kujikonga nafsi zao na tamaa ya mwili lakini matendo yao
yote huleta tafrani katikati ya watu. Aina hii ya mafundisho ya uongo hupindisha njia ya kweli katika kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu mbele ya Mungu.

Hata leo, wengi wa mitume waongo hufanya kazi za ibilisi kupitia mambo yasiyo sahihi ya kidini, wakijifanya kutenda kazi za Roho Mtakatifu. Wakristo walio wa kweli ni lazima
walishike neno la Mungu ambalo ndiyo ufahamu pekee wa kuweza kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu ndani. Wale wote wanaojifanya kuwa ni Wapentekoste, ambao husisitizia mwonekano wa nje kimwili nilazima waache imani hizi potofu wayarejee maneno ya Mungu na kuamini ukweli ambao kwa hakika utawaongoza katika kumpokea Roho Mtakatifu ndani yao.

Simoni alikuwa mchawi maarufu Samaria katika nyakati hizo. Baada ya kuwaona mitume wa Yesu wakisababisha watu kumpokea Roho Mtakatifu, alitamani kumnunua Roho Mtakatifu kwa fedha. Watu wa imani ya aina hii bila shaka huishia kuwa watumwa wa ibilisi wakitumiwa kutenda kazi zake. Simoni alitaka kumpokea Roho Mtakatifu lakini tama zake zilikuwa si nyingine bali ni kujipatia kipato binafsi.

Tunaweza kuona aina hii ya imani siyo yakupelekea kumpokea Roho. Simoni alijaribu kumnunua Roho Mtakatifu kwa fedha kwasababu ya uchoyo ulio tokana na kutamani nguvu za Roho Mtakatifu. Alikemewa vikali na mtumishi wa Mungu Petro. Ingawa ilisemekana kwamba Simoni alikuwa akimwamini Yesu hakuwa ni mtu kamwe aliyekuwa amempokea Roho Mtakatifu kupitia ondoleo la dhambi. Kwa maneno mengine yeye alidhani
ya kwamba angeweza kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yake kwa kutoa mali za kidunia kwa Mungu.

Ingawa muonekano wake wa nje ulionyesha kwamba alikuwa akimwamini Yesu, mawazo yake halisi ndani yalikuwa hayawiani na maneno ya Yesu. Badala yake alijawa na tamaa za kimwili. Petro aliye yagundua mawazo ya Simoni alimkemea kwa kuwa alijaribu kutaka kumpokea Roho Mtakatifu ambaye ni zawadi ya Mungu kwa fedha. Alimtaadharisha Simoni kwamba angeweza kuangamia na fedha hizo zake.

Nyakati hizi mitume waongo walio tawaliwa na roho za ibilisi hunena kwa kuwalaghai watu kwa kuwafanya kudhani kwamba miujiza na maajabu yote ni kazi za Roho Mtakatifu. Tunaweza kuona mara nyingi watu wakifurahia aina hizi za nguvu na kuomba kwa dhati nao waweze kumpokea Roho Mtakatifu. Hata hivyo mtu imempasa kuwa makini kwamba hapana yeyote utakaye mpokea Roho Mtaktifu ndani yake kupitia maombi yaliyo na tamaa za kidunia.
Je, wapo pia watu wa uamsho wa vipawa (karismatiki) kati yako kwa nafasi yoyote? Imekupasa uwe mwangalifu dhidi ya watu wa aina hii.

Huwafata watu kwa imani hizi za mashamshamu na kishabiki. Husema kwamba wanaweza
kukemea mapepo na hata kuweza kuwafanya watu kumpokea Roho Mtakatifu kupitia kuwawekea mikono. Hata hivyo watu hawa huwa na nguvu ambazo si za Roho Mtakatifu bali ni
nguvu za pepo wachafu. Wale wanaodai kumpokea Roho Mtakatifu kwa njia ya kuwekewa mikono hujiongoza wao binafsi na wengie katika kumpokea roho chafu.

Kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu huja kwa sisi wote tu, tunaoamini maneno ya maji na Roho (1 Yohana 5:3-7). Ingawa injili ya maji na Roho imeandikwa kwa uwazi katika Biblia, bado watu walio wengi hudhani mioyoni mwao kwamba wataweza jaribu kumfikia Mungu kwa kupitia nguvu za miujiza na kwa hali za kupumbaza, kunena kwa lugha, maono na kukemea pepo. Na ndiyo maana manabii waongo wameweza kuwadanganya watu wengi katika kuamini mazingaombwe ya Kikristo yatokanayo na ibilisi mwovu.


Petro alimkemea Simoni kwa kumwambia, “Fedha yako na ipotee mbali pamoja nawe, kwa kuwa umedhania kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali. Huna fungu wala huna sehemu katika jambo hili. Basi tubia uovu wako huu ukamwombe Bwana ili kama yamkini usamehewe fikra hii ya moyo wako. Kwa maana nakuona u katika uchungu kama nyongo na tena u katika kifungo cha uovu.” Yatupasa kujawa na simanzi kwa sababu leo hii wapo watumishi wa aina hii. Wengi wao ni wale wajiitao wenye vipawa au wakarismatiki. Hudai fedha kwa makundi yao. Tuwe mbali sana nao na watu wa imani hizi na tumpokee Roho Mtakatifu ndani yetu kwa Injili ya kweli katika maji na Roho (Mathayo 3:15, 1 Petro 3:21, Yohana 1:29, Yohana 19:21-23).

Jumapili, 6 Aprili 2014

NJIA SAHIHI YA KUMPOKEA ROHO MTAKATIFU – 2


Sehemu ya pili
Roho Mtakatifu aliwashukia Wafuasi wa Yesu ghafla toka Mbinguni!
“Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja”(Matendo 2:1). Wafuasi wa Yesu walikusanyika wakisubiri kutimia kwa ahadi ya Mungu kumtuma Roho Mtakatifu. Ndipo Roho Mtakatifu alipokuja juu yao. “Kukaja ghafla kutoka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kwa kasi ukaijaza nyumba yote waliokuwa wameketi. Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliwakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka” (Matendo 2:2-4).
Roho Mtakatifu alishuka “ghafla kutoka mbinguni” hapo neno “ghafla” maana yake kulifanyika si kwa kupitia mapenzi ya Mwanadamu. Kwa nyongeza tafsiri ya “toka Mbinguni” inaweza kuelezwa mahali Roho Mtakatifu alipotoka, na pia kuondoa mawazo kwamba ujazo wa Roho Mtakatifu ndani ya mtu hutokana na mapenzi yake au juhudi. Tafsiri “Toka mbinguni” inatuonyesha kwamba, kusema Roho Mtakatifu anaweza kupatikana kwa kupitia maombi ni hoja za kitapeli. Kwa maneno mengine, kusema kwamba Roho Mtakatifu alishuka ghafla toka mbinguni maana yake kuwa na Roho Mtakatifu ndani hakutokei kwa kupitia namna za kidunia kama vile kunena kwa lugha au kujitoa nafsi. Wafuasi wa Yesu walinena kwa lugha hapo awali katika kuhubiri Injili njema kwa watu wa mataifa yote.
Sababu ya hili ni kuwa aliwawezesha kuhubiri Injili kwa lugha za kigeni toka ile ya Kiyahudi kwa msaada wake. Watu toka Mataifa yote waliweza kusikia wafuasi hao wakinena kwa lugha zao ingawa wengi wa wafuasi hawa walitokea Galilaya. “Kukawatokea ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu wakaanza kusema kwa lugha nyingine kama Roho alivyowajalia kutamka…” (Matendo 2:3-4). Hapa ni lazima kuwa makini zaidi tunapoona tafsiri, Roho Mtakatifu “kuwakalia kila mmoja wao”. Wafuasi walisubiri kuja kwa Roho Mtakatifu mahali pamoja wakiwa tayari wamekwisha kuamini Injili ya kuzaliwa upya mara ya pili katika maji na Roho.
 Wakristo wengi nyakati hizi huelewa vibaya sehemu hii ya kifungu, wakiamini ya kwamba ujio wa Roho Mtakatifu hutokea kwa sauti kama ya upepo uvumao wanapokuwa kwenye maombi. Hata hivyo hili ni jambo potofu kuhusiana na Roho Mtakatifu litokanalo na upumbavu na kuchanganyikiwa. Je, Roho Mtakatifu hufanya sauti pindi anaposhuka juu ya watu? Hapana, hakika hafanyi.

Kile watu wanachosikia ni sauti ya shetani afanyayo pale anaposhambulia roho za watu. Hufanya sauti hizi pale anapofanya mazingaombwe, sauti za kunongoneza na miujiza ya uongo katika juhudi za kuwaingiza watu katika kuchanganyikiwa kwa kusingizia kuwa ni Roho Mtakatifu. Watu wengi hupokea kwa kudhani mambo haya yote ni ishara na ushuhuda wa kushuka kwa Roho Mtakatifu. Pia hudhani kwamba Roho Mtakatifu huja kwa sauti kama ya “Shwuihhh….” Kama ya upepo mkuu. Wanadanganyika na mapepo. Kuja kwa Roho Mtakatifu kama ilivyoandikwa katika Matendo alikuja kwa kupitia imani katika Injili njema tu.
Imani ya Petro (1 Petro 3:21) ilikuwa ni sahihi kumwezesha kupokea Roho Mtakatifu ndani yake.
Kwa kuweka bayana tukio la kwanza la Pentekoste katika Matendo 2, Mungu anataka kuweka msisitizo wa ukweli kuwa Roho Mtakatifu alishuka juu yao kwa sababu walikuwa tayari wamekwisha amini Injili ya maji na Roho. Lakini watu mara nyingi hudhani Pentekoste ni wakati ule Roho Mtakatifu anaposhuka toka mbinguni kwa ishara zisizo za kawaida na tafrani za makelele. Na ndiyo maana nyakati hizi katika mikutano ya uamsho inaaminika kwamba mtu aweza kupokea Roho Mtakatifu kupitia sala za kurudia rudia, kufunga kula au kuwekewa mikono. Matukio yasiyo ya kawaida kama vile kuwa na mapepo, kuanguka bila fahamu, kukosa fahamu kwa siku kadhaa au kutetemeka bila kujizuia hizi si kazi za Roho Mtakatifu.
Roho Mtakatifu ni nafsi iliyo na utashi kamili na kamwe haidharau utu wa mwanadamu. Roho Mtakatifu hana tabia ya kumdhalilisha mtu kwa sababu yeye ni nafsi ya Mungu aliye na utashi akili na hisia. Huja juu ya watu pale tu wanapoamini maneno ya Injili ya maji na Roho (Matendo 2:38). Petro alishuhudia kwamba Roho Mtakatifu alikuja juu ya wafuasi kama ilivyo tabiriwa na Nabii Joeli. Ilikuwa ni kutimizwa kwa ahadi ya Mungu iliyo sema kwamba Roho Mtakatifu atawashukia wale wote watakao pokea ondoleo la dhambi. Kwa maneno mengine kuwa na Roho Mtakatifu ndani huja kwa wale wanaoamini ukweli kuwa Yesu alibatizwa na Yohana na kusulubiwa ili kuwaokoa wanadamu na dhambi zao. Hotuba ya Petro ukijumuisha na unabii wa Yoeli, hutuonyesha kwamba yatupasa kujua kwanini Yesu alibatizwa, na kwa nini imetulazimu kuamini hili. Kwa kujua ukweli huu ndipo kunako pelekea Wakristo kumpokea Roho Mtakatifu.
Je, unaamini Injili hii njema ambayo Petro anayoshuhudia? (1 Petro 3:21) au bado wewe unaamini upuuzi na mazingaombwe ya imani zisizo na umuhimu kinyume na Injili njema? Je, unajaribu kumpokea Roho Mtakatifu kwa kupitia juhudi zako kwa kuweka kando mpangilio wa Mungu? Hata ikiwa mtu atamwamini Mungu na kufanya maombi ya toba kwa
matumaini ya kutakaswa dhambi zake hakuna njia nyingine ya kuweza kumpokea Roho Mtakatifu zaidi ya kuamini injili ya majina Roho. Je, bado unasubiri kumpata Roho Mtakatifu ndani yako huku ukiwa huna ufahamu wa injili ya maji na Roho? Je, wajua maana halisi ya ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani ambayo hupelekea Roho Mtakatifu kuja ndani ya moyo wako? Ni lazima ujue kwamba Roho Mtakatifu kuweza kuwa ndani yako kunawezakana ikiwa tu unapoamini injili ya maji na Roho. Ukweli wa Roho Mtakatifu kuwa ndani yako unawezekana kwa wote wale watakaoamini Injili ya maji na Roho.
Tunamshukuru Mungu kwa kutupatia Injili yake ya maji na Roho ambayo ndiyo pekee ituwezeshayo kumpokea Roho Mtakatifu ndani yetu.

Ijumaa, 4 Aprili 2014

NJIA SAHIHI YA KUMPOKEA ROHO MTAKATIFU – 1


Sehemu ya kwanza
Je unafahamu juu ya Injili iwezayo kukupatia Roho Mtakatifu? Ikiwa unataka kumwomba Mungu kumpokea Roho Mtakatifu, ndipo basi kwanza yakupasa kupata ufahamu halisi juu ya hili na kuwa na imani nalo. Sasa basi, nini kilicho muhimu katika kuhitimu kumpokea Roho Mtakatifu? Ni kutakaswa dhambi zako zote kupitia Injili njema ya maji na Roho (inapatikana katika blog hii). Ni pale tu utakapokubali juu ya ufahamu huo, ndipo utatakapompokea Roho Mtakatifu.
Katika jamii ya leo, watu wengi hawaelewi ukweli wa Injili ya maji na Roho, na wanateseka chini ya makosa ya kihisia wanayo pandikizwa na walimu waongo. Watu hao hukusanyika katika kile kinachoitwa mikutano ya uamsho huku wakipiga makofi kwa furaha ya mashamushamu. Mhubiri anapokuwa jukwaani akiimbisha mapambio huku akiwaasa watu kutubu katika Mikutano ya aina hii ambayo mara nyingine huwa katika hali ya mashamushamu, watu hupiga makelele na kuita “Bwana!” na kurudia hata zaidi ya mara tatu wakimwomba Mungu ujazo wa Roho Mtakatifu hadi sauti kukauka.
Wale wote wenye kuhudhuria mikutano kama hii hujifanya kulia wakati wote badala ya kufanya maombi. Hali inapo fikia kilele katika tafrani hii watu hupiga makelele na mayowe hadi kuzimia. Hata hivyo mhubiri aliye jukwaani au madhabauni huweka kipaza sauti karibu kabisa na mdomo wake na kufanya sauti kama upepo upulizao huku akiwaongoza watu katika kina cha mashamshamu ya kidini. Ndipo huaza kuomba kwa kunena kwa lugha huku akiruka ruka na kuanza kuwawekea mikono watu juu ya vichwa vyao. Baadhi yao huanza kunena kwa lugha , na wengine huanguka kwa nguvu ghafla sakafuni na kuzimia.
Watu wengi huvutiwa na mzuka huu wa kidini huku wakitumaini kumpokea Roho Mtakatifu. Huamini kwamba wataweza kumpokea Roho Mtakaatifu kwa kufikia hali ya kiwango cha juu cha mfadhaiko na mzuka wao. Lakini haya yote hutokana na shetani.
Kwa kuchunguza mambo haya namengine ya aina hii tunaweza kuwaona wakristo wanyakati hizi wamepatwa na ugonjwa ambao utaweza kuelezeka kuwa ni “Uamsho wa Wapentekoste” (the pentecostal-Charismatic Movement) au Upentekoste wa kileo (Neo Pentecostalism) ambao umetokana na dini ya Kishama (shamanism). Kwanini basi wanapatwa na ugonjwa huu wa mzuka? Kwa sababu wamekataa ukweli ambao hunena kwamba, imewapasa kumpokea Roho Mtakatifu kwa kuamini injili njema ya maji na Roho tu.
Aina hii ya vuguvugu ya uamsho katika dini za nyakati hizi yametapakaa duniani pote na Wakristo walio wengi wamechanganyikiwa kwa sababu hawawezi kujua ni ipi kazi ya Roho Mtakatifu na ile ya mapepo.
Roho Mtakatifu Hufanya kazi kupitia ahadi ya Neno la Mungu
( Matendo 1:4-8 )
“Hata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kwangu; ya kwamba Yohana aliwabatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada siku hizi chache. Basi walipokutanika, wakamwuliza, wakisema Je? Bwana wakati huu ndipo unapowarudishia Israeli ufalme? Akawaambia si kazi yenu kujua nyakati wala majira Baba aliyo weka katika mamlaka yake mwenyewe. Lakini mtapokea nguvu, akisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu na katika Uyahudi yote, na Samaria nahata mwisho wa nchi.”
Roho Mtakatifu hukaa ndani ya mioyo ya walio zaliwa upya ambao dhambi zao zote zimesamehewa kwa kuiamini Injili ya maji na Roho. Punde, anapo kuja juu ya mtakatifu, hufanya makazi ndani yake milele na kamwe hatomwacha peke yake kadiri atakapo endelea kuamini Injili. Humpa ushawishi mtakatifu huyo, katika kumwongoza kuelekea mapenzi ya Mungu, kumwongoza katika Biblia, humpatia nguvu ili kushinda majaribu na taabu anazokutana nazo hapa ulimwenguni, na humfanya azae matunda ya Roho kwa wingi. Mungu huutukuza mwili wa mtakatifu ukiwa ni hekalu lake kupitia kuweka makazi ya Roho Mtakatifu (Matendo 2:38-39, Yohana 14:16, 16:8-10, 1 Korintho 3:16, 6:19, Wagalatia 5:22-23).
Wakristo walio wengi hujaribu kumpokea Roho Mtakatifu kwa namna ile alivyo washukia wafuasi wa Yesu katika siku ile ya Pentekoste. Wapo baadhi ya watu wamepata vitita vya fedha kwa kutumia njia hii. Hujidai kwamba Roho Mtakatifu ni kitu fulani kinachoweza kupatikana kupitia juhudi ya mtu binafsi.
Hutamani kuona maono, kutenda miujiza, kuisikia sauti ya Yesu, kunena kwa lugha, kuponya magonjwa na kukemea mapepo. Hata hivyo ndani yao huwa na dhambi mioyoni na wapo katika msukumo wa roho za shetani (Waefeso 2:1-2).
Hata leo hii watu wengi bado wanaendelea kuishi pasipo kujua kwamba wapo chini ya nguvu za roho wa shetani. Hiki ndicho chombo na ulaghai wa shetani anao tumia dhidi ya watu kwa kutumia kila aina ya njia kama vile miujiza na maajabu ambayo hakika ni kiini macho tu. Yesu aliwaagiza wafuasi wake wasitokeYerusalamu, bali waingoje ahadi ya Baba (Matendo1:4). Kupokewa kwa Roho Mtakatifu kunakofunuliwa katika Matendo si kwakupitia “mazoea”, “kujitoa” au “sala za toba” bali kupitia kungojea ahadi ya Baba kumleta Roho Mtakatifu kwao.
Kile tunacho paswa kujifunza kutoka katika ujumbe huu ni kwamba, uwepo wa Roho Mtakatifu ndani ya mtu hautegemei kupitia maombi ya dhati afanyayo. Hii ni karama ya Mungu ambayo itaweza kupatikana pale tu kupitia imani kamili katika Injili njema ya maji na Roho ambayo Baba Mungu na Yesu Kristo aliyowapa wanadamu. Uwepo wa Roho Mtakatifu ndani ya mtu hutokea kupitia imani ya Injili ambayo Yesu kristo ametupatia. Mungu ametupa ukweli wa maji na Roho ili kwamba tuweze kumpokea Roho Mtakatifu ndani yetu (1 Yohana 3:3-5). Neno “ahadi ya Roho Mtakatifu” hutokea mara nyingi katika Agano Jipya. Petro anaongelea katika mahubiri yake (Matendo 2:38-39) juu ya ubatizo wa Roho Mtakatifu katika siku ya Pentekoste. “Ni ahadi ya Mungu kutupatia Roho mtakatifu kwa wale walio pokea msamaha wa dhambi kutokana na kuamini injili njema.”
Roho Mtakatifu ni kipawa kilichomo ndani ya wale wote walio pokea msamaha wa dhambi zao na kujumuisha maana ya kutimia kwa ahadi ya Mungu. Roho Mtakatifu katika Agano Jipya si kitu kinachoweza kupatikana kupitia makubaliano kati ya Mungu na watu bali ni ahadi ya zawadi toka kwa Mungu. Hivyo Roho Mtakatifu ndani ya mtu kama ilivyoanishwa katika matendo sio kitu kinachoweza kupatikana kupitia maombi (Matendo 8:19-20).
Roho Mtakatifu huja juu ya wale wote wanaoamini Injili ya maji na Roho ambayo Yesu aliyotupatia. Yesu aliwaahidi Wanafunzi wake kumtuma Roho Mtakatifu ili kwamba waweze kuwa naye ndani yao. “Yohana aliwabatiza kwa maji bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache” (Matendo 1:5). Kwa kuangalia imani za hawa walio katika Biblia ambao walipokea uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yao, tunagundua kwamba haya yalitokea si kwa kupitia juhudi zao bali kwa mapenzi ya Mungu. Uwepo wa Roho Mtakatifu ndani ya wafuasi hao katika Matendo haukutokea kwa msingi wa juhudi za kibinamu au maendeleo ya kiroho. Kuja kwa Roho Mtakatifu punde juu ya wafuasi wa Kristo kama ilivyoandikwa katika Matendo kulitokea kweli.
Hivyo Mitume wake walisubiri kutimia kama vile Yesu alivyosema “siyo siku chache kuanzia sasa”. Hii ndiyo iliyokuwa baraka ya kwanza katika kipindi cha Kanisa la kwanza. Kwa kuchunguza maandiko tunaweza kuona ahadi ya Mungu iliweza kutimia si kwa kupitia kufunga, maombi au kujitolea nafsi bali kupitia imani katika Kristo Yesu. Baada ya Yesu kupaa, waumini walimpokea Roho Mtakatifu kwa wakati mmoja.


IMANI KATIKA MSAMAHA WA DHAMBI


Tunaamini kuwa Mungu pekee ndiye anayeweza kuondoa dhambi kwa njia ya Injili ya maji na Roho.( Isaya 1:18) inasema, “haya, njooni, tusemezane, asema Bwana’, dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theruji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu”. katika (1 Yohana 1:9) tunasoma  “Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.” Hapa ni lazima tutambue kwamba “tukiziungama dhambi zetu” haimaanishi kuwa Mungu hutusamehe dhambi tukitoa sala za toba. Katika 1Yohana 1:9 ina maana, tunapokea ondoleo la dhambi pale tunapokiri kuwa tuna dhambi mbele za Mungu na kuamini kuwa Mungu tayari amekwisha safisha dhambi za dunia kwa njia ya ubatizo alioupokea kutoka kwa Yohana na damu yake msalabani.
Dhambi hapa ni ipi?
Yeyote aliyezaliwa katika uzao wa Adamu ana dhambi. Hivyo hakuna hata mmoja anayeweza kudai kuwa hana dhambi, ile kuwa wandamu, tumezaliwa katika hali ya dhambi, tayari tuna dhambi hata kama hatutendi dhambi. Hii inamaanisha kuwa kila mmoja anahitaji mkombozi anayeweza kumkomboa kutoka dhambini. Wale wanaodai kutokuwa na dhambi na kutokuona umuhimu wa kumwamini Yesu huishia kusimama kinyume na Mungu. Hapo mwanzo, Mungu aliumba dunia na mbingu, alitengeneza bustani ya Edeni na akamruhusu Adamu na Hawa kuishi humo. Katika dunia hiyo ambayo ilikuwa haina dhambi kabisa, mahusiano ya Mungu nao yalikuwa makubwa. Lakini kuwafanya kuwa watoto wake Mungu aliwapa sheria. Sheria hii ilikuwa ni ya kutokula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Mungu alimwambia, “Siku mtakayokula matunda hayo hakika mtakufa” Na ili kuwapa baraka na uzima wa milele, Mungu aliwaambia kula matunda ya mti wa uzima. Lakini badala ya kula matunda ya mti wa uzima kama Mungu alivyowaagiza, walikula mti wa ujuzi wa mema na mabaya, mti ambao ungewaletea mauti (mwanzo 2:17, 3:22).
Kutumbukia katika majaribu ya shetani, Adam na Hawa waliishia kula matunda yaliyozuiliwa, matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Mauti ilikua kama mshahara kwa dhambi hiyo. Ndio sababu (warumi 5:12) inasema “kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi.” Kwa kifupi ndio sababu wanadamu wanahitaji mwokozi. Watu wengine wanajiamini, kama yule kijana tajiri katika mathayo 19, hujiamini kuwa wameshika amri zote za Mungu tangu utoto, lakini hakuna mwanadamu yeyote aliyezitunza amri zote 613 za Mungu.
 Kwa nini Mungu alitupa sheria ambazo hatuwezi kuzizingatia kabisa? Biblia inasema kuwa kwa sababu ya kuwepo kwa sheria, tumeitambua dhambi (warumi 3:20) Amri kumi ambazo Mungu alitupa zinatuonyesha dhambi. Kwa mfano, mtu anaweza kumchukia mzazi wake, akisema Rohoni mwake “mzee yule ni mjeuri” mtu huyo tayari amekwisha vunja sheria au amri ya tano ya Mungu. Na mtu yeyote akimtamani mwanamke, hata kama asipofanya naye uzizi, tayari amekwishavunja mari ya saba Mungu pia anahesabu tama, uchoyo, wivu, chuki kuua hata kama hatujamuua mtu, kwani matendo haya ndiyo yanayosababisha watu kuuana. Ni nani sasa anayeweza kuzitunza amri za Mungu bila kuzipaka madoa katika ufahamu wa kawaida?
Pia katika (Yakobo 2:10) tunasoma “maana mtu awaye yote, atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika Neno moja, amekosa juu ya yote.” kwa mwanga huu, ni nani atasema hana dhambi mbele ya hii sheria kali ya Mungu?
Katika madhaifu yetu daima tunaanguka dhambini. Kwa nini jambo hili? Ni kwa sababu ile dhambi yetu ya asili, wanadamu kwa asili ni wenye dhambi. Ndio sababu Daudi alitubu kwa kuvunja amri ya saba, kama inavyoonekana katika zaburi 51:5 “Tazama mimi naliumbwa katika hali ya uovu; mama yangu alinichukuwa mimba hatiani.” Daudi kwa maneno mengine alikiri dhambi hiyo ya msingi. Sala za toba zinazotolewa siku hizi za wakristo wa kawaida na ukiri wa Daudi juu ya dhambi ni tofauti sana. Kale walijutia dhambi ile tu mtu aliyoitenda, wakati za siku hizi, kinyume chake mtu hujiona hawezi kujisaidia mwenyewe kwa sababu ya dhambi ya asili. Wale tu wanaotambua dhambi zile za asili na kuamini Injili ya maji na Roho ndio wanaoweza kupata neema ya ondoleo la dhambi kutoka kwa Mungu. Ni jambo lipi jema kwetu kutenda? Je ni kuorodhesha dhambi zetu za kila siku mbele za Mungu na kuomba msamaha. Tukiamini kuwa, kwa kujua na kuamini Injili ya maji na Roho matatizo yetu yanaweza kutatuliwa.
Katika (Yohana 6:53-55) Yesu alisema “hakika nawaambia msipokula mwili wangu na damu yangu hamuwezi kuingia ufalme wa mbinguni. Yeyote aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu, anao uzima wa milele, naye atafufuliwa siku ya mwisho, kwa kuwa mwili wangu ni chakula hakika na damu yangu ni kinywaji” hakika hapa ni lazima tule mwili wa Yesu na kuinywa damu yake, maana yake, ni sharti tuwe na imani ya kuamini Yesu alichukua dhambi za dunia kwa ubatizo aliopokea kutoka kwa Yohana. Maana yake ni kama hatujui ukweli juu ya ubatizo wa Yesu, basi hatuwezi kumpa dhambi zetu, na dhambi zetu haziwezi kusamehewa. Kama kusingekuwa na ubatizo ambao Yesu alipokea kutoka kwa Yohana mbatizaji, mwakilishi wa wanadamu, dhambi zetu kamwe zisingesamehewa (Mathayo 3:15, 11:11-13).
Kusulubiwa kwa Yesu yalikuwa ni matokeo ya ukweli kuwa, kabla ya hili alikuwa amebeba dhambi za wanadamu kwa njia ya ubatizo wa Yohana. Mungu ametuokoa kutoka dhambini kwa kusulubiwa, kuimwaga damu yake ya thamani, na hapo kubeba makosa ya dhambi zetu.
Tunapokiri kumwamini Yesu ni lazima tuamini kuwa, alichukua dhambi zetu zote kwa ubatizo wake. Biblia inasema wazi juu ya ondoleo la dhambi, habari ambayo tunaweza kuifupisha katika pointi mbili kuu.
Kwanza, inatuambia kuwa kwa kubatizwa, Yesu alizikubali dhambi za dunia zilizopitia katika mwili wake. Zaburi 32:1 inasema, “Heri aliyesamehewa dhambi, Na kusitiriwa makosa yake” Neno ‘kusitiriwa’ lina maana kuchukua dhambi na kuzikubali dhambi na 1 Petro 3:21 inasema “mfano wa mambo hayo ni ubatizo unaowaokoa ninyi pia siku hizi (sio kuwekea mbali uchafu wa mwili bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu) kwa kufufuka kwake Yesu kristo” kwa ubatizo aliopokea kutoka kwa Yohana dhambi zote za wanadamu zimeondoshwa moja kwa moja.
 Pili, Biblia inatuambia kuwa Yesu ameondosha dhambi za dunia. Isaya 43:25 inasema, “Mimi, naam mimi ndiye niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako” kuyafuta makosa maana yake ni kuyapoteza kabisa kutoka katika maandishi.
Ina maana, Mungu baba amesafisha dhambi za dunia kwa kuzipitisha kwa mwanae kwa njia ya ubatizo. Kwa wale kati yetu wanaoweza kusema “sina tumaini kwa kuwa nimetenda dhambi nyingi sana” wao pia wanaweza kuwekwa huru mbali na dhambi kwa kulisikia Neno la Injili ya maji na Roho. Shetani anatuambia, “Je hujatenda dhambi nyingi?” Lakini hata kama tungesikia maneno hayo, tukiamini ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani hapo tunaweza kukombolewa kutoka dhambini. Tukiwa na imani kama hii, shetani hupata woga na kukimbia. Tumshawishi kuwa Bwana amesamehe dhambi kwa njia ya ubatizo na damu yake msalabani. Tukiamini kuwa Yesu amesamehe dhambi kwa njia ya ubatizo na damu yake msalabani ndipo amani ya ajabu huingia maishani mwetu. Hii ndio imani kuu ya ukristo, Imani ya ondoleo la dhambi.

Jumapili, 30 Machi 2014

MANABII WA UONGO


(Yuda 1:11) inasema, “Ole wao! Kwa sababu walikwenda katika njia ya kaini, na kulifuata kosa la Balaamu pasipo kujizuia, kwa ajili ya ujira, nao wameangamia katika maasi ya kora.” Ipi sasa ndio njia ya Kaini? Kaini alienda mbali na njia ya Mungu, na Mungu akamwadhibu. Wale waliotekwa na shetani wanafanya kazi ili kupata pesa. Kifungu kinaendelea kusema, “wameikimbilia tamaa katika kosa la Balaam kwa kutafuta faida” Wachungaji waliotekwa na shetani wanahubiri sana ili kupata pesa, wamefungwa na shetani, wanatenda kazi za manabii wa wa uwongo. Manabii hawa wa uwongo hufurahia kupata pesa nyingi zinazotolewa kama sadaka makanisani. Wanatumia nguvu kubwa kuhubiri pale wanapoona waumini wao wanamwaga pesa nyingi makanisani kama sadaka. Na pale waumini wanatoa pesa kidogo, manabii wa uwongo hata hawathubutu kuwabariki. Hivi ndivyo ilivyo kuwa waliomezwa na shetani wanatoa huduma makanisani ili hatimaye wapate pesa.
Ukitoa pesa nyingi, wanakupa hata madaraka makubwa kanisani kama mtumishi ama mzee wa kanisa. Lakini kama wewe sio mtoaji, hawawezi kamwe kukupa hata cheo kanisani. Hawa ambao kifungu hiki cha maneno kinawazungumzia ni wale wapenda pesa tu. Hawa walikuwa akina nani? Biblia inawataaja akina Balaam, Nabii wa Agano la Kale, aliyewaingiza watu wa Israeli katika biashara ya kuwauza ili kupata pesa. Watu kama Balaam wanafanya kazi kwa nguvu za shetani, hao ndio wanaofanya huduma kujichumia pesa. Fungu hilo la maneno hatimaye linatuambia kuwa watu wanaingia kuwa “mateka wa Kora” Watu hawa waliunda vyama vyao na kusimama kinyume na makanisa ya Mungu. Watu wanaopenda pesa wataishia kuwa watu wa kusimama kinyume na Mungu.
(Yuda 1:12) Inasema, “Watu hawa ni miamba yenye hatari katika karamu zenu za upendo walapo karamupamoja nanyi, wakijilisha pasipo hofu; ni mawinguyasiyo na maji, yachukuliwayona upepo; ni miti iliyopukutika, isiyo na matunda, iliyokufa mara mbili, na kung’olewa kabisa.” Wale wanaowatazama watu kwa mtazamo wa pesa, ni wataalamu wa kudanganya wengine na kuwaibia waumini wao pesa. Kwa kuwa watumishi wa shetani ni aina ya watumishi wenye njaa ya kujishibisha, wanajijali wao wenyewe, hawafikiri juu ya Roho za wengine. Hata kama watu wanamwamini Yesu, wengi wao wanatawaliwa na hawana amani ndani yao, wana hofu juu ya dhambi zao, na wanaendeshwa na ujinga wa hofu zao. Watumishi wa shetani wanapanda mbegu ya uongo kwa kudanganya wakifuata nguvu ya shetani. Na kila mara wakiongea habari za neno la Mungu, wanachanganya na uongo hata hawana aibu. Kwa hiyo Biblia inawaelezea wao kama “mawimbi yenye nguvu ya baharini, yanayobubujika aibu yao” (Yuda 1:13).
Wakati wa siku za mwisho ukifika, mapepo yataongeza nguvu ya kupotosha watu. Na hivyo hata watumishi watazidisha nguvu. Katika nyakati za mwisho, kabla ya Yesu hajarudi, shetani atafanya kazi kubwa hata ndani ya makanisa katika ulimwengu huu. Mapepo yatapamba moto, unabii utazidi sana. Jambo la muhimu sana hapa ni kwa wale ambao bado hawajazaliwa kwa upya hata kama wanamwamini Yesu, hata kama waiamini Injili ya Maji na Roho iliyotolewa na Bwana, na kupokea ondoleo la dhambi na karama za roho Mtakatifu. Na kwa kuwa na Roho Mtakatifu, ni sharti wawe na uzima wa milele. Lakini wale watumishi wa Mungu waliotekwa na shetani, hutafuta baraka za mwili tu, nguvu ya uponyaji, kuongea kwa ndimi, na kutenda miujiza kama misingi ya matakwa yao na malengo. Ndiyo sababu watu hawa huweka kipaumbele kwa yale shetani anayowaagiza. Katika dunia ya leo, mtu akianza kuongea kwa ndimi katika nyumba zao za ibada, watu wanaomzunguka mtu huyu humsifu na hata kumpigia makofi. Na wale wasioweza kuongea kwa ndimi huwekwa katika chumba kimoja na kufundishwa namna ya kunena kwa lugha ama kuongea kwa ndimi, wakirudia rudia “Lul-lu-lujah, Lul-lu-lujah,
Haleluya.” Wanapojaribu kurudiarudia maneno haya kwa haraka, inafikia hatua wanaongea maneno yasiyoeleweka, maneno ya ajabu ajabu, kama vile umeweka kanda mbovu kwenye redio (Katika kuongea haraka, maneno yanakwama katika ulimi). Inapofikia asilimia 80 ya watu wamepoteza namna ya kuongea vizuri, kwa ndimi zao kukwamisha maneno, ni nani kati yao ataweza kutamka maneno kwa ukamili? Ni kwa sababu wafuasi hao wamewekewa mikono na watu wenye pepo, nao pia hupandwa na roho hiyo. Pepo hufanya makao na kukaa mioyoni mwao. Ni kwa sababu wamejaa pepo, ndiyo maana wanaongea kwa kuongozwa na pepo. Msidanyike na kazi za mapepo, lakini iaminini kuwa Injili ya kweli ya Roho Mtakatifu mioyoni na kati ya wale wanaoamini Injili ya Maji na Roho iliyoandikwa katika Biblia. Hata sasa, kazi potofu za mapepo zinaendelea kati ya wale wanofuata imani za Kikarismatiki.
Lakini Mkitubu Siku Hiyo
(Mathayo 7:22-23) inasema, “Wengi wataniambia siku ile, Bwana Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza? Ndipo nitaawambia dhahiri, sikuwajua ninyi kamwe, ondokeni kwangu ninyi mtendao maovu.” Watu wengi wanaamini kwamba kujifanya nabii kwa jina la Bwana, kutoa pepo, kutenda miujiza, kwa jina la Bwana, ni kazi za Mungu na Roho Mtakatifu, Kuna wakristo katika dunia ya leo wanaodai kutoa pepo kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, Manabii wanapoonekana kutenda miujiza, wanasema kwa kujiamini, hiyo ni kazi ya Roho Mtakatifu. Lakini neno linasema, mambo hayo sio kazi ya Roho Mtakatifu. Neno linasema kuwa nguvu hiyo ya kuondoa mapepo, ishara, maajabu na miujiza mbalimbali ni kazi za shetani. Licha ya hayo, watu bado wanaamini kuwa hizo ni kazi za Roho Mtakatifu. Kazi za shetani zilikuja kwa ajili ya wale waliuoandaliwa maangamizi, na watu wale ambao wanafanya ishara na miujiza kamwe hawawezi kuokolewa. Kwa hiyo Biblia inatuonya kuwa “Wapendwa, msiziamini kila roho, bali zijaribuni kuona kama zinatoka kwa Mungu, kwa sababu, manabii wa uongo wamekwenda duniani.” (1 Yohana 4:1).