Jumamosi, 31 Mei 2014

INJILI YA MAJI NA ROHO

MAANA YA UBATIZO
Ubatizo maana yake kusafishwa, kuzikwa, (kuzamishwa) na maana ya kiroho kutwikwa dhambi kwa kuwekea mikono, kama ilivyofanywa katika Agano la kale, (Walawi 4:29, 16:21).
Wakati wana wa Israeli walipotoa sadaka ya upatanisho katika nyakati za Agano la Kale, isingekuwa njia sahihi kumchinja mnyama wa sadaka pasipo kwanza kuwekewa mikono juu ya kichwa chake kwa kutwikwa dhambi juu yake kwa niaba yao na ilikuwa ni kuonyesha jinsi ya ubatizo wa Yesu utakao kuja katika Agano Jipya. Hivyo inakuwa ni kosa na kuvunja sheria ya Mungu kuamini msalaba wa Yesu pekee bila kuamini pia ubatizo wake.
Katika Agano Jipya, ubatizo wa Yesu na Yohana Mbatizaji ulikuwa ni kusafisha dhambi za ulimwengu. “ubatizo wa Yesu” una maana ya kuchukua dhambi zote za wanadamu, kutakaswa kwa dhambi zote za ulimwengu.
Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizaji, mwakilishi wa wanadamu na kuhani mkuu katika uzao wa Haruni, na kubebeshwa dhambi zote za ulimwengu juu yake. Hili ni dhumuni kuu la ubatizo.
Maana ya kiroho neno “ubatizo” ni “kutwika, kuzikwa” Hivyo “ubatizo wa Yesu” maana yake dhambi zote alitwikwa Yesu na kuhukumiwa badala yetu. Ili kuokoa wanadamu, Yesu alizibeba dhambi zetu zote kwa ubatizo wake na kufa kwa dhambi hizo.
Yote haya, kifo chake na pia kifo chako na changu wenye dhambi wote ulimenguni na ufufuko wake ni ufufuo wa watu wote. Kujitoa kwake sadaka ni wokovu wa wenye dhambi na ubatizo ni ushuhuda Halisi katika kutusafisha dhambi zetu zote sisi walimwengu. Hivyo, Mtume Paulo alisema “Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi; (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamira safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo. (1Petro 3:21)
Sisi kama waumini wa Kristo yatupasa kujifunza maana halisi ya ubatizo, maana katika huo tunapata wokovu. Maji hayana la kufanya katika wokovu, bali ni ishara ya nje ya kile ulichokiamini ndani yako.
Rejea maandiko haya katika Biblia “Basi Myahudi mmoja, jina lake Apolo, mzalia wa Iskanderea. Mtu wa elimu akafika Efeso; alikuwa hodari katika maandiko. Mtu huyo alikuwa amefundishwa njia ya Bwana; Na kwa kuwa roho yake ilikuwa ikimwaka, alianza kunena na kufundisha kwa usahihi habari za Yesu; naye alijua ubatizo wa Yohana tu. Akaanza kunena kwa ujasiri katika sinagogi; hata Prisila na Akila walipomsikia wakamchukuwa kwao, wakamweleza njia ya bwana kwa usahihi zaidi. (Matendo 18:24-26)
Apolo aliyajua maandiko na alijua ubatizo wa Yohana tu, ambao haukuwezesha waumini kupokea Roho Mtakatifu, hata Prisila na Akila walipomsikia walimchukua na kumfundisha njia ya bwana kwa usahihi zaidi. Hata leo hii kuna watu wengi hawajui maana ya ubatizo kwa ujumla wake. Kwanini Apolo alifundishwa njia ya bwana kwa usahihi zaidi? Jibu la swali hili tutalipata katika aina nyingine ya ubatizo wa Yesu.
Watu wengi ulimwenguni hawafahamu ni kwanini Yesu alikuja katika ulimwengu na kubatizwa na Yohana Mbatizaji. Hivyo hebu tuzungumzie sababu za ubatizo wa Yesu na juu ya Yohana Mbatizaji aliyembatiza Yesu.
Kwanza, yatupasa kuwaza juu ya nini kilichomfanya Yohana Mbatizaji abatize watu katika mto Yordani. Inaelezwa katika( Mathayo 3:1-12) kwamba Yohana Mbatizaji alibatiza watu ili kuwalejesha kwa Mungu toka katika dhambi kwa kutubu kwao.
Kimsingi umuhimu wa ubatizo uliofanywa na Yohana Mbatizaji ulikuwa kwaajili ya toba ambayo iliwarudisha Waisrael kwa Yesu ambaye angekuja baadaye. Toba maana yake kugeuka toka maisha ya dhambi na kumwani Masiya ili kusamehewa dhambi zote.
Jambo la kwanza Yesu alilolifanya katika huduma yake ya wazi ilikuwa ni kubatizwa na Yohana Mbatizaji. Dhambi zote za ulimwengu zilitwikwa juu yake kwa njia hii.
Hivyo ubatizo wa Yesu ulikuwa ndiyo mwanzo wa wokovu wa Mungu kwa wanadamu pamoja pia na tendo la haki kwa Yesu kuweza kutakasa dhambi zote za ulimwengu juu yake kwa njia ya ubatizo.
Yesu alikuja ulimwenguni na kubatizwa na Yohana Mbatizaji, injili ya ufalme wa Mbinguni ndipo ilipoanza. Mbingu zilifunuka kwa ubatizo wake kama ilivyoelezwa katika Mathayo 3:15 ilikuwa sawa sawa kabisa na sadaka ya upatanisho iliyoelezwa katika (Walawi 1:1-5, 4:27-31) nyakati za Agano la kale.
Moja ya mafundisho potofu katika nyakati hizi za imani ya kikiristo ni kwamba, utaweza kuokolewa unapomkiri Yesu kuwa mwokozi kwa kuwa bwana ni pendo. Biblia inasema “Yeyote aliitaye jina la Bwana ataokolewa” (Matendo 2:21, Warumi10:13) ambapo pia inasema “Si kila mtu aniitaye Bwana Bwana ataingia ufalme wa mbinguni, bali wale wote watendao mapenzi ya Baba yangu wa Mbinguni”(Mathayo 7:21).
Kwanini tujifunze ubatizo kwa undani, hebu soma kifungu hichi” Ikawa, Apolo alipokuwa Korintho, Paulo, akiisha kupita kati ya nchi za juu, akafika Efeso; akakutana na wanafunzi kadha wa kadha huko, akawauliza je? Mlimpokea Roho Mtakatifu Mlipoamini? Wakamjibu, La hata kusikia kwamba kuna roho Mtakatifu hatukusikia. Akawauliza mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, kwa ubatizo wa Yohana. Paulo akisema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu.” (Matendo 19:1-4)
“Je ulipokea Roho Mtakatifu pale ulipoamini?” hata waKristo swali hili hawalifahamu. Mtume Paulo aliwauliza waamini wa Yesu kama walipokea Roho Mtakatifu pale walipoamini kwa mara ya kwanza na akafafanua jinsi waamini wanavyoweza kumpokea Roho Mtakatifu. Katika fungu hili la maneno kwa kupata ushuhuda wa nguvu ya ubatizo wa Yesu, Paulo aliamsha imani zao tena. Apollo alipokuwa Korintho, baada ya Paulo kupita Asia ndogo, na kufika Efeso, na kuwakuta wanafunzi wa Yesu, aliwaambia, “Je mlipokea Roho Mtakatifu mara mlipoamini?” Usharika wa korintho haukuelwa lolote juu ya ukweli huu, kuwa wanapokea Roho Mtakatifu wakimwamini Yesu.
*      Wangelijua na kuamini ubatizo ambao Yesu alipokea
Kusikia kuwa walikuwa wamebatizwa kupitia ubatizo wa Yohana pekee, Paulo alifafanua juu ya mahusiano ya ubatizo wa Yesu na ule wa Roho Mtakaifu. Ndipo wakaelewa maana ya ubatizo wa Yesu walioupokea. Kuna tofauti kubwa sana kati ya kumwamini yeye huku tukijua maana ya ubatizo ambao Yesu alipokea kutoka kwa Yohana, na kumwamini yeye bila kujua maana ya mahusiano ya ubatizo wa Yesu na ule wa Roho Mtakaifu. Ndipo wakaelewa maana ya ubatizo wa Yesu walioupokea.
Sasa je, ni ubatizo gani Yohana aliutoa kwa watu? Yohana aliwaambia watu kutubu, kuikimbia dhambi na kumrudia Mungu. Ubatizo ambao Yohana aliutoa ulikuwa ni ubatizo wa kutubu ambao uliwafanya watu watubu. Lakini ubatizo ambao Yesu alipokea kutoka kwa Yohana katika Mathayo 3:13-17 ulipokewa ili kuitimiza haki ya Mungu, na ndio maana tunasema ulikuwa tofauti na wa Yohana.
Ubatizo ambao Yesu aliupokea kutoka kwa Yohana ulikuwa wa kuondoa dhambi za wanadamu.
Imani yao ilikuwa tofauti kabisa na imani ya Paulo, kwani ubatizo walioupokea haukuwa wa kujua picha halisi ya ukweli huu.
Sasa ubatizo huu ni kuikamilisha haki ya Mungu unamaanisha nini? Una maana kwamba kwa
kubatizwa, Yesu alichukua dhambi za wanadamu kuanzia dhambi ya Adamu mpaka Mwanadamu yule wa mwisho.

Mathayo 3:15-16 Inasema “Yesu akajibu akasema, na iwe hivyo, kwa kuwa imetupasa kuitimiza haki yote, ndipo akamruhusu.”Haki ya Mungu inaweza kupatikana katika ubatizo ambao Yesu alipokea ndani ya imani inayoikubali damu ya msalabani kwa hiyo wale ambao mioyo yao imesamehewa dhambi kwa kuamini ubatizo huo na damu yake msalabani ni lazima wapokee ubatizo wa maji kwa imani. Kwa nini? Kwa sababu kwa imani ya ubatizo wake, dhambi zote zimeondoshwa kikamilifu, ndio maana Paulo alieleza ubatizo wa Yesu kwa wale ambao hawakupokea Roho Mtakatifu.
Watu wengi wamekuwa wakijaribu kumpokea Roho Mtakatifu kwa njia wanazozifahamu wao kama kurudia rudia maneno na nyinginezo, lakini hizo si njia sahihi katika wokovu.
Yatupasa kuwa na uelewa sahihi katika neno la ubatizo, ukisoma (Matendo 18:24-26, na Matendo 19: 1-4) utaona ya kwamba Apolo alipita Efeso akahubiri ubatizo, na uelewa wake ulikuwa katika ubatizo wa Yohana tu. Na Paulo alipita eneo hilo hilo la Efeso baada ya Apolo kuondoka na kuwafundisha ubatizo kwa usahihi zaidi ambapo walipokea Roho Mtakatifu. Hivyo katika ubatizo tunapokea Roho Mtakatifu.
Damu ya Yesu msalabani ni matokeo ya ubatizo na si kumwaga damu msalabani ndiko kuliko mwezesha Yesu kubeba dhambi zetu. Alibeba dhambi zetu pale alipo batizwa na ndipo alipokwenda msalabani akiwa tayari amekwisha beba dhambi hizo zote za ulimwengu hatimaye kufa ili kuleta upatanisho wa dhambi za ulimwengu.
Hivyo msalaba ni matokeo ya ubatizo aliopokea Yesu, kwa kuwa Yesu alikwisha beba dhambi zetu kwa njia ya ubatizo wake, kumwaga damu msalabani ndiko hitimisho la kuelekea upatanisho wa dhambi zetu zote.

Unapomtwika Yesu dhambi zako katika ubatizo unakuwa umesamehewa makosa yako yote, ndipo Roho Mtakatifu anapata nafasi ya kukaa ndani yako. Tunaweza kuzaliwa upya kiroho kwa kuamini ubatizo na damu ya Yesu.

Jumatatu, 5 Mei 2014

TOBA YA KWELI KATIKA KUMPOKEA ROHO MTAKATIFU


(Matendo 2:38) “Petro akawaambia tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo mpate ondoleo la dhambi zenu nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.”
Biblia inasema katika (Matendo 2) kwamba mahubiri ya Petro yaliwagusa kwa undani watu na hata kuwasababisha watubu dhambi zao. Walichomwa mioyo yao na kumwambia Petro na mitume wengine, “Tutendeje ndugu zetu? Petro akawaambia tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kisto mpate ondoleo la dhambi zenu nayinyi mtapokea kipawa cha Roho Mtaakatifu” (Matendo 2:38). Mahubiri ya Petro yanatuonyesha wazi kuwa imani katika injili nzuri ya maji na ya Roho ni ya muhimu sana katika kumpokea Roho Mtakatifu na pia inatuonyesha jinsi toba la kweli lilivyo. Tunapaswa kutambua kuwa tunaweza kumpokea Roho Mtakatifu sambamba na ondoleo la dhambi kwa kuyaangalia maandiko matakatifu kwa karibu na kwa kuamini katika injili nzuri ya maji na ya Roho.
Jambo la kwanza tunalotakiwa kuwa nalo ili kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu ni imani katika toba la kibiblia. Hata hivyo, tunatakiwa kuwa makini ili tusije tukalielewa toba hili kuwa ni majuto. Toba maana yake ni imani katika Yesu Kristo. Tunaweza kuona katika Biblia kuwa watu walijuta kwa kumsulubisha Bwana. Walijuta kumuuliza Petro kwamba wafanye nini na walizikiri dhambi zao hata kabla ya Petro kuwaambia watubu. Tunaweza kuona kuwa toba ambalo Petro alilizungumzia halikuwa kuzijutia dhambi wala kuzikiri, bali ilikuwa ni kumpokea Yesu Kristo katika moyo wa kila mtu kama Mwokozi na kuwa na imani katika injili nzuri ambayo Yesu ametupatia. Na hii ndiyo asili nzuri ya toba.
Upendo wa Yesu Kristo ulikuja kwetu kabla hayajakuwepo majuto-binafsi kwa dhambi za mioyo yetu. Hii inamaanisha kuwa Yesu alizichukua dhambi zetu pale alipobatizwa katika Mto Yordani, alikufa Msalabani, na kisha akafufuka toka kwa wafu. Kwa njia hii, alizisafisha hatia na dhambi zetu zote.
Toba la kweli maana yake ni kuamini katika ukweli huu. Je, unafikiri kuwa dhambi zetu zimesafishwa moja kwa moja kwa kule kujuta na kuomba msamaha? Ukweli ni kuwa hili sio toba la kweli. Toba la kweli maana yake ni kupokea ondoleo la dhambi zetu kwa kuamini katika injili nzuri ya ubatizo wa Yesu na damu yake. Biblia inasema kuwa tunasamehewa dhambi zetu kwa toba. Vivyo hivyo, inatupasa kuiamini injili ya ubatizo wa Yesu na damu yake ili tuweze kupokea ondoleo kamili la dhambi zetu.
Petro alitoa huduma ya ubatizo “katika jina la Yesu Kristo” kwa wale waliomwamini Yesu. Yesu alibatizwa ili aweze kuzichukua dhambi za wanadamu wote. Ubatizo na kifo chake juu ya Msalaba ulikuwa ni ukamilifu wa injili nzuri inayowawezesha waamini kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu (Mathayo 3:15-17). Mwanadamu anaweza kutakaswa kwa kuamini katika ubatizo wa Yesu na damu yake pale Msalabani. Kwa kifupi, wale waliopokea ondoleo la dhambi kwa kuamini katika injili wamempokea Roho Mtakatifu.
Je, sala zitaweza kuleta uwepo wa Roho Mtakatifu ndani?
Watu hawatoweza kupokea msamaha wa dhambi na uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yao hata ikiwa watafanya maombi ya dhati kutaka uwajilie. Ili tuweze kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu, ni muhimu kuamini injili njema iliyokamilishwa kwa ubatizo wa Yesu na damu yake pale msalabani. Roho Mtakatifu wa Mungu hutunukiwa kwa wale walio kuwa na dhambi amabao wametakaswa moja kwa moja.
Imani katika injili ni kumkubali Yesu kama mwokozi wa kweli. Matendo 2:38 inasema, “tubuni mbatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo mpate ondoleo la dhambi zenu nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.”Mtume Petro alisema kwamba uwepo wa Roho Mtakatifu hutolewa kwa wale walio samehewa dhambi zao kwa njia ya imani katika toba ya kweli. Msamaha wa dhambi na kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu ni pacha.
Biblia inasema“Tubuni mkabatizwe kilammoja kwa jina lake Yesu Kristo mpate ondoleo la dhambi zenu nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu kwa kuwa ahadi hii ni kwaajili yenu na kwa watoto wenu kwa watu wote walio mbali na kwa wote watakao itwa na Bwana Mungu wetu wa mbinguni” (Matendo 2:38-39).
Mtu aweza kupokea Roho Mtakatifu kwa sharti kwamba moyo wake umetakaswa, usio na dhambi. Hivyo imetupasa kuamini injili ambayo Yesu Kristo ametupatia. Lazima tutakaswe baada ya kupokea msamaha wa dhambi kwa kuamini injili njema inayosema dhambi zetu zote ulimwenguni zilitakaswa pale Yesu Kristo alipobatizwa. Ndipo hapo tutakapoweza kupokea Roho Mtakatifu. Ni mapenzi ya Mungu kwa Roho Mtakatifu kuweka makazi ndani ya wanadamu “maana hayo ndiyo mapenzi ya Mungu kutakaswa kwenu” (1 Wathesalonike 4:3).
Msamaha wa kweli hutolewa si kwa njia na juhudi za watu kujitoa muhanga au kuwa wema, bali kwa kuamini injili ambayo Mungu Utatu Mtakatifu aliyoitimiza kupitia Yohana mbatizaji. Mungu Utatu Mkatifu huwatunukia uwepo wa Roho Mtakatifu kwa wale wote waliokwisha samehewa dhambi zao kwa kuamini injili njema. Umati wa watu ulichomwa mioyo pale ulipo yasikia Petro aliyoyanena siku ile ya pentekoste. Walipaza sauti na kuuliza “Tutendeje ndugu zetu?”  (Matendo 2:37). Hii hudhihirisha kwamba tayari wamekwisha badilishwa kifikra zao na sasa wanamwamini Yesu Kristo kuwa ni mwokozi na Bwana wao. Na pia wamekwisha okolewa kutokana na dhambi zao kwa kuamini toba ya kweli aliyo ihubiri Petro. Msamaha wa dhambi ulikwisha tolewa kwa wanadamu wote kwa kutegemea imani zao katika injili njema ya ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani.
Dhumuni la ubatizo wa Yesu ni kumwezesha yeye abebe dhambi za ulimwengu. Kwa kuamini hili ndilo sharti moja wapo muhimu la kupokea Roho Mtakatifu. Mungu ametupatia uwepo wa Roho Mtakatifu kwa wale wanao iamini injili ya kweli iliyo na msingi wa ubatizo wa Yesu Kristo. “Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini na tazama mbinguni zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama huwa akija juu yake” (Mathayo 3:16). Kuja kwa Roho Mtakatifu katika siku ile ya pentekoste kuna uhusiano wa pekee na imani ya mitume katika injili njema: ubatizo wa Yesu, damu yake msalabani na ufufuko.
Katika Matendo inasema kwamba watu waliobatizwa katika jina la Yesu walimpokea Roho Mtakatifu moja kwa moja katika muda huo huo. Yatupasa kuamini kwamba kupokea Roho Mtakatifu ni karama ya pekee toka kwa Mungu. Ili tuweze kupokea karama hii, inatupasa kwamba dhambi zetu zote zisafishwe kwa kupitia imani katika ubatizo wa Yesu na kifo chake msalabani.
Kulingana na Matendo, wale wote walio sikia mahubili ya Petro ambapo alishuhudia akisema, “Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi”  (Matenda 2:40).  Walitii maonyo yake na kubatizwa. Kile tunachojifunza tokakatika biblia ni kwamba, mitume katika siku hizo za kanisa la mwanzo walimpokea Roho Mtakatifu kwa msingi wa imani zao katika ubatizo wa Yesu Kristo na damu yake msalabani. Hili ndilo sharti muhimu la kuweza kumpokea Roho Mtakatifu. Imani katika ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani ni jambo lisilo wekwa kando ikiwa mtu atahitaji msamaha wa dhambi.
Imani ituongozayo katika kumpokea Roho Mtakatifu kwa njia ya toba ya kweli.
Hebu tuangalie katika Mtendo 3:19,“tubuni basi mrejee, ili dhambi zenu zifutwe zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana.” Tutawezaje basi kuelezea nini maana ya toba? Hebu na tufikirie upya tena.
Katika biblia, toba maana yake ni kuirudia imani ya ukombozi. Katika nyakati hizo watu walishika tabia kama walivyo penda nafsini mwao na kuviabudu vitu vilivyo umbwa na Mungu. Lakini baada ya kugundua kwamba Yesu Kristo alikwisha kuwaokoa toka dhambini kwa maji na kwa damu yake, ndipo wakaanza kubadilika. Hii ndiyo toba ya kibiblia. Toba ya kweli ni kuirudia injili njema ya maji na Roho.
Ni ipi toba iliyo ya kweli inayo hitajika katika kumpokea Roho Mtakatifu? Ni katika kuamini ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani “zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana.”Ikiwa watu watakuwa na imani hii, basi watasamehewa dhambi zao na kumpokea Roho Mtakatifu. Kwa kuwa Yesu amewatakasa wenye dhambi wote duniani kwa njia ya ubatizo wake na damu yake msalabani, imetupasa basi kuamini hili ili tuweze kupokea ukombozi na uwepo wa Roho Mtakatifu.
Ili tuweze kumwamini Yesu na kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu, inahitajika dhambi zote zitwikwe juu ya Yesu kwa imani ya ubatizo wake na kifo chake msalabani. Yatupasa kuamini kwamba Yesu alizichukua dhambi zetu zote na kufa msalabani ili ahukumiwe kwa ajili ya dhambi hizo. Hii ndiyo imani sahihi na toba ya kweli, amabayo inayotuwezesha kuwa na uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yetu.
Roho Mtakatifu huja juu ya wale wote walio kwisha samehewa dhambi zao zote. Kwanini Mungu ametoa Roho Mtakatifu kama karama kwa wale wote walio kwisha pokea ukombozi? Kwasababu Roho Mtakatifu, akiwa mtakatifu, anahitaji kuweka makazi ndani yao na kuwachapa mhuri kuwa wana wa Mungu.
Roho Mtakatifu ni Mungu. Baba, Mwana na Roho Mtakatifu ni Mungu mmoja. Ni nafsi tatu lakini ni Mungu mmoja kwa wale wote wenye kuamwamini Yesu. Baba alikuwa na mpango wa kutuokoa sisi tokana na dhambi zetu, na hivyo Mwana Yesu alikuja ulimwenguni akabatizwa na Yohana ili kuzichukua dhambi za ulimwengu, alikufa msalabani, alifufuka toka kuzimu siku ya tatu na kupalizwa mbinguni. Roho Mtakatifu hutuongoza katika kuiamini injili njema kwa kushuhudia juu ya ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani.
Mungu huwaweka mihuri wale wote walio kwisha kuokolewa kwa kupitia Roho Mtakatifu. Mungu huwatunukia Roho Mtakatifu wale wote wanao amini injili inayo sema kuwa, Yesu alizichukua dhambi za ulimwengu. Mungu huwapa Roho Mtakatifu kama ahadi na kama mhuri kuashiria kuwa ni watoto wake. Roho Mtakatifu ni uthibitisho wa mwisho katika wokovu wa dhambi kwa wale wenye kuamini injili njema.
Wale wote walio na Roho Mtakatifu ni watoto wa Bwana. Wale walio na uwepo wa Roho Mtakatifu wakati wote hupata nguvu upya kila wakati. Huwa na imani madhubuti katika maneno ya Mungu juu ya ubatizo waYesu na damu yake pale msalabani. Ni wenye furaha ya kweli. Wale wote wenye kutubu
kwa njia iliyo sahihi hawatakuwa na dhambi tena mioyoni mwao na hivyo watakuwa na uwepo wa Roho Mtakatifu.

Biblia inasema kwamba, ipo toba iletayo msamaha wa dhambi. Je, umekwisha fanya toba ya aina hiyo? Ukitubu na kuifuata imani ya kweli, nawe pia utaweza kupokea injili njema. Nakusihi utubu dhambi zako na umpokee Roho Mtakatifu. Je, uko tayari kutubu na kuamini injili njema ambayo itakuongoza katika kumpokea Roho Mtakatifu?