Jumatatu, 10 Machi 2014

JENGA MADHABAHU KATIKA MOYO WAKO


Tunaweza kuona katika (kutoka 25:8-9) Nao wanifanyie patakatifu; ili nipate kukaa kati yao. Sawasawa na haya yote nikuonyeshayo, mfano wa maskani, na mfano wa vyombo vyake vyote, ndivyo mtakavyo vifanya.” (waebrania 3:6) “bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba ya Mungu; ambaye nyumba yake ni sisi, kama tukishikamana sana na ujasiri wetu na fahari ya taraja letu mpaka mwisho.”  kwamba Mungu alimwita Musa na akammwambia kupajenga mahali pa kuabudia ambapo Mungu ataishi. Mahali ambapo Mungu anaishi au kushinda hapo panaitwa madhabahu. Katika malango na katika mapaa ya madhabahu hii kulikuwa na fumbo lililokuwa limefichika, yaani fumbo la Yesu Kristo. Katika kifungu hiki ambacho Mungu aliwaamuru watu wa Israeli kuijenga madhabahu hii, basi ninaamini kuwa Mungu anatueleza sisi kuijenga madhabahu hii katika mioyo yetu ili kwamba aweze kuishi ndani yetu.
Nini ambacho tunapaswa kukifanya ikiwa tunahitaji Mungu akae ndani yetu? Kwanza kabisa, kwa kweli ni lazima tufahamu jinsi ambavyo Mungu alivyozisafisha dhambi zetu zote kwa kupitia Neno la Injili ya maji na Roho. Na ni lazima tuamini katika ukweli huo. Ili kufanya hivyo, kwanza ni lazima tuziangalie nafsi zetu kimsingi. Tangu kuzaliwa kwetu hatukuwa na chaguo jingine lolote bali kuzaliwa kama wenye dhambi. Inawezekanaje basi kwa Roho wa Mungu mtakatifu kukaa katika mioyo ya watu kama sisi? Ili Roho wa Mungu aweze kukaa katika mioyo ya wenye dhambi ni lazima  basi hawa wenye dhambi wawe na imani inayoamini katika Injili ya kweli. Kwa maneno mengine, Roho mtakatifu anakaa ndani yetu pale tu tunapokuwa tumezioshelea mbali dhambi zetu kwa kufahamu na kuamini katika Injili ya maji na Roho. Kule kusema kuwa Roho mtakatifu anaweza kukaa katika mioyo kumwezesha kwa kuamini katika ukweli wa milele wa maji na Roho.
Madhabahu ambapo Mungu anapenda kukaa
Hata hivyo, watu wengi ambao bado hawajapokea ondoleo la dhambi hawafahamu ukweli huu.  Unafikiri ni kwa nini Mungu alimwamuru Musa kulijenga Hema takatifu la kukutania? Alimwamuru Musa kwa sababu alitaka kukaa katika mioyo yetu. Tatizo ni kuwa watu wengi kutokana na kutojua kwao juu ya ukweli huu (Injili ya maji na Roho), wanatuimia kiasi kikubwa cha fedha kujenga majengo ya makanisa makubwa na ya kushangaza na wanadanganyika kuamini kuwa haya ndiyo mahekalu ambapo Mungu anaishi.
Watu wa jinsi hiyo wapo tayari kutoa fedha yote walioweza kuipata katika kipindi chote cha maisha yao kwa Mungu, kwa sababu wanafikiria kimakosa kuwa makanisa yao yanaweza kufanyika  ni mahekalu ya Mungu mtakatifu ikiwa kama watayajenga majengo ya kifahari na makubwa. Lakini je, ni kweli kuwa Mungu atapendezwa ikiwa tutajenga makanisa makubwa ya kupendeza na kisha tukampatia Mungu?. Je, ni kweli kuwa Mungu atakubaliki ikiwa utafanya jambo kama hili?  Je, kanisa hili litafanyika kuwa madhabahu ambayo inakaliwa na Mungu? Hivyo si kweli kabisa. Haya ni matokeo ya imani isiyofahamu ukweli wa Injili ya maji na Roho na walioangukia katika uongo mkuu.
Madhabahu ambayo Mungu anataka kuishi si jengo kubwa la kanisa bali ni moyo wako ambao umeoshwa dhambi zako. Mungu anapenda kukaa ndani ya mioyo ya wenye haki ambao wamepokea ondoleo la dhambi na waliofanyika watakatifu. Ili kulifanya hili liwezekane tunatakiwa kutoa sala zetu za toba ili tuweze kutakaswa? Hapana, kwa kweli siyo hivyo. Hata hivyo, kuna watu wengi wakristo wa siku hizi wanafikiri na kuamini namna hii.
Ili kulijenga Hema takatifu la kukutania kwa kupitia Musa, Mungu aliwaamuru wana wa Israeli kumtolea sadaka. Kama ilivyoandikwa katika (kutoka 25:3-7). Baada ya kuzipokea sadaka hizi kupitia Musa alijenga madhabahu ya Mungu kwa vifaa hivi kwa kupitia wafanyakazi ambao waliipokea hekima toka kwa Mungu. Kama ambavyo Mungu alimwamuru Musa kulijenga Hema takatifu la kukutania katika Agano la kale, basi katika Agano jipya, Mungu anatutaka sisi pia kujenga madhabahu katika mioyo yetu ili aweze kuishi ndani yetu. Vifaa vya imani ambavyo kwa hivyo tunaweza kuvitumia katika kuijenga madhabahu hii ni Neno la Injili ya maji na Roho. Kwa vifaa vya Injili hii ya maji na Roho ni lazima tuzioshelee mbali dhambi zetu zote na kusafishwa. Kwa kutueleza sisi kujenga madhabahu yake Mungu anatueleza sisi kuweka wazi moyo wako na kisha kuamini katika Injili ya maji na Roho.
Jambo hili sasa linazusha swali jingine juu ya aina ya imani ambayo tunapaswa kuwa nayo ili Mungu aweze kuishi katika mioyo ya wenye dhambi. Jibu ni rahisi na la wazi. Kwa kuwa Mungu mtakatifu aweze kuishi katika mioyo ya wenye dhambi, ni lazima kwanza wenye dhambi hawa wafahamu kile ambacho Injili ya maji na roho inawaeleza, na kisha ni lazima waamini katika ukweli huo. Ndipo mioyo yao inapoweza kusafishwa na kupokea ondoleo la dhambi, na ndipo hapo tu Mungu Mtakatifu anapoweza hatimaye kuishi katika mioyo ya watu wa jinsi hiyo ambao wamepokea ondoleo la dhambi wanapokuwa wameuachilia mbali ugumu wao na wakamini katika  Injili ya maji na roho, ambayo ni majaliwa ya Mungu, basi Mungu anaweza kuja na kukaa katika mioyo yao.
Hii ndiyo sababu 1wakorintho 3: 16-17 inasema, “Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.” Mungu ni mtakatifu na asiye na dhmbi. Kwa hiyo, anaeza tu kuja katika mioyo yetu wakati inapokuwa imesafishwa vizuri kwa Neno la Injili ya maji na Roho. Biblia inasema kwa wazi kuwa ni wale tu waliopokea ondoleo la dhambi ndiyo wanaweza kupokea karama ya Roho Mtakatifu (Matendo ya mitume 2:38)
"Injili ya maji na Roho" inapatikana katika blog hii



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni