(Yuda 1:11) inasema, “Ole wao! Kwa sababu walikwenda katika njia ya kaini, na
kulifuata kosa la Balaamu pasipo kujizuia, kwa ajili ya ujira, nao wameangamia
katika maasi ya kora.” Ipi sasa ndio njia ya Kaini? Kaini alienda mbali
na njia ya Mungu, na Mungu akamwadhibu. Wale waliotekwa na shetani wanafanya
kazi ili kupata pesa. Kifungu kinaendelea kusema, “wameikimbilia tamaa katika kosa la Balaam kwa kutafuta faida” Wachungaji
waliotekwa na shetani wanahubiri sana ili kupata pesa, wamefungwa na shetani,
wanatenda kazi za manabii wa wa uwongo. Manabii hawa wa uwongo hufurahia kupata
pesa nyingi zinazotolewa kama sadaka makanisani. Wanatumia nguvu kubwa kuhubiri
pale wanapoona waumini wao wanamwaga pesa nyingi makanisani kama sadaka. Na
pale waumini wanatoa pesa kidogo, manabii wa uwongo hata hawathubutu
kuwabariki. Hivi ndivyo ilivyo kuwa waliomezwa na shetani wanatoa huduma makanisani
ili hatimaye wapate pesa.
Ukitoa pesa nyingi, wanakupa hata madaraka makubwa kanisani
kama mtumishi ama mzee wa kanisa. Lakini kama wewe sio mtoaji, hawawezi kamwe
kukupa hata cheo kanisani. Hawa ambao kifungu hiki cha maneno kinawazungumzia
ni wale wapenda pesa tu. Hawa walikuwa akina nani? Biblia inawataaja akina
Balaam, Nabii wa Agano la Kale, aliyewaingiza watu wa Israeli katika biashara
ya kuwauza ili kupata pesa. Watu kama Balaam wanafanya kazi kwa nguvu za
shetani, hao ndio wanaofanya huduma kujichumia pesa. Fungu hilo la maneno
hatimaye linatuambia kuwa watu wanaingia kuwa “mateka wa Kora” Watu hawa waliunda vyama vyao na kusimama kinyume
na makanisa ya Mungu. Watu wanaopenda pesa wataishia kuwa watu wa kusimama
kinyume na Mungu.
(Yuda 1:12) Inasema, “Watu hawa ni miamba yenye hatari katika karamu zenu za
upendo walapo karamupamoja nanyi, wakijilisha pasipo hofu; ni mawinguyasiyo na
maji, yachukuliwayona upepo; ni miti iliyopukutika, isiyo na matunda, iliyokufa
mara mbili, na kung’olewa kabisa.” Wale wanaowatazama watu kwa mtazamo
wa pesa, ni wataalamu wa kudanganya wengine na kuwaibia waumini wao pesa. Kwa
kuwa watumishi wa shetani ni aina ya watumishi wenye njaa ya kujishibisha,
wanajijali wao wenyewe, hawafikiri juu ya Roho za wengine. Hata kama watu
wanamwamini Yesu, wengi wao wanatawaliwa na hawana amani ndani yao, wana hofu
juu ya dhambi zao, na wanaendeshwa na ujinga wa hofu zao. Watumishi wa shetani
wanapanda mbegu ya uongo kwa kudanganya wakifuata nguvu ya shetani. Na kila
mara wakiongea habari za neno la Mungu, wanachanganya na uongo hata hawana
aibu. Kwa hiyo Biblia inawaelezea wao kama “mawimbi
yenye nguvu ya baharini, yanayobubujika aibu yao”
(Yuda 1:13).
Wakati wa siku za mwisho ukifika, mapepo yataongeza nguvu ya
kupotosha watu. Na hivyo hata watumishi watazidisha nguvu. Katika nyakati za
mwisho, kabla ya Yesu hajarudi, shetani atafanya kazi kubwa hata ndani ya
makanisa katika ulimwengu huu. Mapepo yatapamba moto, unabii utazidi sana.
Jambo la muhimu sana hapa ni kwa wale ambao bado hawajazaliwa kwa upya hata
kama wanamwamini Yesu, hata kama waiamini Injili ya Maji na Roho iliyotolewa na
Bwana, na kupokea ondoleo la dhambi na karama za roho Mtakatifu. Na kwa kuwa na
Roho Mtakatifu, ni sharti wawe na uzima wa milele. Lakini wale watumishi wa
Mungu waliotekwa na shetani, hutafuta baraka za mwili tu, nguvu ya uponyaji,
kuongea kwa ndimi, na kutenda miujiza kama misingi ya matakwa yao na malengo.
Ndiyo sababu watu hawa huweka kipaumbele kwa yale shetani anayowaagiza. Katika
dunia ya leo, mtu akianza kuongea kwa ndimi katika nyumba zao za ibada, watu
wanaomzunguka mtu huyu humsifu na hata kumpigia makofi. Na wale wasioweza
kuongea kwa ndimi huwekwa katika chumba kimoja na kufundishwa namna ya kunena
kwa lugha ama kuongea kwa ndimi, wakirudia rudia “Lul-lu-lujah, Lul-lu-lujah,
Haleluya.”
Wanapojaribu kurudiarudia maneno haya kwa haraka, inafikia hatua wanaongea
maneno yasiyoeleweka, maneno ya ajabu ajabu, kama vile umeweka kanda mbovu
kwenye redio (Katika kuongea haraka, maneno yanakwama katika ulimi). Inapofikia
asilimia 80 ya watu wamepoteza namna ya kuongea vizuri, kwa ndimi zao
kukwamisha maneno, ni nani kati yao ataweza kutamka maneno kwa ukamili? Ni kwa
sababu wafuasi hao wamewekewa mikono na watu wenye pepo, nao pia hupandwa na
roho hiyo. Pepo hufanya makao na kukaa mioyoni mwao. Ni kwa sababu wamejaa
pepo, ndiyo maana wanaongea kwa kuongozwa na pepo. Msidanyike na kazi za
mapepo, lakini iaminini kuwa Injili ya kweli ya Roho Mtakatifu mioyoni na kati
ya wale wanaoamini Injili ya Maji na Roho iliyoandikwa katika Biblia. Hata
sasa, kazi potofu za mapepo zinaendelea kati ya wale wanofuata imani za
Kikarismatiki.
Lakini Mkitubu Siku
Hiyo
(Mathayo 7:22-23)
inasema, “Wengi wataniambia siku ile, Bwana Bwana,
hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako
kufanya miujiza? Ndipo nitaawambia dhahiri, sikuwajua ninyi kamwe, ondokeni
kwangu ninyi mtendao maovu.” Watu wengi wanaamini kwamba kujifanya nabii
kwa jina la Bwana, kutoa pepo, kutenda miujiza, kwa jina la Bwana, ni kazi za
Mungu na Roho Mtakatifu, Kuna wakristo katika dunia ya leo wanaodai kutoa pepo
kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, Manabii wanapoonekana kutenda miujiza, wanasema
kwa kujiamini, hiyo ni kazi ya Roho Mtakatifu. Lakini neno linasema, mambo hayo
sio kazi ya Roho Mtakatifu. Neno linasema kuwa nguvu hiyo ya kuondoa mapepo,
ishara, maajabu na miujiza mbalimbali ni kazi za shetani. Licha ya hayo, watu
bado wanaamini kuwa hizo ni kazi za Roho Mtakatifu. Kazi za shetani zilikuja
kwa ajili ya wale waliuoandaliwa maangamizi, na watu wale ambao wanafanya
ishara na miujiza kamwe hawawezi kuokolewa. Kwa hiyo Biblia inatuonya kuwa “Wapendwa, msiziamini kila roho, bali zijaribuni kuona
kama zinatoka kwa Mungu, kwa sababu, manabii wa uongo wamekwenda duniani.”
(1 Yohana 4:1).