sheria sehemu ya sita
Katika Warumi 3:20 tunasoma “ Kwa maana kutambua dhambi huja
kwa njia ya sheria”. Mwanzo kabisa nilichukulia kifungu hiki kuwa ujumbe
binafsi kwa Mtume Paulo na kuamini maneno niliyopendelea. Lakini baada ya
machozi yangu kukauka hakika sikuweza kuendelea na maisha yangu ya imani ya
kidini. Hivyo niliendelea na dhambi na kufikia hatua ya kugundua nina dhambi
ndani ya moyo wangu na kushindwa kuishi kwa sheria. Sikuweza kuvumilia ingawa
sikuweza kuachana na sheria kwa kuwa niliamini ilikuwepo ili niweze kuitii.
Hatima yake nikawa mwanasheria kama walionyeshwa katika maandiko hapo awali.
Ikawa ni vigumu kwangu kuendelea na maisha ya imani.
Nilikua na dhambi nyingi hata kufikia kila ninapo soma
sheria naanza kugundua dhambi hizo kila ninapozivunja amri 10 ndani ya moyo wangu.
Ikumbukwe kuwa na dhambi moyoni ni sawa kutenda dhambi tu! Sikuweza kufahamu kwamba
nilikuwa tayari muumini wa sheria.
Nilipofuata sheria nilifarijika. Lakini nilipoanguka nilikua
mnyonge, mwenye hasira na huzuni. Na wakati huo nikawa mwenye kukosa matumini kwa
yote. Ingeweza kuwa rahisi ikiwa hapo awali ningefundishwa ukweli juu ya sheria
kama vile “Hapana, siyo hivi! Ipo maana nyingine ya sheria nayo ni kama taa
kuonyesha dhambi zako kama vile wewe unapenda fedha, kupenda jinsia tofauti na
vitu vizuri vya kuonekana.Una vitu unavyovipenda kuliko umpendavyo Mungu.
Unapenda sana kufuata mambo ya dunia. Sheria
iliwekwa kwako si uifuate bali uweze kugundua nafsi yako kama mwenye dhambi
aliye na uovu moyoni”.
Ikiwa mtu yoyote angeweza kunifundisha hivi basi nisingeweza
kuteseka kwa muda mrefu namna ile. Hivi ndivyo nilivyo weza kuishi kwa sheria kwa
miaka mingi kabla ya kuja kugundua hili. Amri ya nne inasema “Ikumbuke siku ya
Sabato na uitakase”. Hii ina maana kwamba tusifanye kazi siku ya
jumamosi.Tunafundishwa tusifanye kazi, sio kutembea mwendo wa mbali katika
safari kwa siku ya Jumamosi.Nilidhani ilikuwa ni sahihi na niheshima kutembea sehemu
nilizo hitaji kuhubiri. Hata hivyo nilitaka kuhubiri sheria. Na nilihisi
ilinipasa kutenda yale nihubiriyo. Ikawa ni vigumu na kushindwa. Kama ilivyo
hapo mwanzo”wasoma je?” sikuelewa swali hili na kuteseka miaka mingi. mwanasheria
hakuelewa vema hili.Alifikiri ya kwamba ikiwa ataheshimu sheria na kuishi kwa
uangalifu mkubwa atakuwa amebarikiwa na Mungu.
Lakini Yesu alimwambia “wasomaje?”. Naye akajibu kwa imani
itokanayo na sheria. Naye akamjibu “umejibu vema, unaichukua kama
ilivyoandikwa. Jaribu kuifuata. Utaishi ikiwa utaweza na utakufa
ukishindwa.Mshahara wa dhambi ni mauti.Hakika ukishindwa utakufa” ( kinyume cha
kuishi ni kufa,sivyo?). lakini mwanasheria huyu hakugundua hili. Mwanasheria ni
mfano wetu sisi leo, mimi na wewe. Nilijifunza theologia (elimu ya dini) kwa
miaka mingi. Nilijaribu kila namna, kusoma kila kitu na kutenda kila jambo;
kufunga kula, kuwa na maono, kunena kwa lugha……. Nilisoma Biblia kwa miaka mingi kwa kutegemea nitahitimisha jambo fulani mbeleni. Lakini kiroho nilikuwa bado
kipofu!
Na ndiyo maana mwenye dhambi huitaji mtu fulani atakayefungua
macho yake, na huyu ni Bwana wetu Yesu Kristo. Ndipo mtu hugundua “Ahaa! Hatuna
uwezo wa kufuata sheria. Haijalishi ni kwa bidii gani tutaweza kujaribu
kuifuata tutaishia kufa tukikosa matumaini. Lakini Yesu alikuja kutuokoa kwa
maji na kwa Roho! Haleluya!” Kwa maji na kwa Roho tutaweza kukombolewa. Ni
neema, zawadi ya Mungu. Na tumsifu Bwana. Nilikuwa mwenye bahati ya pekee
kuhitimu toka kwenye njia ya kukosa matumaini katika sheria, naamini wengi
huchukua muda mrefu zaidi katika maisha yao kusoma theologia katika njia panda
na bila kugundua ukweli hadi umauti. Wengine huamini kwa mioyo mingi, kizazi
hadi kizazi na hawazaliwi upya.
Tunahitimu kutokuwa wadhambi pale tu tunapogundua hatuna
uwezo wa aina yeyote binafsi wa kufuata sheria na kusimama mbele ya Yesu kwa
kukubali kuisikiliza Injili ya maji na Roho. Tunapokutana na Yesu tunahitimu
kutoka kwenye hukumu na jehanamu. Sisi ni wenye wingi wa dhambi, lakini
tunafanyizwa haki kwa sababu Yesu ametuokoa katika maji na damu yake. Yesu
amesema hatuwezi kuishi katika mapenzi yake. Alimwambia mwanasheria, lakini
hakuelewa hili. Hivyo alimpa mfano huu.
“Mtu mmoja alishuka
toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang`anyi; wakamvua nguo,
wakamtia jeraha wakaenda zao,wakamwacha karibu kufa” (Luka 10:30) Yesu alimpa
Mwanasheria mfano huu ili kuamsha dhamira yake kwakua huteseka kwa maisha yake
yote kama jinsi Mtu yule aliyepigwa na wanyang`anyi karibu kufa.
Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko. Yeriko
inawakilisha dunia hii ya sasa, hali Yerusalemu inawakilisha mji wa kidini, mji
wa imani uliojawa na majigambo ya sheria. Mfano huu hutuelezea ikiwa tutamwani
Kristo kwa njia ya udini tutaangamia.
“ Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko akangukia
kati ya wanyang`anyi, wakamvua nguo wakamtia jeraha wakenda zao wakimwacha
karibu kufa”. Yerusalemu ulikuwa ni mji mkubwa ukiwa na wakazi wengi. Kulikuwa
na Kuhani Mkuu, Jeshi la Makuhani Walawi na wengi wa Wakuu mashuhuri wa dini.
Palikuwepo na wengi wenye kuelewa sheria vema. Na walijaribu kuishi kwa sheria,
lakini walishindwa na kukimbilia Yeriko wakangukia duniani ( Yeriko ) na
kushindwa kuzuia kukutana na wanyang`anyi
Mtu huyu pia alikutana njiani na wanyang`anyi toka
Yerusalemu kwenda Yeriko wakamvua nguo. “Kuvuliwa nguo” maana yake kupoteza
haki. Ni vigumu kwetu kuishi kwa kufuata sheria, kuishi kwa sheria Mtume Paulo
amesema katika Warumi 7:19-20 “Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi, bali
lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo. Basi kama lile nisilolipenda ndilo
nilipendalo si mimi nafsi yangu nilitendalo, bali ni ile dhamiri ikaayo ndani
yangu”.
Ningetamani kutenda mema na kuishi katika Neno lake Mungu.
Lakini ndani ya moyo wa mwanadamu umefurika mawazo mabaya, uasherati,wivi,
uuaji, unzizi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi,
upumbavu ( Marko 7: 21-23 ).Kwa kuwa haya ndiyo yaliyomo ndani ya mioyo yetu,
basi tunafanya yale tusiyopaswa na hatufanyi yale yatupasayo kufanya.
Tunaendelea kurudia maovu haya ndani ya mioyo yetu. Hivyo shetani huitaji kukuhamasisha
kwa kiasi kidogo tu ili uweze kutenda dhambi.
Alikutana na nani njiani alipokuwa akienda Yeriko? Alikutana
na wanyang’anyi. Yeyote yule asiyetambua na kuishi kwa sheria, maisha yake
yanafananishwa na mbwa aliyetelekezwa. Hula na kunywa na kwenda haja mahala
popote. Mbwa wa aina hii huamka asubuhi nyingine na kwenda haja na kula tena.
Huweza hata kula kinyesi chake.
Ndiyo maana mtu huyu hufananishwa na mbwa. Hula na kunywa na
kwenda haja lakini huomba toba asubuhi inayofuata na kurudia yale yale kwa mara
zote. Ni sawa na mtu aliyekutana na wanyang’anyi akienda Yeriko. Akaachwa akiwa
amejeruhiwa karibu ya kifo. Ina maana kwamba kuna dhambi ndani ya moyo. Na hii
ndivyo ilivyo kwa mwanadamu.
Watu humwamini Yesu na kujaribu kuishi kwa sheria katika
Yerusalemu, jamii ya dini, lakini wanaachwa na dhambi ndani ya mioyo yao. Kile
wanachoweza kuonyesha katika maisha yao ya udini ni majeraha ya dhambi. Wale
wenye dhambi mioyoni mwao hakika siku za mwisho watakwenda motoni. Wanajua
hili, lakini hawajui lakufanya. Je ni kweli hata wewe upo katika mji huo wa
dini? Ndiyo. Hata sisi tulikuwepo.
Mwanasheria aliyeshindwa kuielewa sheria ya Mungu
angehangaika maishani pote, lakini angeishia motoni kwa majeraha. Ni sisi kati
yetu, mimi na wewe. Yesu pekee aokoa. Wapo watu wengi wenye uerevu kati yetu na
kila mara kupayuka wanayoyajua. Wote hawa hujifanya kwa kuishi katika sheria ya
Mungu na hawapo kweli nafsini mwao. Hawawezi kuita beleshi kuwa ni beleshi,
mara zote huzificha nafsi zao kwa nje ili kuonekana waaminifu.
Kati yao ni wenye dhambi kuelekea Yeriko, wale waliopigwa na
waovu na kuachwa karibu kufa. Tunapaswa kuelewa vile tusivyo imara, wepesi wa
kuumizwa mbele za Mungu. Yatupasa tukiri mbele zake “Bwana, hakika nitaishia motoni
ikiwa hutoniokoa. Naomba uniokoe. Nitakufuata popote, ikiwa ni penye kimbunga
au dhoruba, ikiwa tu nitaweza kusikia Injili. Ukiniacha peke yangu, nitakwenda
motoni. Nakusihi niokoe!”
Wale wenye kugundua kuwa wapo karibu na jehanamu na kujaribu
kutenda matendo ya kujitafutia haki wakiwa wanaambatana na Bwana ndiyo pekee
watakaookolewa. Hatuwezi kuokolewa kwa juhudi zetu binafsi. Yatupasa kuelewa
kwamba, tutafananishwa na mtu yule aliye angukia katika mikono ya wanyang’anyi.
kumbuka
mwenye haki hatendi dhambi makusudi kwa sababu ana Roho wa mungu soma katika blog hii "injili ya maji na roho."