Somo la tatu
Maana
ya kiroho ya
Mti wa mshita,
mafuta, na viungo
(Kutoka 25:1-9) “BWANA
akanena na Musa, akamwambia: waambie wana wa Israeli kwamba wanitwalie sadaka;
kila mtu ambaye moyo wake wampa kupenda mtatwaa kwake sadaka yangu. Sadaka
utakayopokea mikononi mwao ni hii: dhahabu, na fedha, na shaba; na nyuzi za
rangi ya bluu (samawiti), na za rangi ya zambarau, na za rangi nyekundu, na
kitani safi, na singa za mbuzi; na ngozi za kondoo waume zilizotiwa rangi nyekundu,
na ngozi za pompoo, na miti ya mshita; na mafuta ya ile taa, na viungo vya
manukato kwa yale mafuta ya kupaka, na kwa ule uvumba wenye harufu nzuri; na
vito vya shohamu, na vito vingine vya kutiwa kwa ile naivera, na kwa kile
kifuko cha kifuani. Nao wanifanyie
patakatifu; ili nipate kukaa kati yao. Sawasawa na haya yote nikuonyeshayo,
mfano wa maskani, na mfano wa vyombo
vyake vyote, ndivyo mtakavyo vifanya.”
Nguzo za hema
takatifu la kukutania, madhahabu ya sadaka ya kuteketezwa, na mbao na vifaa
vingine vya madhabahu vyote vilitengenezwa
kwa mbao za mti wa mshita. Kwa kawada mti katika Biblia unamaanisha
wanadamu (waamuzi 9:8-15, marko 8:24). Pia mti hapa unamaanisha kwetu juu ya
asili ya mwanadamu; ile hali ya kuwa mti huu wa mshita ulitumika katika nguzo,
katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, na katika hema takatifu la kukutania
lenyewe inatueleza kuwa kama ambavyo mizizi ya mti wa mshita mara zote
imefunikwa ardhini, basi asili yetu ni ile ambayo haiwezi kujisaidi bali
kutenda dhambi wakati wote. Ni lazima watu wote wakiri kuwa hawawezi kujisaidia
bali wataendelea kuwa wasio na haki na kutenda dhambi kila mara.
Kwa wakati huo
huo, mti wa mshita una maanisha juu ya ubinadamu wa Yesu Kristo. Masihi aliyekuja
katika mwili wa binadamu alibeba dhambi zote za ulimwengu, na alihukumiwa kwa
haki kwa ajili ya wanadamu. Yeye ni mungu mwenyewe, na kwa hiyo, sanduku la
ushuhuda, meza ya wa wonyesho, madhabahu ya uvumba, na mbao za Hema takatifu la
kukutania vyote vilitengenezwa kwa mti wa mshita na vikafunikizwa kwa dhahabu
safi.
Mafuta kwa ajili
ya mwanga na manukato kwa ajili ya mafuta ya kujipaka na kuwekea wakfu na kwa
uvumba wa manukato vinamaanisha juu ya imani yetu ambayo tunaitoa kwa Yesu Kristo.
Yesu Kristo ni masihi aliyetuokoa mimi na wewe. Maana ya jina “Yesu” ni “yeye
atakaye waokoa watu wake toka katika dhambi zao,” na jina “Kristo” lina maana
ya “mtiwa mafuta,” hivyo majina haya yanatueleza sisi kuwa Yesu Kristo ni Mungu
mwenyewe na kuhahani mkuu wa Mbinguni aliyetuokoa sisi. Ili kuheshimu mapenzi
ya Mungu, Bwana wetu alikuja hapa duniani katika mwili wa mwanadamu,
alibatizwa, alisulubiwa, msalabani kwa
ajili yetu, na kwa hiyo ametupatia zawadi ya wokovu. Kwa hakika jukumu la
kuhani mkuu lililochukuliwa na Yesu aliye tupatia wokovu wetu lilikuwa ndiyo
kazi nzuri sana.
Vito vya Shohamu, na Vito
vingine vya kuwekwa katika Naivera na katika kile Kifuko cha kifuani cha kuhani
mkuu.
Vito kumi na mbili vya aina tofauti
vimetajwa hapa ambavyo vitawekwa katika naivera na katika kifuko cha kifuani
cha kuhani mkuu. Kuhani mkuu alivaa kwanza gwanda kama kanzu fupi, kisha
akavaa joho la bluu, na kisha akavaa naivera juu ya joho. Kisha, kifuko cha
kifuani kiliwekwa katika naivera ambayo ilivaliwa wakati wa sherehe maalum ya
sadaka ya kuteketezwa, na katika kifuko hiki cha kifuani viliwekwa vito kumi na
mbili vya dhamani. Hii inatuonyesha sisi kuwa jukumu la kuhani mkuu lilikuwa ni
kuwakumbatia na kuwa jumuisha wa Israeli pamoja na watu wengine wa ulimwengu
mzima katika kifua chake, kwenda mbele za Mungu, na kumtolea mungu sadaka zao
za kuteketezwa.
Yesu, ambaye ni kuhani mkuu wa
milele wa Mbinguni pia aliyakumbatia mataifa yote ya ulimwengu katika kifua
chake, akautoa mwili wake mwenyewe ili kuzichukuwa dhambi zetu kwa ubatizo wake
na akasulubiwa kwa ajili yetu, na kwa hiyo amewaweka wakfu watu wake kwa Mungu Baba.
Vito vya thamani kumi na mbili vilivyowekwa katika kifuko cha kifuani vina maana ya mataifa yote ya ulimwengu huu,
na kuhani mkuu aliye vaa vito hivyo ni alama ya Yesu Kristo ambaye amewaokoa
mataifa na kuyakumbatia mataifa yote ya ulimwengu katika kifua chake.
Hivyo, hizi zilikuwa ni sadaka
ambazo Mungu wetu aliwaambia Waisraeli kumtolea ili kulijenga hema takatifu la
kukutania kwa jili yake. Kuna maana ya kiroho katika ukweli kuwa Mungu
aliwaambia Waisraeli kumjengea hema takatifu la kukutania, mahali ambapo Mungu
angeishi, kwa sadaka zao. Mara nyingi watu wa Israeli walibakia ni wenye dhambi
kwa sababu hawakuweza kuitunza na kuifuata sheria ambayo Mungu aliwapatia. Hii
ndiyo sababu Mungu aliwaeleza kupitia Musa kulijenga hema takatifu la kukutania
na kuwapatia utaratibu wa sadaka ya kuteketezwa, ambayo kwa hiyo
ondoleo la dhambi lilitolewa kwa sadaka ya kuteketezwa iliyotolewa katika Hema
takatifu la kukutania. Kwa maneno mengine, Mungu alizifuta dhambi zote za Waisraeli
kwa kuzipokea sadaka zao, kwa kutumia sadaka kuijenga nyumba yake, na kwa kuwafanya
kumtolea sadaka zao za kuteketezwa katika Hema takatifu la kukutania kwa mujibu
wa kanuni za utaratibu wa sadaka ya kuteketezwa. Hivyo ndivyo ambavyo Mungu
angeliweza kuishi katika Hema takatifu la kukutania pamoja na watu wa Israeli.
kumbuka tunapoongelea kulijenga hema takatifu, tunamaanisha vihi sasa wewe ni nyumba (hema) ya Mungu, vifaa vyote vilivyo agizwa na Mungu ni lazima hata sasa vitumike kukujenga kiroho kwa imani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni