(Matendo 2:38) “Petro
akawaambia tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo mpate ondoleo
la dhambi zenu nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.”
Biblia inasema katika (Matendo 2) kwamba
mahubiri ya Petro yaliwagusa kwa undani watu na hata kuwasababisha watubu
dhambi zao. Walichomwa mioyo yao na kumwambia Petro na mitume wengine, “Tutendeje
ndugu zetu? Petro akawaambia tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kisto
mpate ondoleo la dhambi zenu nayinyi mtapokea kipawa cha Roho Mtaakatifu” (Matendo 2:38). Mahubiri ya Petro yanatuonyesha wazi
kuwa imani katika injili nzuri ya maji na ya Roho ni ya muhimu sana katika kumpokea
Roho Mtakatifu na pia inatuonyesha jinsi toba la kweli lilivyo. Tunapaswa kutambua
kuwa tunaweza kumpokea Roho Mtakatifu sambamba na ondoleo la dhambi kwa kuyaangalia
maandiko matakatifu kwa karibu na kwa kuamini katika injili nzuri ya maji na ya
Roho.
Jambo la kwanza tunalotakiwa kuwa nalo ili kupokea uwepo wa
Roho Mtakatifu ni imani katika toba la kibiblia. Hata hivyo, tunatakiwa kuwa
makini ili tusije tukalielewa toba hili kuwa ni majuto. Toba maana yake ni
imani katika Yesu Kristo. Tunaweza kuona katika Biblia kuwa watu walijuta kwa kumsulubisha
Bwana. Walijuta kumuuliza Petro kwamba wafanye nini na walizikiri dhambi zao
hata kabla ya Petro kuwaambia watubu. Tunaweza kuona kuwa toba ambalo Petro alilizungumzia
halikuwa kuzijutia dhambi wala kuzikiri, bali ilikuwa ni kumpokea Yesu Kristo
katika moyo wa kila mtu kama Mwokozi na kuwa na imani katika injili nzuri
ambayo Yesu ametupatia. Na hii ndiyo asili nzuri ya toba.
Upendo wa Yesu Kristo ulikuja kwetu kabla hayajakuwepo majuto-binafsi
kwa dhambi za mioyo yetu. Hii inamaanisha kuwa Yesu alizichukua dhambi zetu
pale alipobatizwa katika Mto Yordani, alikufa Msalabani, na kisha akafufuka
toka kwa wafu. Kwa njia hii, alizisafisha hatia na dhambi zetu zote.
Toba la kweli maana yake ni kuamini katika ukweli huu. Je, unafikiri
kuwa dhambi zetu zimesafishwa moja kwa moja kwa kule kujuta na kuomba msamaha?
Ukweli ni kuwa hili sio toba la kweli. Toba la kweli maana yake ni kupokea
ondoleo la dhambi zetu kwa kuamini katika injili nzuri ya ubatizo wa Yesu na
damu yake. Biblia inasema kuwa tunasamehewa dhambi zetu kwa toba. Vivyo hivyo,
inatupasa kuiamini injili ya ubatizo wa Yesu na damu yake ili tuweze kupokea
ondoleo kamili la dhambi zetu.
Petro alitoa huduma ya ubatizo “katika jina la Yesu Kristo” kwa
wale waliomwamini Yesu. Yesu alibatizwa ili aweze kuzichukua dhambi za wanadamu
wote. Ubatizo na kifo chake juu ya Msalaba ulikuwa ni ukamilifu wa injili nzuri
inayowawezesha waamini kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu (Mathayo
3:15-17). Mwanadamu anaweza kutakaswa kwa kuamini katika ubatizo wa Yesu
na damu yake pale Msalabani. Kwa kifupi, wale waliopokea ondoleo la dhambi kwa
kuamini katika injili wamempokea Roho Mtakatifu.
Je,
sala zitaweza kuleta uwepo wa Roho Mtakatifu ndani?
Watu hawatoweza kupokea msamaha wa dhambi na uwepo wa Roho
Mtakatifu ndani yao hata ikiwa watafanya maombi ya dhati kutaka uwajilie. Ili
tuweze kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu, ni muhimu kuamini injili njema
iliyokamilishwa kwa ubatizo wa Yesu na damu yake pale msalabani. Roho Mtakatifu
wa Mungu hutunukiwa kwa wale walio kuwa na dhambi amabao wametakaswa moja kwa
moja.
Imani katika injili ni kumkubali Yesu kama mwokozi wa kweli.
Matendo 2:38 inasema, “tubuni mbatizwe kila
mmoja kwa jina lake Yesu Kristo mpate ondoleo la dhambi zenu nanyi mtapokea
kipawa cha Roho Mtakatifu.”Mtume Petro alisema kwamba uwepo wa Roho Mtakatifu
hutolewa kwa wale walio samehewa dhambi zao kwa njia ya imani katika toba ya
kweli. Msamaha wa dhambi na kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu ni pacha.
Biblia inasema“Tubuni mkabatizwe kilammoja kwa jina lake Yesu
Kristo mpate ondoleo la dhambi zenu nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu
kwa kuwa ahadi hii ni kwaajili yenu na kwa watoto wenu kwa watu wote walio
mbali na kwa wote watakao itwa na Bwana Mungu wetu wa mbinguni” (Matendo 2:38-39).
Mtu aweza kupokea Roho Mtakatifu kwa sharti kwamba moyo wake
umetakaswa, usio na dhambi. Hivyo imetupasa kuamini injili ambayo Yesu Kristo
ametupatia. Lazima tutakaswe baada ya kupokea msamaha wa dhambi kwa kuamini injili
njema inayosema dhambi zetu zote ulimwenguni zilitakaswa pale Yesu Kristo
alipobatizwa. Ndipo hapo tutakapoweza kupokea Roho Mtakatifu. Ni mapenzi ya
Mungu kwa Roho Mtakatifu kuweka makazi ndani ya wanadamu “maana hayo
ndiyo mapenzi ya Mungu kutakaswa kwenu” (1 Wathesalonike
4:3).
Msamaha wa kweli hutolewa si kwa njia na juhudi za watu kujitoa
muhanga au kuwa wema, bali kwa kuamini injili ambayo Mungu Utatu Mtakatifu
aliyoitimiza kupitia Yohana mbatizaji. Mungu Utatu Mkatifu huwatunukia uwepo wa
Roho Mtakatifu kwa wale wote waliokwisha samehewa dhambi zao kwa kuamini injili
njema. Umati wa watu ulichomwa mioyo pale ulipo yasikia Petro aliyoyanena siku
ile ya pentekoste. Walipaza sauti na kuuliza “Tutendeje ndugu zetu?” (Matendo 2:37). Hii
hudhihirisha kwamba tayari wamekwisha badilishwa kifikra zao na sasa wanamwamini
Yesu Kristo kuwa ni mwokozi na Bwana wao. Na pia wamekwisha okolewa kutokana na
dhambi zao kwa kuamini toba ya kweli aliyo ihubiri Petro. Msamaha wa dhambi ulikwisha
tolewa kwa wanadamu wote kwa kutegemea imani zao katika injili njema ya ubatizo
wa Yesu na damu yake msalabani.
Dhumuni la ubatizo wa Yesu ni kumwezesha yeye abebe dhambi
za ulimwengu. Kwa kuamini hili ndilo sharti moja wapo muhimu la kupokea Roho
Mtakatifu. Mungu ametupatia uwepo wa Roho Mtakatifu kwa wale wanao iamini
injili ya kweli iliyo na msingi wa ubatizo wa Yesu Kristo. “Naye Yesu alipokwisha
kubatizwa mara akapanda kutoka majini na tazama mbinguni zikamfunukia, akamwona
Roho wa Mungu akishuka kama huwa akija juu yake” (Mathayo
3:16). Kuja kwa Roho Mtakatifu katika siku ile ya pentekoste kuna
uhusiano wa pekee na imani ya mitume katika injili njema: ubatizo wa Yesu, damu
yake msalabani na ufufuko.
Katika Matendo inasema kwamba watu waliobatizwa katika jina
la Yesu walimpokea Roho Mtakatifu moja kwa moja katika muda huo huo. Yatupasa
kuamini kwamba kupokea Roho Mtakatifu ni karama ya pekee toka kwa Mungu. Ili
tuweze kupokea karama hii, inatupasa kwamba dhambi zetu zote zisafishwe kwa
kupitia imani katika ubatizo wa Yesu na kifo chake msalabani.
Kulingana na Matendo, wale wote walio sikia mahubili ya Petro
ambapo alishuhudia akisema, “Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi” (Matenda 2:40). Walitii maonyo yake na kubatizwa. Kile
tunachojifunza tokakatika biblia ni kwamba, mitume katika siku hizo za kanisa
la mwanzo walimpokea Roho Mtakatifu kwa msingi wa imani zao katika ubatizo wa
Yesu Kristo na damu yake msalabani. Hili ndilo sharti muhimu la kuweza kumpokea
Roho Mtakatifu. Imani katika ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani ni jambo
lisilo wekwa kando ikiwa mtu atahitaji msamaha wa dhambi.
Imani ituongozayo
katika kumpokea Roho Mtakatifu kwa njia ya toba ya kweli.
Hebu tuangalie katika Mtendo 3:19,“tubuni
basi mrejee, ili dhambi zenu zifutwe zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako
kwake Bwana.” Tutawezaje basi kuelezea nini maana ya toba? Hebu na
tufikirie upya tena.
Katika biblia, toba maana yake ni kuirudia imani ya ukombozi.
Katika nyakati hizo watu walishika tabia kama walivyo penda nafsini mwao na
kuviabudu vitu vilivyo umbwa na Mungu. Lakini baada ya kugundua kwamba Yesu
Kristo alikwisha kuwaokoa toka dhambini kwa maji na kwa damu yake, ndipo
wakaanza kubadilika. Hii ndiyo toba ya kibiblia. Toba ya kweli ni kuirudia
injili njema ya maji na Roho.
Ni ipi toba iliyo ya kweli inayo hitajika katika kumpokea Roho
Mtakatifu? Ni katika kuamini ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani “zipate kuja
nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana.”Ikiwa watu watakuwa na
imani hii, basi watasamehewa dhambi zao na kumpokea Roho Mtakatifu. Kwa kuwa
Yesu amewatakasa wenye dhambi wote duniani kwa njia ya ubatizo wake na damu yake
msalabani, imetupasa basi kuamini hili ili tuweze kupokea ukombozi na uwepo wa
Roho Mtakatifu.
Ili tuweze kumwamini Yesu na kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu,
inahitajika dhambi zote zitwikwe juu ya Yesu kwa imani ya ubatizo wake na kifo
chake msalabani. Yatupasa kuamini kwamba Yesu alizichukua dhambi zetu zote na
kufa msalabani ili ahukumiwe kwa ajili ya dhambi hizo. Hii ndiyo imani sahihi
na toba ya kweli, amabayo inayotuwezesha kuwa na uwepo wa Roho Mtakatifu ndani
yetu.
Roho Mtakatifu huja juu ya wale wote walio kwisha samehewa
dhambi zao zote. Kwanini Mungu ametoa Roho Mtakatifu kama karama kwa wale wote
walio kwisha pokea ukombozi? Kwasababu Roho Mtakatifu, akiwa mtakatifu, anahitaji
kuweka makazi ndani yao na kuwachapa mhuri kuwa wana wa Mungu.
Roho Mtakatifu ni Mungu. Baba, Mwana na Roho Mtakatifu ni
Mungu mmoja. Ni nafsi tatu lakini ni Mungu mmoja kwa wale wote wenye kuamwamini
Yesu. Baba alikuwa na mpango wa kutuokoa sisi tokana na dhambi zetu, na hivyo Mwana
Yesu alikuja ulimwenguni akabatizwa na Yohana ili kuzichukua dhambi za
ulimwengu, alikufa msalabani, alifufuka toka kuzimu siku ya tatu na kupalizwa
mbinguni. Roho Mtakatifu hutuongoza katika kuiamini injili njema kwa kushuhudia
juu ya ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani.
Mungu huwaweka mihuri wale wote walio kwisha kuokolewa kwa
kupitia Roho Mtakatifu. Mungu huwatunukia Roho Mtakatifu wale wote wanao amini
injili inayo sema kuwa, Yesu alizichukua dhambi za ulimwengu. Mungu huwapa Roho
Mtakatifu kama ahadi na kama mhuri kuashiria kuwa ni watoto wake. Roho
Mtakatifu ni uthibitisho wa mwisho katika wokovu wa dhambi kwa wale wenye
kuamini injili njema.
Wale wote walio na Roho Mtakatifu ni watoto wa Bwana. Wale
walio na uwepo wa Roho Mtakatifu wakati wote hupata nguvu upya kila wakati. Huwa
na imani madhubuti katika maneno ya Mungu juu ya ubatizo waYesu na damu yake
pale msalabani. Ni wenye furaha ya kweli. Wale wote wenye kutubu
kwa njia iliyo sahihi hawatakuwa na dhambi tena mioyoni mwao
na hivyo watakuwa na uwepo wa Roho Mtakatifu.
Biblia inasema kwamba, ipo toba iletayo msamaha wa dhambi.
Je, umekwisha fanya toba ya aina hiyo? Ukitubu na kuifuata imani ya kweli, nawe
pia utaweza kupokea injili njema. Nakusihi utubu dhambi zako na umpokee Roho
Mtakatifu. Je, uko tayari kutubu na kuamini injili njema ambayo itakuongoza katika
kumpokea Roho Mtakatifu?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni