(Mtendo 19:1–3)
“Ikiwa Apolo alipokuwa Korintho, Paulo, akiisha kupita kati ya nchi za
juu alifika Efeso, akakutana na Wanafunzi kadhaa wa kadha huko akawauliza Je,
mlimpokea Roho Mtakatifu mlipo amini? Wakajibu la, hata kusikia kwamba kuna
Roho Mtakatifu hatukusikia. Akawauliza basi mlibatizwa kwa ubatizo gani?
Wakasema kwa ubatizo wa Yohana.”
Aina
gani ya Injili Paulo alihubiri? Alihubiri Injili ya ubatizo wa Yesu na damu
yake. Matendo 19:1-2 inasema “Ikiwa, Apolo alipokuwa Korintho, Paulo akiisha
kupita kati ya nchi za juu akafika Efeso, akakutana na Wanafunzi kadhaa wa kadha
huko akawauliza, Je, mlimpokea Roho Mtakatifu mlipoamini?”
Hata
hivyo watu hawa walikuwa wamekwisha mwamini Yesu huku wakiwa wameweka kando
maana ya ubatizo wa Yesu. Hawakujua juu ya Injili njema ambayo hupelekea
kumpokea Roho Mtakatifu ndani. Na hii kupelekea Paulo kuuliza “Je, mlimpokea Roho Mtakatifu
mlipoamini?” lilikuwa swali geni kwa baadhi ya
wafuasi. Watu wengine wangeliweza kuuliza “Je, una mwamini Yesu?” Lakini Paulo
aliuliza swali katika njia isiyokuwa ya kawaida ili kwamba waweze kumpokea Roho
Mtakatifu, ndani yao kwa kufanya upya imani zao katika Injili njema. Huduma ya
Paulo ilikuwa ni kuhubiri Injili njema ya ubatizo wa Yesu kwa Yohana Mbatizaji.
Hebu
tuone ushuhuda wa Mitume katika Injili ya ubatizo. Kwanza Paulo alishuhudia “Hasha sisi tulioifia
dhambi tutaishije tena katika
dhambi? Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo
Yesu tulibatizwa katika mauti yake?” (Warumi 6:2-3). “Maana ninyi nyote
mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo” (Wagalatia 3:27).
Mtume
Petro naye pia alishuhudia Injili ya ubatizo wa Yesu katika 1 Petro 3:21–22
akisema “Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unawaokoa
ninyi pia siku hizi (siyo kuweka mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamira
safi mbele za Mungu) kwa kufufuka kwake Yesu Kristo. Naye yupo mkono wa kuume
wa Mungu amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zikiisha kutiishwa
chini yake.”
Mtume
Yohana pia alishuhudia hii Injili njema katika 1
Yohana 5:5-9 “Mwenye kuushinda
ulimwenguni ni nani isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni mwana wa Mungu?
Huyu ndiye aliye kuja kwa maji na damu. Naye Roho ndiye ashuhudiaye kwa sababu
Roho ndiye kweli. Kwa maana wako watatu washuhudiao mbinguni Baba na Neno na
Roho Mtakatifu na watatu hawa ni umoja. Kisha wako watatu washuhudiao duniani,
Roho na maji na damu na watatu hawa hupatana kwa habari moja”.
Yohana
Mbatizaji alichukua nafasi muhimu, katika kukamilisha Injili njema. Biblia
inazungumzia yafuatayo juu ya Yohana Mbatizaji katika Malaki
3:1-3 na Mathayo 11:10-11.
Yohana
Mbatizaji alikuwa mwakilishi wa wanadamu na alikuwa ni nabii Eliya ajaye kama
alivyoandikwa katika Agano la Kale. Katika Agano la Kale, sadaka ya dhambi ilichinjwa
ili kumwaga damu baada ya kubeba dhambi za mtu kwa tendo la kuwekewa mikono.
Katika Agano Jipya, hata hivyo Yesu ndiye aliyesimama kama sadaka ya dhambi kwa
kubeba dhambi ya ulimwengu kwa njia ya ubatizo na kifo chake Msalabani kulipa mshahara
wa dhambi. Ubatizo wa Yesu kwa Yohana Mbatizaji pale Yordani ndiyo uliokoa
wanadamu wote.
Mungu
alipanga aina mbili za matukio ili kuweza kuwaokoa wanadamu tokana na dhambi
zao na kuweza kutimiza haki yote. Tukio la kwanza lilikuwa ni kumfanya Yesu aje
ulimwenguni kupitia mwili wa mwanamwali Bikira Mariam, na kuwezesha abatizwe na
kusulubiwa ili kuondoa dhambi za ulimwengu. Tukio la pili ni kuwepo kwa Yohana
Mbatizaji duniani kupitia Elizabeti mama yake. Mungu alisababisha matukio haya
mawili yatokee ili wanadamu waweze kuokolewa kwa
dhambi zao zote.
Hii ni kazi ambayo Mungu aliipanga katika utatu. Mungu
alimtuma Yohana Mbatizaji ulimwenguni miezi sita kabla ya Yesu, ndipo akatumwa
Yesu Kristo mwokozi wa
wanadamu hapa duniani kuwaweka huru wanadamu tokana na
hukumu ya dhambi zao.
Yesu
alishuhudia juu ya Yohana Mbatizaji katika Mathayo 11:9
“Lakini kwa nini mlitoka? Ni
kuona Nabii? Naam, nawaambia
na aliye mkuu zaidi ya Nabii”. Zaidi
ya yote, pale Yohana Mbatizaji aliyemtwika dhambi zote za ulimwengu Yesu, alipo
mwona tena siku aliyofuata yeye mwenyewe alishuhudia kwa kusema “Tazama! mwana kondoo aichukuaye dhambi ya ulimwengu” (Yohana 1:29).
Biblia
ina taarifa nyingi za Yohana, aliye mbatiza Yesu na inatupasa kupekuwa na kutafuta
ili kuweza kuwa na ufahamu mzuri juu yake. Yohana Mbatizaji alikuja ulimwenguni
kabla ya
Yesu
jukumu lake likiwa kutimiza Injili njema ambayo ndiyo mpango wa Mungu. Biblia
inasema kwamba Yesu alikubali dhambi zote za ulimwengu juu yake toka kwaYohana,
naye Yohana
alimtwika dhambi hizo juu yake ili kutimiza mapenzi ya Mungu.
Tunamwita
kuwa ni Yohana Mbatizaji kwa sababu alimbatiza Yesu. Ubatizo wa Yesu una maana
gani? Neno “ubatizo” linamaanisha “kuoshwa” kwa kuwa dhambi zote zimekwisha
kutwikwa juu ya Yesu kwa kupitia ubatizo wake, hivyo basi zimekwisha kuoshwa.
Ubatizo wa Yesu una maana sawa na tendo la “kuwekea mikono” ambalo ile sadaka
ya dhambi ilipokea katika Agano la Kale. Maana ya kiroho ya tendo la ubatizo ni
“kutwika, kuoshwa au kuzikwa”. Ubatizo wa Yesu kwa Yohana ulikuwa ni tendo la
ukombozi katika kuondoa dhambi zote za watu wa ulimwengu.
Ubatizo
wa Yesu unaumuhimu sawa kama ilivyo tendo la kuwekea mikono, ambapo ni njia ya
kutwika dhambi juu ya sadaka ya dhambi katika Agano la Kale. Kwa maneno
mengine,
watu
wa Israeli walitwika dhambi zao za mwaka mzima juu ya sadaka ya dhambi katika
siku ya Upatanisho kwa kupitia tendo la kuwekea mikono ya kuhani mkuu. Sadaka
hii katika Agano la Kale
ilikuwa na dhambi sawa na ubatizo wa Yesu na kifo chake msalabani.
Mungu
aliiteuwa siku ya Upatanisho kuwa ni muda wa kuondoa dhambi za wana wa Israeli.
Katika siku ya kumi ya mwezi wa saba, kuhani mkuu alitwika dhambi za mwaka za watu
wake juu ya kichwa cha sadaka ya dhambi kwa kuwekea mikono juu ya sadaka kwa upatanisho
wa dhambi za watu. Na huu ndio mpangilio wa utoaji wa sadaka ambao Mungu aliuweka.
Ilikuwa ndio njia pekee katika kutwika dhambi za watu juu ya sadaka ya dhambi
na alifanya hivyo kwa tendo la kuwekea mikono ambalo ndiyo sheria ya milele
Mungu aliyoweka.
“Na Haruni ataweka mikono yake
miwili juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai, na kuungama juu yake uovu wote
wa wana wa Israeli na makosa yao, naam dhambi zao zote, naye
ataziweka juu ya kichwa chake
yule mbuzi kisha atampeleka aende jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari na
yule mbuzi atachukua juu yake uovu wao wote, mpaka nchi isiyo watu, naye atamwacha
mbuzi jangwani” (Walawi 16:21-22).
Katika
Agano la Kale, mwenye dhambi aliweka mikono juu ya kichwa cha sadaka ya dhambi
na kutwika dhambi zake juu yake ili aweze kusamehewa. Na siku ya Upatanisho
Haruni Kuhani Mkuu akiwa mwakilishi wa Waisrael wote, aliweka mikono yake juu
ya kichwa cha sadaka ya dhambi ili kutwikwa sadaka hiyo dhambi zote za
Waisraeli. Ndipo sadaka hiyo huchinjwa
baada ya kubeba dhambi hizo.
Tendo
hilo linamaana sawa ya kiroho kwa ubatizo (“Baptisma” ni Kigiriki, maana yake “kusafisha
kuzikwa kutwikwa”) ambapo Yesu aliupokea toka kwa Yohana katika Agano Jipya.
Kama alivyokuwa Kuhani Mkuu katika Agano la Kale alipoweka mikono yake juu ya
sadaka ya dhambi ili kutwika dhambi za watu wa Israel, ndivyo hivyo dhambi zote
za wanadamu zilitwikwa juu ya Yesu kupitia ubatizo wake na Yohana Mbatizaji.
Ndivyo Yesu alivyokufa Msalabani katika kutupatanisha kwa dhambi zetu.
Hii
ni Injili njema. Kama ilivyo Haruni kuhani Mkuu alivyotoa sadaka ya Upatanisho
kwa niaba ya watu wa Israeli, Yohana Mbatizaji naye aliye uzao wa Kuhani Haruni
alichukua jukumu hilo akiwa mwakilishi wa wanadamu juu yake Yesu. Mungu
anaeleza mpango huu ulio mzuri wa ajabu kuhusiana na upendo wake katika Biblia
kama ifuatavyo katika kitabu cha Zaburi 50:4-5 “Ataziita mbingu zilizo juu na
Nchi pia wahukumu watu wake. Nikusanyieni wacha Mungu wangu waliofanya Agano
nami kwa dhabihu” Amen, Haleluyah.
Historia
ya Kanisa inasema kwamba hapakuwepo na Krismasi kwa karne mbili za mwanzo
katika kuanzishwa kwake. Kanisa la Wakristo wa mwanzo pamoja na Mitume wa Yesu
waliadhimisha
January 6 kama “Siku ya Ubatizo wa Yesu” tu, uliofanyika katika mto Yordani na
Yohana Mbatizaji. Kwa nini waliweka msisitizo zaidi katika hilo, yaani ubatizo
wa Yesu katika imani yao? Jibu lake ndilo ufunguo halisi wa Ukristo wadesturi
ya Kitume.
Lakini
natumaini hamtochanganya ubatizo wa waumini na ule ubatizo wa Yesu. Ubatizo wa
waumini kama ilivyo siku hizi una maana tofauti na ule ubatizo wa Yesu
alioupokea katika mto Yordani. Hivyo imetupasa sisi sote kupokea uwepo wa Roho
Mtakatifu kwa kuamini ubatizo wa Yesu Kristo ambao alioupokea toka kwa Yohana
na pia damu yake Msalabani. Ikiwa mtazamo wa Kanisa la kwanza uliweka
kipaumbele juu ya hili kuwa ndilo Sakramenti muhimu, basi hili kwao waliona
ndiyo egemeo la imani katika ubatizo wa Yesu na hivyo hata sisi leo hii
tuchukulie ubatizo wa Yesu kwa Yohana kuwa ni sehemu isisyo epukika katika
wokovu wetu.
Zaidi
ya yote ni lazima tuufikie na kuikumbatia imani iliyo sahihi yenye ufahamu
kamili ambayo husema kwamba Yesu ilimbidi asulubiwe kutokana na kubatizwa kwake
na Yohana. Imetupasa
kuelewa
kwamba Roho Mtakatifu huanza kuweka makazi ndani yetu pale tu tunapoamini
ubatizo wa Yesu, kufa kwake msalabani na kufufuka kwake ili awe Mwokozi wetu.
Ubatizo wa Yesu kwa Yohana na damu yake msalabani vyote vinamaana ya pakee
katika Injili njema.
Njia
ya tahadhari kwako katika kumpokea Roho Mtakatifu ni kuamini Injili njema ya
ubatizo wa Yesu na damu yake. Ubatizo wa Yesu ulitakasa dhambi zote za wanadamu
mara moja. Ulikuwa ni ubatizo wa ukombozi uliopelekea kwetu kumpokea Roho
Mtakatifu. Kwa kuwa baadhi ya watu hawajagundua nguvu iliyomo katika ubatizo wa
Yesu, basi wao huelewa hili kuwa ni kama sherehe ya kawaida.
Ubatizo
wa Yesu hufanya sehemu muhimu katika Injili njema ambayo hutueleza namna ile
Yesu alivyobeba dhambi zote za ulimwengu juu yake na hata kuikubali hukumu yake
kwa kumwaga damu yake msalabani. Yeyote anayeamini maneno ya Injili hii iliyo
njema hufanywa kuwa msharika wa Kanisa ambalo linamilikiwa na Bwana, na
kufurahiya baraka ya Roho Mtakatifu.
Roho
Mtakatifu ni karama toka kwa Mungu kwa wale wote waliokwisha kusamehewa dhambi
zao. Kwa ubatizo wake, Yesu alikuwa “Mwanakondoo
wa Mungu
aichukuaye dhambi ya ulimwengu” kwa
namna iliyotosha (Yohana 1:29). Katika Yohana 1:6-7 inasema “Palitokea mtu
ametumwa kutoka kwa Mungu jina
lake Yohana. Huyo alikuja kwa ushuhuda ili ashuhudie ile nuru, wote wapate
kuamini kwa yeye”. Ili kumwamini Yesu kuwa ni mwokozi wetu
aliyechukua
dhambi
zetu zote ni lazima tuelewe juu ya huduma ya Yohana na ushuhuda kama ilivyo
andikwa katika Biblia. Ndipo tutaweza kumwamini Yesu Kristo kama Mwokozi wetu.
Ili kuweza kumpokea Roho Mtakatifu pia tunahitajika kuwa na imani madhubuti
iliyoshuhudiwa moyoni.
Hivyo
kukamilisha Injili ya kweli iliyo njema ni lazima kuamini ubatizo wa Yesu kwa
Yohana
na damu yake pale msalabani. Katika Mathayo 11:12
imeandikwa “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa Ufalme wa
mbinguni hupatikana kwa nguvu
na wenye nguvu wauteka”. Kifungu hiki husemekana kuwa ndicho kifungu kigumu kueleweka
kati ya vifungu kadha katika Biblia. Hata hivyo imetupasa kuwa makini kwa
sehemu isemayo “Tangu siku za Yohana Mbatizaji”. Hakika hapa inatangaza kwamba
huduma ya Yohana ilikuwa iimeunganika moja
kwa moja na huduma ya Yesu kwa wokovu wetu.
Yesu
anatuhitaji tuingie katika Ufalme kwa ujasiri wa imani kama ulivyo ujasiri wa
mwenye nguvu. Tunatenda dhambi kila leo, sisi ni dhaifu lakini ameruhusu tuweze
kuingia katika Ufalme wake kwa imani, kifua mbele bila ya kujali udhaifu wetu.
Hivyo kifungu hiki kina maana kwamba watu wataweza kuuteka Ufalme wa mbingu kwa
imani katika Injili njema isemayo kwamba Yesu amefuta dhambi zote za ulimwengu
kwa kupitia ubatizo wake kwa Yohana na damu yake msalabani. Kwa
maneno mengine ina maana kwamba mbingu inawezwa kutekwa kwa imani madhubuti
katika Injili hii njema ya ubatizo wa Yesu na damu yake.
Ubatizo
wa Yesu ndiyo uliobeba dhambi zote na imani yetu juu yake hatupa uhakika kwamba
tutapokea uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yetu. Lazima tuhubiri Injili hii kwa
majirani zetu,
ndugu zetu, wapendwa wetu na kwa yeyote Yule ulimwenguni. Lazima tuwe na imani
katika Injili njema ambayo inasema kwamba dhambi zetu zote ulimwenguni
zilitwikwa kwake
Yesu kupitia ubatizo wake. Kwa kupitia imani yetu ndipo basi tutaweza kupokea
tulizo la ukombozi na uwepo wa Roho Mtakatifu ndani. Kila mtu ataweza kuwa
mwana wa Bwana ambamo ndani yake Roho Mtakatifu atakaa, kuwa moja kati ya kaka
na dada kwa kuamini Injili njema ya maji na Roho. Ni lazima muwe na imani sawa
katika Injili njema kama aliyokuwa nayo Paulo. Namshukuru Bwana kwa kutupa
Injili njema na kumsifu yeye. Ameni.