( Mathayo 27: 50-53) “Naye
Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake. Na tazama, pazia
la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka;
miamba ikapasuka; makabuli yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu
waliolala; nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake,
wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi.”
Patakatifu pa patakatifu palikuwa ni mahali ambapo Mungu
aliishi. Na ni kuhani mkuu tu ndiye aliye ruhusiwa kuingia hapo mara moja kwa
mwaka, katika ile siku ya Upatanisho hali akiwa amebeba damu ya mbuzi wa sadaka
ya kuteketezwa kwa ajili ya ondoleo la dhambi la Waisraeli. Kuhani mkuu
alifanya hivyo kwa sababu Patakatifu pa patakatifu katika Hema Takatifu la
kukutania Palikuwa ni mahali patakatifu sana ambapo hawakuweza kuingia mpaka
awe na damu ya mwanasadaka, ambaye kwa huyo mikono iliwekwa juu ya kichwa chake
ili kuyatowesha mbali maovu ya wenye dhambi. Kwa msemo tofauti, hata kuhani
mkuu hakuweza kuikwepa adhabu ya Mungu hadi baada ya kuwa amepokea ondoleo la
dhambi zake kwa kutoa sadaka ya kuteketezwa kabla ya kuingia katika uwepo wa
Mungu.
Je, ni lini pazia la Hekalu lilipasuka? Lilipasuka
wakatiYesu alipoimwaga damu yake na kufa Msalabani. Kwa nini ilimpasa Yesu
kumwaga damu yake Msalabani na kisha kufa? Kwa sababu Yesu mwana wa Mungu kwa
kuja kwake hapa duniani katika mwili wa mwanadamu alikuwa ameyachukuwa katika
mwili wake maovu yote ya wenye dhambi kwa kubatizwa na Yohana katika mto
Yordani. Kwa sababu Yesu alikuwa amezichukuwa katika mwili wake dhambi zote za
ulimwengu kwa kupitia ubatizo wake, basi Yesu aliweza kuzimaliza adhabu zote za
dhambi ikiwa tu angeliimwaga damu yake na kisha kufa msalabani. Hii ndiyo
sababu lile pazia lililokuwa likitenganisha kati ya mahali patakatifu na Patakatifu pa patakatifu
lilipasuka toka juu mpaka chini. Hii inamaanisha kuwa ule ukuta wa dhambi ambao
ulimtenganisha Mungu na mwanadamu ulikuwa umeanguka chini mara moja na daima.
Kwa maneno mengine, kupitia ubatizo ambao Yesu aliupokea na damu yake aliyoimwaga Msalabani, Yesu
amezifanya dhambi zote kutoweka. Kwa ubatizo na damu ya Yesu Kristo, Mungu baba
amezitowesha mbali dhambi zetu zote mara moja na kwa wote na ameufungua mlango
wa Mbinguni, ili kwamba mtu yeyote aweze kuingia Mbinguni kwa kuamini katika
ubatizo huu na damu ya Yesu iliyomwaguka.
Wakati Yesu alipokuwa msalabani, giza lilifunika pale
alipokuwepo kwa masaa matatu. Baada ya kuwa amezibeba dhambi zote za ulimwengu
kwa kupitia ubatizo wake katika mto Yordani, Yesu alisulubiwa na karibu na kifo
chake alilia, “Eloi, Eloi, lama
sabaktani?” maana yake, “Mungu wangu,
Mungu wangu, mbona umeniacha?” (Mathayo 27:46).
Kisha akisema neno lake la mwisho, “Imekwisha!”
kisha akafa, na baada ya siku tatu akafufuka kena toka kwa wafu, akabeba
ushuhuda kwa siku 40, na kisha akapaa Mbinguni mbele ya macho ya wanafunzi wake
na wafuasi wake wengi.
Je, ni kweli kuwa Baba alikuwa amemwacha Yesu?
Kwa sababu Yesu alikuwa amezichukuwa dhambi za ulimwengu
katika mwili wake kwa kubatizwa na Yohana, Yesu alikuwa ameachwa kwa muda na
Baba pale alipokuwa amezibeba adhabu ya dhambi Msalabani. Mungu Baba alipaswa
kumuadhibu mtu yeyote ambaye alikuwa na dhambi, na kwa sababu dhambi zote za
ulimwengu zilikuwa zimepitishwa kwa Yesu, basi Yesu alipaswa kuraruliwa na
kisha kuimwaga damu yake msalabani kama adhabu ya dhambi hizi.
Kwa sababu Yesu ni Mungu mwenyewe katika uwepo wake alikuwa
amezichukuwa dhambi zote za wanadamu katika mwili wake kwa kubatizwa, basi
dhambi za ulimwengu zilikuwa zimehamishwa katika mwili wake Mtakatifu. Kwa
hiyo, alipaswa kuachwa na Mungu Baba kwa kitambo tu, kuteseka hadi kifo
Msalabani ili kulipa mshahara wa dhambi zote.
Kama ambavyo unafahamu, baada ya kujengwa kwa Hekalu katika utawala
wa mfalume Sulemani, basi nafasi ya Hema Takatifu la Kukutania ilichukuliwa na Hekalu.
Lakini msingi wa utaratibu wa Hema Takatifu la kukutania iliendelea kutumika
katika Hekalu kama ambavyo ilikuwa ikitumika katika Hema takatifu la kukutania kabla Hekalu halijajengwa . kwa
hiyo, kulikuwa na pazia ambalo lilitenganisha kati ya mahali patakatifu na
Patakatifu pa patakatifu katika hekalu. Na wakati ule ule Bwana alipopiga
kelele Msalabani, “Eloi, Eloi, Eloi, lama
sabaktani?” pazia hili la Hekalu lilipasuka toka juu hadi chini. Ukweli
unaozungumziwa na tukio hili ni kuwa kwa sababu Bwana amezioshelea mbali dhambi
zetu kwa ubatizo ambao aliopokea na kwa damu ya thamani ambayo aliimwaga
Msalabani, basi sasa lango la Mbinguni limefunguliwa ili kwamba wote wanaoamini
waweze kuingia. Sasa kwa kuamini katika Injili ya maji na Roho, sisi sote
tunaweza kuingia Mbinguni kwa imani.
Ule ukweli kuwa pazia la Hekalu lilipasuka toka juu hadi
chini wakati Yesu alipokufa Msalabani unatufundisha sisi ukweli kwamba katika
kipindi hiki, wale wote ambao wamesafishwa toka katika dhambi kwa kuamini
injili ya maji na Roho na damu wanaweza kuingia Mbinguni. Kulikuwa na ukuta wa
dhambi ambao ulikuwa umetutenganisha uliokuwa ukituzuia sisi kuja mbele za
Mungu, lakini kwa ubatizo na damu yake, Yesu ameufanya huu ukuta wa dhambi
kupotea mara moja na kwa wote. Kule kusema kuwa Muungu alilipasua pazia la
Hekalu toka juu hadi chini kunamaanisha kuwa yeyote anayeamini katika ubatizo
ambao kwa huo mwana wa Mungu aliyachukuwa katika mwili wake maovu yote ya wenye
dhambi na katika damu ya msalaba anaweza kusafishwa dhambi zake kikamilifu na
kisha kuingia Mbinguni. Mungu ametuokoa sisi toka katika dhambi kwa namna hii.
Yesu alilipasua pazia la Hekalu toka juu hadi chini kuwa
ushuhuda wa kazi hizi za wokovu ambazo alizitimiza. Kwa hiyo (Waebrania 10:19-22) inasema “Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia
patakatifu kwa damu ya Yesu, njia ile aliyotuanzia iliyo mpya, iliyo hai,
ipitayo katika pazia, yaani mwili wake; na kuwa na kuhani mkuu juu ya nyumba ya
Mungu: na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, hali
tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamira mbaya, tumeoshwa miili kwa maji safi.”
Wakati Yesu alipokufa msalabani, mlango wa kuingilia
Patakatifu pa patakatifu ulifunguliwa kwa kuwa pazia lake lilipasuliwa, na huu
mlango ulifunguliwa wa Patakatifu pa patakatifu ni neno la Mungu la Injili
ambalo limefungua njia mpya na iliyo hai ya kwenda Mbinguni. Hapa, Biblia
inatueleza sisi kuwa dhambi zote za mioyo yetu na miili yetu zilitoweshwa mbali
kwa kupitia ubatizo wake (maji safi) na damu yake, na kwa hiyo tunaweza
kusafishwa kwa uhakika wa imani katika wokovu wake mkamilifu.
Ni lazima kuwepo na “utimilifu
wa imani” kama ilivyo andika hapo juu, imani yoyote ambayo inaamini
katika mambo mawili tu, kwa mfano damu na Roho Mtakatifu haijakamilika. Kujua
kanini nasema hivi soma “Injili ya maji
na roho” katika blog hii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni