(Kutoka 27: 1-8) “Nawe fanya madhabahu ya mshita; urefu wake utakuwa ni
dhiraa tano; hivyo madhabahu itakuwa mraba; na kwenda juu kwake kutakuwa dhiraa
tatu. Nawe fanya pembe nne; hizo pembe zitakuwa za kitu kimoja na madhabahu;
nawe utayafunika shaba. Na vyombo vyake vya kuyaondoa majivu yake utavifanya,
na majembe yake, na mabakuli yake, na uma zake, na meko yake; vyombo vyake
vyote utavifanya vya shaba. Nawe uifanyie hiyo madhabahu wavu wa shaba; kisha
utie pete nne za shaba katika hizo pembe nne za ule wavu. Nawe tia huo wavu
chini ya kizigo kiizungukacho madhabahu upande wa chini, ili huo wavu ufikilie
katikati ya hiyo madhabahu, miti ya mshita, na kuifunika shaba. Na hiyo miti
itatiwa katika pete, na ile miti itakuwa katika pande mbili za madhabahu, wakati
wa kuichukuwa. Uifanye ya mbao, yenye mvungu ndani yake; kama ilivyoonyeshwa mlimani, ndiyo watakavyoifanya.”
Tujadili juu ya imani inayodhihirishwa katika madhabahu ya
sadaka ya kuteketezwa. Wakati watu wa Israeli walipovunja mojawapo ya kanuni
613 za sheria ya Mungu na maagizo yake ambayo walipaswa kuyatii katika maisha
yao ya kila siku, na walipozitambua dhambi zao walimtolea Mungu sadaka isiyo na
mawaa kwa mujibu wa utaratibu wa sadaka ya kuteketezwa uliowekwa na Mungu. Mahali walipozitolea sadaka
hizi ni katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa. Kwa maneno mengine, watu wa
Israeli, walipokea ondoleo lao la dhambi kwa kuwekea mikono yao katika kichwa
cha mnyama wa sadaka asiye na mawaa, na kwa kukata koo la mnyama na kuikinga
damu yake, na kuiweka damu hiyo katika pembe za madhabahu ya sadaka ya
kuteketezwa na kisha kuimimina ardhini damu iliyosalia, na hatimaye kumchoma
mnyama huyo katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa.
Maana ya kiroho ya madhabahu ya sadaka ya
kuteketezwa .
Wakati Waisraeli walipoiangalia madhabahu hii ya sadaka ya
kuteketezwa, ndipo walipotambua kuwa wao walikuwa wamefungwa katika kifungo cha
hukumu (Shaba) na adhabu na kuwa wasingeweza kuikwepa hukumu yao. Na kama
ambavyo mnyama wa sadaka ya kuteketezwa alivyouawa, ndipo walipotambua kuwa,
hata wao walistahili kufa kwa sababu ya dhambi zao. Pia waliamini kuwa masihi
atakuja hapa duniani na atazitowesha dhambi zao kwa kuwadhibiwa na kuuawa kama
ilivyokuwa kwa mnyama wa sadaka ya kuteketezwa kwa sababu ya dhambi zao.
Madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa ilikuwa ni kivuli cha
Yesu Kristo Mwokozi wetu. Kama ambavyo wanyama wasio na mawaa walivyouawa kwa
kuwekewa mikono na kisha kumwaga damu yao, Yesu Kristo alikuja kwetu kama Mwana wa Mungu na akabeba
adhabu ya dhambi zetu zote. Kama ambavyo sadaka ya kuteketezwa ya Agano la kale
alivyopokea dhambi zote kwa kuwekewa mikono na kumwaga damu, Yesu alizipokea
dhambi zote za ulimwengu zilizopelekwa kwake
kwa kubatizwa na Yohana, na akabeba adhabu ya dhambi hizi kwa kuimwaga
damu yake msalabani.
Kwa njia hii, madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa
inatuonyesha sisi kuwa Yesu Kristo alizichukuwa dhambi zetu akafufuka toka kwa
wafu, na kwa hiyo ametuokoa sisi.
Vyombo vyote vya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa
vilitengenezwa kwa Shaba
Vyombo vya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa vilivyotumika
kuweka na kuondoa majivu vyote vilitengenezwa kwa shaba. Madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa yenyewe ilitengenezwa kwa mti wa mshita na kisha
ikafunikwa kwa shaba, na kwa hiyo madhabahu na vyombo vyake vyote vilitengenezwa
kwa Shaba.
Shaba hii ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa ina maana
kamili ya kiroho. Shaba inamaanisha hukumu ya dhambi mbele za Mungu. Kwa hiyo,
madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa ni mahali panapotuonyesha vizuri kwamba
wenye dhambi kwa hakika watahukumiwa kwa dhambi zao. Kwa hakika, Mungu
atawaadhibu kwa dhambi zao pasipo kushindwa. Madhabahu hii ya sadaka ya
kuteketezwa ni mahali ambapo wnyama wa sadaka ya kuteketezwa walihukumiwa kwa
ajili ya wenye dhambi kwa kuteketezwa, madhabahu hii na Vyombo vyake vyote
vilitengenezwa kwa shaba; kwa hiyo, vitu hivi vinatueleza sisi kuwa kwa hakika
kila dhambi inahusisha hukumu yake.
Madhabahu inatuonyesha sisi kuwa kwa sababu ya dhambi zao,
watu wamefungwa kuwadhibiwa na kisha kuuawa, lakini kwa kuwaleta wanyama wao wa
kuteketezwa katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na kumpatia Mungu,
wanaweza kuoshwa dhambi zao, kupokea ondoleo la dhambi, na kisha kuishi tena
kwa upya. Hapa, sadaka zilizoteketezwa
katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa vyote vinatueleza kuwa ubatizo wa Yesu
Kristo na kule kuimwaga damu yake kumezisamehe dhambi za waamini. Kwa hiyo,
imani hii iliyotoa sadaka ya kuteketezwa katika madhabahu ya sadaka ya
kuteketezwa inaendelezwa katika kipindi cha Agano jipya kama imani katika
ubatizo na damu ya Yesu Kristo.
Tunapomwamini Yesu Kristo kuwa ni mwokozi wetu, ni lazima
tumpe Mungu imani Yetu inayoamini katika ubatizo na damu ya Yesu kama ondoleo
la dhambi zetu zote. Katika Agano la kale, imani hii inahusianishwa na imani
inayofungua na kuingia katika lango la ua wa Hema takatifu la kukutania
lililokuwa limefumwa kwa nyuzi za bluu,zambarau, na nyekundu, na kitani safi ya
kusokotwa.
Sadaka zote ambazo ziliteketezwa katika
madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa ni kivuli cha Yesu Kristo.
Yesu Kristo alifanya nini alipokuja hapa duniani? Tulikuwa wenye
dhmbi; tulikuwa tumetenda dhambi kinyume na Mungu na Tulikuwa tumevunja sheria
na maagizo yake. Lakini ili kuzitowesha dhambi zetu, Yesu Kristo alibatizwa na
Yohana na alichukuwa dhambi za ulimwengu katika mwili wake, na kwa hiyo
akamwaga damu yake msalabani. Bwana wetu alibeba hukumu ya adhabu kwa dhambi
zetu zote ili sisi tusiadhibiwe kwa dhambi zetu. Kwa hiyo, ametuokoa toka
katika dhambi zetu zote na adhabu.
Pia kuna maana nyingine ya madhabahu ya sadaka ya
kuteketezwa, ambayo ni “kupaa.” Kusema kweli, wewe na mimi tunatenda dhambi
kila siku. Kwa hiyo, inatulazimu kutoa sadaka zetu za kuteketezwa kila wakati
mbele za Mungu, na kwa sababu ya hali hii, moshi wa adhabu ya dhambi zetu kila
siku unapaa kwenda kwa Mungu. Je, kuna siku yoyote ambayo hautendi dhambi bali
unaishi kikamilifu? Sadaka ya kuteketezwa ya watu wa Israeli ilitolewa kila
siku hadi pale makuhani walipochoka kuzitoa hizi ambazo zilileteleza msamaha wa
dhambi za Waisraeli wengi. Kwa sababu watu wa Israeli walivunja sheria na
wakafanya dhambi kinyume na Mungu kila siku, vivyo hivyo walipaswa kutoa sadaka
zao za kuteketezwa kila siku.
Musa, akiwakilisha taifa la Israeli, alizitamka kanuni 613
za sheria na amri za mungu kwa Waisraeli; “sasa
basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika Agano langu, hapo
ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kiliko makabila yote ya watu; maana dunia yote
pia ni mali yangu. Nanyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu. Hayo
ndiyo maneno utakayowaambia wana wa Israeli” (kutoka 19:5-6).
Kisha watu wa Israeli wakaahidi, “hayo
yote aliyoyasema BWANA tutayashika” (kutoka 19:8). Hivyo watu wa Israeli
walitaka kumtambua na kumwamini huyu Mungu aliyemtokea Musa na akaongea nao kwa
kupitia Musa kama Mungu wao Halisi, na walitaka Mungu huyu awalinde. Kwa hiyo, walijitahidi kuzituza amri zote za
Mungu ambazo aliwapatia.
Je, Mungu alifahamu mapema kuwa Waisraeli watatenda dhambi? Kwa
kweli alifahamu. Hii ndiyo sababu Mungu alimwita Musa katika mlima Sinai,
akamwonyesha Hema Takatifu la kukutania katika maono, akamweleza juu ya muundo
wake wa kina, na kisha akamfanya Musa kulijenga kama alivyo mwamuru. Pia
akaanzisha utaratibu wa sadaka ya kuteketezwa ambao kwa huo sadaka zilipaswa
kutolewa katika hili Hema Takatifu la kukutania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni