Alhamisi, 27 Machi 2014

VIPAWA VYA ROHO MTAKATIFU


Tukiangalia Biblia tunaweza kuona vipawa vya Roho mtakatifu vinatajwa sehemu tofauti tofauti. Vipawa hivi vinawakilishwa na warumi 12:6-8, 1 wakorintho 12:8-10 na waefeso 4:11. lakini leo hebu tuangalie vipawa tisa vilivyotajwa katika 1wakorintho 12.
1) Kipawa cha Neno la ufahamu. Huu ni ufahamu wa siri ya Injili ya maji na Roho iliyofichika kulingana na uvuvio wa Mungu, katika maandiko ya Biblia yenye nguvu ya Roho mtakatifu. Uwezo wa kueleza na kueneza Injili hii ya maji na Roho hii kipawa cha Neno la ufahamu.
2) Kipawa cha Neno la Busara. Kipawa cha neno la busara haina maana ya busara ya kibinadamu kama vile akili na utambuzi. Kipawa hiki cha kile cha kutatua matatizo mbalimbali yaletwayo na wanadamu katika kueleza neno la Biblia kwa imani.
3) Kipawa cha Imani. Kipawa cha Imani ni ile hali ya kuonyesha imani ya matendo katika Neno. Kipawa hiki hutolewa pale tunapolisikia neno la Mungu na tunapoliamini neno hili kwa imani thabiti. Roho mtakatifu anafanya kazi ili imani yetu ikue ndani ya mioyo yenu. Kwa kipawa hiki, Mungu anatuwezesha kuziokoa Roho za watu kutoka katika dhambi zao.
4) Kipawa cha Uponyaji: Badala ya kujaribu kuponya magonjwa ya mwilini, mitume lazima watambue kuwa Mungu anawataka watambue mapenzi ya Mungu kupitia madhaifu yao ya mwilini. Anataka wajue ukuu wa Mungu kupitia magonjwa walio nayo, yeye anaangalia uponyaji wa kiroho zaidi kwanza kuliko yale ya kimwili. Mungu anatushauri kuwaombea wagonjwa (James 5:14-15) na sala hizi ni zile ambazo kila mtakatifu anaweza kusema.
5) Kipawa cha kutenda miujiza. Hii ni ile nguvu ya imani inayoamini na kufuata neno la Mungu miujiza inalenga imani inayoamini neno la Mungu linalotengua sheria ya asili ya Imani ambazo zinafahamika Imani hiyo ya mitume inajenga nguvu katika imani zetu na kutuwezesha kuzaa matunda zaidi. Mungu anawafanya mitume watende kwa imani.
6) Kipawa cha Unabii. Hii ni kuamini neno la Mungu na kulieneza kwa niaba yake. Tangu Agano la kale hata jipya Mungu ametufunulia mapenzi yake na mipango. Hivyo manabii wa kweli ndio wanaoweza kuthibitisha usahihi au makosa ya wengine katika maandiko ya neno la Mungu. Kwa hiyo wale wasioeneza neno la Mungu lililoandikwa katika maandiko kwa imani za manabii wa uwongo. Unabii sahihi ni kueneza neno la Mungu kwa imani. Kwa kuwahubiria watu neno la Mungu mitume na watumishi wa Mungu ni lazima wawawezeshe kumwabudu Mungu, kufariji na kuhimizana. Yesu kristo ametoa pamoja na mwili wake, kanisa, kipawa cha imani inayoamini neno la watumishi wa Mungu.
7) Kipawa cha kupambanua Roho. Kupambanua Roho ni kipawa au uwezo wa kutambua kama watu wamepokea ondoleo la dhambi au tu wamesikia kinachosemwa. Kwetu sisi tunaoishi nyakati hizi za mwisho, kama hatuna kipawa hiki, tunadanganywa na shetani (1 Timotheo 4:1) na kipawa hiki, tunaweza kuwatambua wale wanaotafuta na kufuata vipawa vya Roho mtakatifu, na kuweza kutofautisha kati ya aliyezaliwa upya na yule ambae hajapokea ondoleo la dhambi na Roho mtakatifu.
8) Kipawa cha kunena kwa lugha. Inaposemwa kuwa mitume wanaongea kuwa lugha ina maana wanaongea ukweli juu ya ufalme wa mbinguni. Mitume wanapomwomba Mungu,, ni rahisi sana kwao kunena kwa lugha, ambayo inaeleweka na Mungu pekee. Licha ya kujaribu kunena, ni sharti tuweke mkazo katika kuelewa Neno la Biblia. Ni lazima tutambue kuwa ni bora kuongea maneno matano tunayoyaelewa na kuwafunza wengine kuliko kunena maneno elfu kumi (1 Wakorintho 14:19).

9) Kipawa cha kutafsiri ndimi. Huu ni uwezo wa kufundisha mapenzi ya Mungu ili kila mmoja aelewe kuwa kutafsiri neno lililotoka kwa Mungu kipawa hiki cha kutafsiri lugha kilitolewa na kanisa la kwanza kwa lengo la kueneza Injili, na sasa kinaweza kuonekana katika huduma ya kutafsiri na kufafanua mafundisho ya Injili. Kama mtu akiweza kuongea kwa lugha za kienyeji, hawezi kuhitaji mtafsiri, ila yule anayeweza kuongea lugha nyingi za duniani anahitaji mtu wa kutafsiri.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni