Jumamosi, 31 Mei 2014

INJILI YA MAJI NA ROHO

MAANA YA UBATIZO
Ubatizo maana yake kusafishwa, kuzikwa, (kuzamishwa) na maana ya kiroho kutwikwa dhambi kwa kuwekea mikono, kama ilivyofanywa katika Agano la kale, (Walawi 4:29, 16:21).
Wakati wana wa Israeli walipotoa sadaka ya upatanisho katika nyakati za Agano la Kale, isingekuwa njia sahihi kumchinja mnyama wa sadaka pasipo kwanza kuwekewa mikono juu ya kichwa chake kwa kutwikwa dhambi juu yake kwa niaba yao na ilikuwa ni kuonyesha jinsi ya ubatizo wa Yesu utakao kuja katika Agano Jipya. Hivyo inakuwa ni kosa na kuvunja sheria ya Mungu kuamini msalaba wa Yesu pekee bila kuamini pia ubatizo wake.
Katika Agano Jipya, ubatizo wa Yesu na Yohana Mbatizaji ulikuwa ni kusafisha dhambi za ulimwengu. “ubatizo wa Yesu” una maana ya kuchukua dhambi zote za wanadamu, kutakaswa kwa dhambi zote za ulimwengu.
Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizaji, mwakilishi wa wanadamu na kuhani mkuu katika uzao wa Haruni, na kubebeshwa dhambi zote za ulimwengu juu yake. Hili ni dhumuni kuu la ubatizo.
Maana ya kiroho neno “ubatizo” ni “kutwika, kuzikwa” Hivyo “ubatizo wa Yesu” maana yake dhambi zote alitwikwa Yesu na kuhukumiwa badala yetu. Ili kuokoa wanadamu, Yesu alizibeba dhambi zetu zote kwa ubatizo wake na kufa kwa dhambi hizo.
Yote haya, kifo chake na pia kifo chako na changu wenye dhambi wote ulimenguni na ufufuko wake ni ufufuo wa watu wote. Kujitoa kwake sadaka ni wokovu wa wenye dhambi na ubatizo ni ushuhuda Halisi katika kutusafisha dhambi zetu zote sisi walimwengu. Hivyo, Mtume Paulo alisema “Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi; (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamira safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo. (1Petro 3:21)
Sisi kama waumini wa Kristo yatupasa kujifunza maana halisi ya ubatizo, maana katika huo tunapata wokovu. Maji hayana la kufanya katika wokovu, bali ni ishara ya nje ya kile ulichokiamini ndani yako.
Rejea maandiko haya katika Biblia “Basi Myahudi mmoja, jina lake Apolo, mzalia wa Iskanderea. Mtu wa elimu akafika Efeso; alikuwa hodari katika maandiko. Mtu huyo alikuwa amefundishwa njia ya Bwana; Na kwa kuwa roho yake ilikuwa ikimwaka, alianza kunena na kufundisha kwa usahihi habari za Yesu; naye alijua ubatizo wa Yohana tu. Akaanza kunena kwa ujasiri katika sinagogi; hata Prisila na Akila walipomsikia wakamchukuwa kwao, wakamweleza njia ya bwana kwa usahihi zaidi. (Matendo 18:24-26)
Apolo aliyajua maandiko na alijua ubatizo wa Yohana tu, ambao haukuwezesha waumini kupokea Roho Mtakatifu, hata Prisila na Akila walipomsikia walimchukua na kumfundisha njia ya bwana kwa usahihi zaidi. Hata leo hii kuna watu wengi hawajui maana ya ubatizo kwa ujumla wake. Kwanini Apolo alifundishwa njia ya bwana kwa usahihi zaidi? Jibu la swali hili tutalipata katika aina nyingine ya ubatizo wa Yesu.
Watu wengi ulimwenguni hawafahamu ni kwanini Yesu alikuja katika ulimwengu na kubatizwa na Yohana Mbatizaji. Hivyo hebu tuzungumzie sababu za ubatizo wa Yesu na juu ya Yohana Mbatizaji aliyembatiza Yesu.
Kwanza, yatupasa kuwaza juu ya nini kilichomfanya Yohana Mbatizaji abatize watu katika mto Yordani. Inaelezwa katika( Mathayo 3:1-12) kwamba Yohana Mbatizaji alibatiza watu ili kuwalejesha kwa Mungu toka katika dhambi kwa kutubu kwao.
Kimsingi umuhimu wa ubatizo uliofanywa na Yohana Mbatizaji ulikuwa kwaajili ya toba ambayo iliwarudisha Waisrael kwa Yesu ambaye angekuja baadaye. Toba maana yake kugeuka toka maisha ya dhambi na kumwani Masiya ili kusamehewa dhambi zote.
Jambo la kwanza Yesu alilolifanya katika huduma yake ya wazi ilikuwa ni kubatizwa na Yohana Mbatizaji. Dhambi zote za ulimwengu zilitwikwa juu yake kwa njia hii.
Hivyo ubatizo wa Yesu ulikuwa ndiyo mwanzo wa wokovu wa Mungu kwa wanadamu pamoja pia na tendo la haki kwa Yesu kuweza kutakasa dhambi zote za ulimwengu juu yake kwa njia ya ubatizo.
Yesu alikuja ulimwenguni na kubatizwa na Yohana Mbatizaji, injili ya ufalme wa Mbinguni ndipo ilipoanza. Mbingu zilifunuka kwa ubatizo wake kama ilivyoelezwa katika Mathayo 3:15 ilikuwa sawa sawa kabisa na sadaka ya upatanisho iliyoelezwa katika (Walawi 1:1-5, 4:27-31) nyakati za Agano la kale.
Moja ya mafundisho potofu katika nyakati hizi za imani ya kikiristo ni kwamba, utaweza kuokolewa unapomkiri Yesu kuwa mwokozi kwa kuwa bwana ni pendo. Biblia inasema “Yeyote aliitaye jina la Bwana ataokolewa” (Matendo 2:21, Warumi10:13) ambapo pia inasema “Si kila mtu aniitaye Bwana Bwana ataingia ufalme wa mbinguni, bali wale wote watendao mapenzi ya Baba yangu wa Mbinguni”(Mathayo 7:21).
Kwanini tujifunze ubatizo kwa undani, hebu soma kifungu hichi” Ikawa, Apolo alipokuwa Korintho, Paulo, akiisha kupita kati ya nchi za juu, akafika Efeso; akakutana na wanafunzi kadha wa kadha huko, akawauliza je? Mlimpokea Roho Mtakatifu Mlipoamini? Wakamjibu, La hata kusikia kwamba kuna roho Mtakatifu hatukusikia. Akawauliza mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, kwa ubatizo wa Yohana. Paulo akisema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu.” (Matendo 19:1-4)
“Je ulipokea Roho Mtakatifu pale ulipoamini?” hata waKristo swali hili hawalifahamu. Mtume Paulo aliwauliza waamini wa Yesu kama walipokea Roho Mtakatifu pale walipoamini kwa mara ya kwanza na akafafanua jinsi waamini wanavyoweza kumpokea Roho Mtakatifu. Katika fungu hili la maneno kwa kupata ushuhuda wa nguvu ya ubatizo wa Yesu, Paulo aliamsha imani zao tena. Apollo alipokuwa Korintho, baada ya Paulo kupita Asia ndogo, na kufika Efeso, na kuwakuta wanafunzi wa Yesu, aliwaambia, “Je mlipokea Roho Mtakatifu mara mlipoamini?” Usharika wa korintho haukuelwa lolote juu ya ukweli huu, kuwa wanapokea Roho Mtakatifu wakimwamini Yesu.
*      Wangelijua na kuamini ubatizo ambao Yesu alipokea
Kusikia kuwa walikuwa wamebatizwa kupitia ubatizo wa Yohana pekee, Paulo alifafanua juu ya mahusiano ya ubatizo wa Yesu na ule wa Roho Mtakaifu. Ndipo wakaelewa maana ya ubatizo wa Yesu walioupokea. Kuna tofauti kubwa sana kati ya kumwamini yeye huku tukijua maana ya ubatizo ambao Yesu alipokea kutoka kwa Yohana, na kumwamini yeye bila kujua maana ya mahusiano ya ubatizo wa Yesu na ule wa Roho Mtakaifu. Ndipo wakaelewa maana ya ubatizo wa Yesu walioupokea.
Sasa je, ni ubatizo gani Yohana aliutoa kwa watu? Yohana aliwaambia watu kutubu, kuikimbia dhambi na kumrudia Mungu. Ubatizo ambao Yohana aliutoa ulikuwa ni ubatizo wa kutubu ambao uliwafanya watu watubu. Lakini ubatizo ambao Yesu alipokea kutoka kwa Yohana katika Mathayo 3:13-17 ulipokewa ili kuitimiza haki ya Mungu, na ndio maana tunasema ulikuwa tofauti na wa Yohana.
Ubatizo ambao Yesu aliupokea kutoka kwa Yohana ulikuwa wa kuondoa dhambi za wanadamu.
Imani yao ilikuwa tofauti kabisa na imani ya Paulo, kwani ubatizo walioupokea haukuwa wa kujua picha halisi ya ukweli huu.
Sasa ubatizo huu ni kuikamilisha haki ya Mungu unamaanisha nini? Una maana kwamba kwa
kubatizwa, Yesu alichukua dhambi za wanadamu kuanzia dhambi ya Adamu mpaka Mwanadamu yule wa mwisho.

Mathayo 3:15-16 Inasema “Yesu akajibu akasema, na iwe hivyo, kwa kuwa imetupasa kuitimiza haki yote, ndipo akamruhusu.”Haki ya Mungu inaweza kupatikana katika ubatizo ambao Yesu alipokea ndani ya imani inayoikubali damu ya msalabani kwa hiyo wale ambao mioyo yao imesamehewa dhambi kwa kuamini ubatizo huo na damu yake msalabani ni lazima wapokee ubatizo wa maji kwa imani. Kwa nini? Kwa sababu kwa imani ya ubatizo wake, dhambi zote zimeondoshwa kikamilifu, ndio maana Paulo alieleza ubatizo wa Yesu kwa wale ambao hawakupokea Roho Mtakatifu.
Watu wengi wamekuwa wakijaribu kumpokea Roho Mtakatifu kwa njia wanazozifahamu wao kama kurudia rudia maneno na nyinginezo, lakini hizo si njia sahihi katika wokovu.
Yatupasa kuwa na uelewa sahihi katika neno la ubatizo, ukisoma (Matendo 18:24-26, na Matendo 19: 1-4) utaona ya kwamba Apolo alipita Efeso akahubiri ubatizo, na uelewa wake ulikuwa katika ubatizo wa Yohana tu. Na Paulo alipita eneo hilo hilo la Efeso baada ya Apolo kuondoka na kuwafundisha ubatizo kwa usahihi zaidi ambapo walipokea Roho Mtakatifu. Hivyo katika ubatizo tunapokea Roho Mtakatifu.
Damu ya Yesu msalabani ni matokeo ya ubatizo na si kumwaga damu msalabani ndiko kuliko mwezesha Yesu kubeba dhambi zetu. Alibeba dhambi zetu pale alipo batizwa na ndipo alipokwenda msalabani akiwa tayari amekwisha beba dhambi hizo zote za ulimwengu hatimaye kufa ili kuleta upatanisho wa dhambi za ulimwengu.
Hivyo msalaba ni matokeo ya ubatizo aliopokea Yesu, kwa kuwa Yesu alikwisha beba dhambi zetu kwa njia ya ubatizo wake, kumwaga damu msalabani ndiko hitimisho la kuelekea upatanisho wa dhambi zetu zote.

Unapomtwika Yesu dhambi zako katika ubatizo unakuwa umesamehewa makosa yako yote, ndipo Roho Mtakatifu anapata nafasi ya kukaa ndani yako. Tunaweza kuzaliwa upya kiroho kwa kuamini ubatizo na damu ya Yesu.

Maoni 1 :

  1. Slotyro Hotel and Casino - Mapyro
    Find your way around 하남 출장샵 the casino, find where everything is located with slotyro's 상주 출장안마 mobile casino app. 대전광역 출장안마 Find 천안 출장샵 the slotyro slotyro 울산광역 출장마사지 mobile app.

    JibuFuta