Na mtu awaye yote katika watu wa
nchi akifanya dhambi pasipo kukusudia, kwa kufanya neno lolote katika hayo
ambayo BWANA alizuiria yasifanywe, naye akapata hatia, akijulishwa hiyo dhambi
yake kwa ajiri ya dhambi yake aliyoifanya, ndipo atakapoleta mbuzi mke
mkamilifu, awe matoleo yake kwajiri ya dhambi yake aliyoifanya. Naye ataweka
mkono wake kichwani mwake hiyo sadaka ya dhambi, na kumchinja sadaka ya dhambi
mahali hapo pa sadaka ya kuteketezwa. Kasha kuhani atatwaa katika hiyo damu
yake kwa kidole chake, na kuitia katika pembe za madhabahu ya kuteketeza na
damu yake yote ataimwaga chini ya
madhabahu (Walawi 4:27-30)
Mwenye dhambi anapotaka kupatanishwa na dhambi alizotenda
kwa kila siku ilimpasa kuleta mnyama asiye na doa mbele ya hema takatifu. Ndipo
ilimpasa kumwekea mikono juu ya sadaka hiyo ya mnyama ili kumtwika dhambi zake zote, kumchinja koo
na kutoa damu kwa kuhani ili iweze kuletwa mbele ya Mungu. Kitakachofuata ni
kumalizia hatua iliyobaki ili ikamilishe msamaha wa wenye dhambi.
Pasipo sheria na amri za Mungu, watu wasingeweza kujua ikiwa
kwamba wana dhambi au la. Tunapojichunguza wenyewe kupitia sheria na amri za
Mungu tunagundua kwamba tuna dhambi. Dhambi zetu hazikuhukumiwa kwa viwango
vyetu, bali ni kwa sheria na amri za Mungu.
Katika Agano la kale, dhambi zilitwikwa juu ya kichwa cha
sadaka ya dhambi kwa kuwekewa mikono. Na baadaye mwenye dhambi hakuwa tena na
dhambi ndipo sadaka hiyo ilipopaswa kuchinjwa na kufa badala ya mwenye dhambi.
Mpangilio huo wa utoaji wa sadaka ya dhambi ni kivuli cha hukumu na upendo wa
Mungu.
“Kisha atayaondoa
mafuta yake yote kama vile mafuta yanayoondolewa katika hizo za amani; kisha
kuhani atayateketeza juu ya madhabahu iwe harufu ya kupendeza kwa bwana” (Walawi 4: 31) mafuta katika biblia yana
maana ya Roho Mtakatifu. Hivyo, ili tuweze kupatanishwa kwa dhambi zetu zote
yatupasa pia kuchukulia ndani ya moyo wetu upatanisho wa dhambi zetu kwa namna
ya Mungu aliyo iweka.
Mungu aliwaeleza wana wa Israel kwamba sadaka ya dhambi
katika Agano la kale ilipaswa iwe ni mwana kondoo, au mbuzi au ndama dume.
Sadaka hiyo ilichaguliwa kwa uwangalifu mkubwa. Sababu ya sadaka kuwa safi ni
kwamba ilipaswa kuonyesha Yesu Kristo ambaye angezaliwa kwa uwezo wa Roho
mtakatifu na kuwa sadaka ya dhambi kwa wanadamu wote.
Watu wa Agano la kale walizitwika dhambi zao kwa kuweka
mikono juu ya mnyama asiye na doa, kuhani alihudumia kwa sadaka hiyo ili
kulipizia dhambi. Hii ndiyo namna ambayo Israel walipatanishwa kwa dhambi.
kifungu kingine kinacho zungumzia mambo hayo ni (Walawi16:21). Hivyo
tafakari kwa kina na utaona kwamba bila kuwekea mikono juu ya sadaka husika,
damu haitakua na maana yoyote katika kuondoa dhambi. Iliwapasa Israel kuamini
katika mambo yote ya sadaka ya dhambi.
SABABU GANI YESU ALIBATIZWA YORDANI?
Hebu sasa natuangalie tukio lile Wakati kuhani mkuu wa
mbingu alipokutana na kuhani mkuu wa mwisho wa wanadamu. Hapa tunaweza kuona
haki ya Mungu kupitia ubatizo ulio leta upatanisho wa dhambi zote za ulimwengu.
Yohana Mbatizaji aliye mbatiza yesu alikuwa mkuu kati ya
wote waliozaliwa na mwanamke. Yesu alimshuhudia Yohana Mbatizaji katika (Mathayo
11:11) “amini nawaambieni, hajaondokea mtu katika
uwazao wa mwanamke aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji”. Namna ile dhambi
za watu zilivyoweza kufutwa wakati kuhani mkuu Haruni alipoweka mikono juu ya
kichwa cha sadaka ya dhambi katika siku ile ya upatanisho, ndivyo hivyo katika Agano
jipya dhambi zote za ulimwengu zilivyoweza kufutwa pia pale Yesu alipobatizwa
na Yohana Mbatizaji.
Injiri ya kuzaliwa upya mara ya pili ni injiri
iliyokamilisha ondoleo la dhambi zetu zote za zamani, za sasa na zijazo
mbeleni. Hivyo injiri ya ukombozi kupitia ubatizo wa Yesu ilikuwa ni injiri ya Mungu
iliyopangiliwa ili kutimiza haki yote, ambayo iliokoa wote duniani. Yesu alibatizwa
kwa jinsi iliyostahili ili kupatanisha dhambi za ulimwengu.
Nini maana ya’ haki yote’? (Yohana 3: 13-15) Maana yake ni Mungu kusafisha
dhambi zote za ulimwengu kwa njia inayostahili. Yesu alibatizwa ili kutakasa
dhambi zote za wanadamu “ kwa maana haki ya Mungu anadhihirishwa
ndani yake toka imani hadi imani”(Warumi 1:17).
Haki ya Mungu imedhihirishwa katika uwamuzi wa kumtuma mwana wake Yesu hapa
duniani ili kutakasa dhambi za ulimwengu kupitia ubatizo wake kwa Yohana Mbatizaji
na kwa kifo chake msalabani.
Katika Agano jipya, haki ya Mungu imeelezwa kupitia ubatizo
wa Yesu na damu yake. Tunakuwa wenye haki kwasababu Yesu Alibeba dhambi zetu
zote katika mto Yordani. Tunapoukubali wokovu huu wa Mungu ndani ya mioyo yetu
haki ya Mungu inatimizwa kwa uhakika.
Kila kitu katika Agano la kale kina mwenzake katika Agano
jipya kwa Agano la kale “tafuteni katika kitabu cha
BWANA mkasome hapana katika hao wote atakayekosa kuwapo, hapona mmoja
atakayemkosa mwenzake; kwa maana kinywa change kimeamuru na roho yake
imekusanya” (Isaya 34:16)
Kutimia kwa unabii wa wokovu katika Agano la kale
kulihitimishwa kwa njia ya ubatizo wa Yesu katika Agano jipya. Hivyo unabii wa Agano
la kale hatimaye ulipata mwenzake katika Agano jipya. Vile watu wa Israel walivyopatanishwa
kwa dhambi zao mara moja kwa mwaka katika Agano la kale, ndivyo ilivyo sasa
dhambi za watu wote ulimwenguni zilivyo twikwa Yesu na kufutiliwa mbali milele
katika Agano jipya.
Ikiwa hukubali na kuamini hili moyoni mwako juu ya huu
ukweli wa ubatizo wa Yesu na kifo chake pale msalabani kamwe hautoweza kutakaswa
dhambi zako hata kama wewe unaishi maisha ya utakatifu kwa kiwango kikubwa. Yesu
alikufa msalabani kwasababu alibeba dhambi zako zote kwa ubatizo wake.
(Warumi 8:3-4) maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa
dhaifu kwasababu ya mwili, Mungu kwa kumtuma mwanawe mwenyewe katika mfano wa
mwili ulio na dhambi aliihukumu dhambi katika mwili, ili maagizo ya tirati
yatimizwe ndani yetu sisi tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili bali mambo ya
roho.
Kwakuwa sisi ni wanadamu tusioweza kamwe kufuata sheria na
amri za Mungu kutokana na udhaifu wa miili yetu, Yesu alibeba dhambi zetu zote
juu yake. Huu ni ukweli wa ubatizo wake. Ubatizo wa yesu ulitabili kifo chake
pale msalabani. Hii ni hekima Halisi ya injiri ya Mungu.
Ikiwa umekuwa ukiamini kifo cha Yesu pekee, sasa nakusihi
ugeuke na ukubali kwa moyo wako wote injiri ya wokovu kupitia ubatizo wa Yesu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni