Lipi lilitangulia,
tohara au sheria?
Lipi kati ya
moja ya haya Mungu aliwapa Waisraeli kwanza? Tohara. Baada ya ahadi ya ufalme
wa Mungu, Mungu alimwambia Abraham na kila mume kati ya wanaume wa nyumba zake
kutahiriwa. Mungu alisema kwamba tohara hiyo ni alama ya Agano la Mungu na wao.
Hivyo Abraham alitahiriwa govi lake. Wanaume wote katika nyumba yake walifuata
tendo hili. Tohara inafanana na imani ambayo tunaiamini.
Tunaokolewa pale
tunapoamini kwa moyo. Mungu anasema “tohara ni ya
moyo katika roho si katika andiko ambayo sifa yake haitoki kwa wanadamu bali
kwa Mungu” (Warumi 2:29). Yatupasa kuwa na ondoleo la dhambi. Ikiwa hatutakuwa
nalo mioyoni mwetu basi ni bure tu. Mwanadamu ana “utu wa ndani” na “utu wa nje”
na kila mtu inamlazimu kupokea ondoleo la dhambi ndani ya utu wake.
Wayahudi
walikuwa wakitahiliwa sehemu ya mwili (utu wa nje), lakini Paulo aliwaambia “tohara ni ya moyo”. Leo hii Mungu anatuambia
nasi kwamba tohara ni ya moyo pale tunapokuwa watoto wake.
Paulo hakuwa
akizungumzia tohara ya nje bali tohara na ondoleo la dhambi katika moyo. Hivyo basi
aliposema “nini basi ikiwa baadhi yao hawakuamini?”(Warumi 3:3). Alimaanisha
kwamba ni nini ikiwa basi baadhi hawatoamini moyoni? Hakuwa akizungumzia juu ya
kuamini kwa nje, bali alisema “amini ndani ya moyo.” Yatupasa kujua kile Paulo mtume
alichokuwa akimaanisha na ni nini maana ya ondoleo la dhambi moyoni mwetu
kupitia neno la Mungu.
“Ni nini basi ikiwa baadhi yao
hawakuamini?” maana
yake ni kwa vipi basi ikiwa Wayahudi hawakuamini juu ya Yesu Kristo kama
mwokozi, je, kutokuamini kwao kutafanya uaminifu wa Mungu kutokuwa na maana? Je,
ukweli wa Mungu kufuta dhambi zote pamoja na dhambi za kizazi cha Abraham utakuwa
ni bure? Kamwe Paulo anasema kwamba hata Wayahudi ambao ni uzao wa Abraham kwa
mwili wataweza kuokolewa pale watakapo amini kwamba Yesu Kristo ni mwokozi,
mwana wa Mungu aliye beba dhambi zote za dunia kwa njia ya ubatizo na
kusulubiwa. Pia anasema kwamba wokovu na neema ya Mungu kupitia Yesu Kristo hautoweza kamwe kubatilika. (Warumi 3:3-4)
Mungu huchunguza
na kuangalia moyoni.Kwa uwazi utu wetu wa ndani umewekwa mbali na hauna
uhusiano kabisa na matendo yetu. Wokovu wenyewe hauna uhusiano na matendo yetu (soma
katika blog hii “sheria alizotupatia Mungu” utaona kuwa kuna Sheria ya Roho wa uzima na sheria ya dhambi na mauti).
Rejea katika kitabu cha (Warumi 4:1-5) Basi tusemeje juu ya Ibrahim baba yetu kwa jinsi ya
mwili? Kwa maana ikiwa Ibrahim alihesabiwa haki kwa ajili ya matendo yake,
analo la kujisifia, lakini si mbela za Mungu maana maandiko yasemaje? Ibrahim alimwamini
Mungu ikahesabiwa kwake kuwa ni haki. Lakini
kwa mtu afanyaye kazi, ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa ni deni.
Lakini kwa mtu asiye fanya kazi, bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki
asiye kuwa mtauwa imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni