Moja, wale
wanaopenda kupokea Roho mtakatifu ni lazima waamini Injili ya maji na Roho na
kupokea ondoleo la dhambi.
Pili, wanahitaji
kuwa na imani thabiti juu ya ukweli kuwa, Mungu anatoa Roho mtakatifu kwa wale
tu waliopokea ondoleo la dhambi, hata sasa kuanzia enzi za mitume (matendo 2:38).
Tatu, mioyo yao
lazima igeuke mbali na dhambi ya kutoamini neno la Biblia na kutokuwa na imani.
Nne, kupokea Roho
mtakatifu, Roho zao zinahitaji kufundishwa neno kikamilifu. Wanapaswa kusikiliza
kwa uangalifu neno lililobarikiwa la kuzaliwa upya kwa maji na Roho, na
wakihitaji zaidi, watapaswa kushirikiana katika vikundi vya Injili pamoja na
watumishi wa Mungu na kupokea Roho mtakatifu. Roho mtakatifu atawafanya
waliamini Neno la Mungu mioyoni mwao, kuzaliwa upya na kumpokea. Lakini kama
wakijaribu kumpokea Roho mtakatifu bila ridhaa yao, ila bila ridhaa kwa kutoa
sala za toba na kujaribu kuishi maisha ya utakatifu,
au pia wakimwigiza Roho mtakatifu wakijaribu kumpokea kwa
kujinyima, kufunga, au sala za milimani, hapo wataishi kuanguka katika
kuchanganyikiwa.
Tunapaswa kukumbuka kwamba Roho wa Mungu haji kwa sababu
watu wanataka kumpokea wenyewe, bali huja kwa wale walio tayari kumpokea. Roho
mtakatifu haji kwa wale wanaashinda milimani wakiomba, kushiriki mikutano ya
karismatiki au wanaotaka vipawa tu, kama unafikiria ulipokea kitu fulani kama
karama ya Roho mtakatifu katika mikutano hiyo, au kwa imani yako, basi hapo kuna
jambo unapaswa kulitafakari kwanza. Na hii ni kama kuna dhambi au hakuna moyoni
mwako. Unapaswa kutambua kuwa ulichokipokea si kutoka kwa Roho mtakatifu bali
shetani, na ni lazima ukiondoe. Ni lazima tutambue ni wapi na kwa nini Roho
mtakatifu anatenda kazi. Kuna jambo ambalo hatupaswi kulisahau katika kutafuta
kupokea Roho mtakatifu. Hii ni kuamini ubatizo wa Yesu (mathayo
3:15) na damu yake msalabani. Roho mtakatifu anajitegemea, ila huja kwa
wale wanaoamini ubatizo wa Yesu kristo na damu yake msalabani na ondoleo la
dhambi zao. Roho mtakatifu huja na kutenda kazi ndani ya maisha ya wale
wanaoiamini Injili ya maji na Roho kama wokovu wao wa kweli.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni