Jumatatu, 30 Juni 2014

YOHANA MBATIZAJI HAKUSHINDWA


(Mathayo 11:1-14)
“Ikawa Yesu alipokwisha kuwaagiza wanafunzi wake kumi na wawili, alitoka huko kwenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao. Naye Yohana aliposikia huko gerezani matendo yake Kristo, alituma wanafunzi wake, kumwuliza, ‘Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine?’ Yesu akajibu akawaambia, ‘Nendeni mkamweleze Yohana mnayoyasikia na kuyaona; vipofu wanapata kuona, viwete wanakwenda, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa habari njema. Naye heri awaye yote asiyechukizwa nami.’ Na hao walipokwenda zao, Yesu alianza kuwaambia makutano habari za Yohana, ‘Mlitoka kwenda nyikani kutazama nini? Unyasi ukitikiswa na upepo? Lakini mlitoka kwenda kuona nini? Mtu aliyevikwa mavazi mororo? Tazama, watu wavaao mavazi mororo wamo katika nyumba za wafalme. Lakini kwa nini mlitoka? Ni kuona nabii? Naam, nawaambia, na aliye mkuu zaidi ya nabii. Huyo ndiye aliyeandikiwa haya,
‘Tazama, mimi namtuma mjumbe wangu Mbele ya uso wako, Atakayeitengeneza njiayako mbele yako.’ Amin, nawaambieni, hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji; walakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye. Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka. Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana. Na ikiwa mnataka kukubali, yeye ndiye Eliya atakayekuja.”
Tunapaswa Kuifahamu Huduma ya Yohana Mbatizaji
Ni huduma gani hasa ambayo Yohana Mbatizaji aliitimiza kabla ya Yesu? Wakristo wengi leo hii hawamfahamu vizuri Yohana Mbatizaji, hivyo wanatakiwa kupata mtazamo mpya kuhusu Yohana Mbatizaji ili waweze kumfahamu na kuikubali huduma yake kikamilifu. Sisi sote tunapaswa kuwa na ufahamu sahihi na kuukubali uhusiano kati ya huduma ya Yesu na ile yaYohana Mbatizaji. Kwa kuufahamu uhusiano huu kikamilifu, basi unapaswa kwanza kulipokea ondoleo la dhambi kwa imani.
Katika kifungu cha leo cha Maandiko, Yesu aliwaambia wanafunzi wa Yohana Mbatizaji, “Nendeni mkamweleze Yohana mnayoyasikia na kuyaona; vipofu wanapata kuona, viwete wanakwenda, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa habari njema.
Kwa kweli vipofu waliokutana na Yesu walifunguliwa macho yao, viwete waliweza kusimama na kutembea, waliokuwa wamepagawa na mapepo waliwekwa huru, na injili ilihubiriwa kwa maskini wa roho.
Tunachopaswa kukitambua hapa ni kwamba huduma ya Yesu ilihusisha kazi ya kuwafungua macho vipofu. Kwa maneno mengine, katika wakati huu, Bwana ametupatia injili ya maji na Roho, ambayo ni injili ya kweli inayowafungua macho wenye dhambi ambao bado wanatembea katika giza. Kabla ya kukutana na Yesu Kristo, kila mtu alikuwa na dhambi katika moyo wake na alikuwa ni kipofu wa kiroho mbele ya Mungu. Sisi pia, tulikuwa hatuufahamu uhalisia wa injili ya maji na Roho, wala hatukutambua kuwa Yesu ni nani, pia sisi sote tulikuwa hatuzifahamu dhambi zetu na matokeo mabaya ambayo yangejiri kwa sababu ya dhambi hizo. Pia hatukuwa na upendo kwa Neno la kweli la injili ya maji na Roho, ambalo ni Kweli ya wokovu ambayo Yesu ametupatia.
Hata hivyo, watu wengi sasa wameisikia Neno lenye nguvu la injili ya maji na Roho, na kwa kule kuiweka imani yao katika Neno la injili, basi macho yao ya kiroho yamefunguliwa na wameuvumbua Ukweli unaowawezesha kuokolewa toka katika dhambi zao zote. Wale wanaoifahamu na kuiamini injili hii ya kweli sasa wameuvumbua Ukweli wa ondoleo la dhambi ambao walikuwa hawaufahamu hapo kwanza: Macho yao ya kiimani yamefunguliwa, na sasa wanaifanya kazi ya Mungu. Kama ilivyo katika macho yetu ya kimwili ambapo tunaona kila kitu katika ulimwengu huu, sasa tunaweza kuona ulimwengu wa kiroho kwa wazi hasa baada ya macho yetu ya kiroho kufunguliwa kwa kupitia imani yetu katika injili ya maji na Roho. Hivi ndivyo mtu anavyoweza kuufikia ufahamu kwamba huduma ya Yesu inahusu hasa huduma ya injili ya maji na Roho.
Kwa sababu ya dhambi zetu, wewe na mimi tulikuwa ni vipofu na viwete wa kiroho, na kwamba hatukuweza kuiona huduma ya Mungu wala kuifanya kazi yake. Kwa maneno mengine, sisi pia tulikuwa ni wenye dhambi ambao tulikuwa tumefungwa ili kwenda kuzimu. Hata hivyo, Yesu Kristo alikja hapa duniani, alibatizwa na Yohana Mbatizaji, akaimwaga damu yake Msalabani, na kwa sababu hiyo akazitimiza kazi ambazo ziliondolea mbali dhambi zote za ulimwengu. Kwa hiyo, yeyote atakayeamini katika Ukweli huu ataona bayana kuwa dhambi zake zote zimeoshelewa mbali kikamilifu. Kwa kweli Yesu Kristo amezisafishilia mbali dhambi zetu zote kwa kuja hapa duniani, kwa kubatizwa na Yohana Mbatizaji, na kwa kuimwaga damu yake Msalabani.
Hata sasa, kazi hizo za Mungu, zinaendelea kujifunua vizuri katika mioyo ya wale wote wanaoamini katika injili ya maji na Roho. Bwana wetu ameyafunua macho ya waamini wake kiroho, na ametufanya sisi tuliokuwa viwete kiroho, kuinuka na kusimama kwa miguu yetu kwa kupitia nguvu ya injili ya maji na Roho.
Hapa tunahitaji kutambua kuwa ikiwa tutajaribu kuifanya kazi ya Mungu pasipo kuwa na imani katika injili ya maji na Roho,  basi ni hakika kuwa hakutakuwa na faida yoyote kwa miili yetu wala kwa roho zetu. Wale ambao bado hawajapokea ondoleo la dhambi zao wanafikiri wakati wote, “Ninapaswa kuishi maisha mema. Ninapaswa kuwa mwema kwa kila mtu.” Lakini hakuna hata mmoja ambaye anaweza kulifanya hili, yaani kutenda mema na kuishi maisha mema.
Kabla hatujaifahamu injili ya maji na Roho, tulikuwa na dhambi katika mioyo yetu na kwa sababu hiyo sisi sote tulikuwa na dhambi katika mioyo yetu na kwa sababu hiyo tulikuwa ni wenye dhambi, na hivyo hatukuweza kuifahamu kazi ya Mungu ya haki ilivyo na wala hatukuweza kuitenda. Hata hivyo, kwa kuwa Bwana wetu alizipokea dhambi zetu zote mara moja na kwa wote kwa kupitia ubatizo wake, na kwa sababu alizisafishilia mbali kwa damu yake aliyoimwaga Msalabani hali akiwa amejitwika dhambi za ulimwengu, basi hapo tuliweza kuokolewa toka katika dhambi zetu zote.
Sasa tunaweza kuishi kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu kwa sababu Yesu Kristo ametuokoa toka katika dhambi kwa nguvu ya injili ya maji na Roho. Sasa tunaweza kumwezesha yeyote yule kuionja radha ya nguvu ya injili  hii ya kweli na kisha kuokolewa.
Yesu Kristo ametuwezesha kuokolewa toka katika dhambi na laana zetu zote kwa kuleta maisha mapya kwako wewe na mimi ambao tulikuwa ni viwete kwa kupitia Ukweli wa wokovu. Alichosema Yesu hapa ni kuwa, “wenye ukoma wanatakaswa na viziwi wanasikia; wafu wanafufuliwa,” kimetimizwa katika mioyo yetu yote inayoamini katika injili ya maji na Roho.
Tulipokuwa tungali wenye dhambi, pia tulikuwa ni wakoma wa kiroho. Wakati huo mioyo yetu ilikuwa na dhambi, na hatukuweza kusafishwa toka katika dhambi zetu zote hadi pale tulipoiweka imani yetu katika injili ya kweli ya maji na Roho.
Pia Bwana wetu alisema kuwa viziwi watasikia. Tulipokuwa wenye dhambi, hatukuweza kulifahamu Neno la Mungu hata pale tuliposikia. Lakini sasa, kwa kuwa tumefunikwa na nguvu ya injili ya maji na Roho kwa kuiweka imani yetu juu yake, tunaweza kulifahamu Neno la Mungu, na kufahamu maana yake ya kweli, na kisha kuliamini hilo Neno kwa mioyo yetu yote.
Kila mtu ulimwenguni pote anaishi katika njaa na kiu ya kiroho. Watu wanateseka kutokana na upofu wa ulemavu wa kiroho. Lakini Bwana bado anawapatia nafasi ya kuponywa mara moja kwa kuturuhusu kuwahubiria injili ya maji na Roho. Ni lazima tuwaonee huruma. Tunahitaji kukumbuka kuwa wakati tulipokuwa hatuifahamu injili hii ya wokovu, ambayo ni injili ya maji na Roho, hatukuwa na ukamilifu, na kwamba hatukuweza kufanya lolote zaidi ya kuishi hali tukiwa na dhambi zetu zote katika mioyo yetu. Hatupaswi kuisahau neema yake yenye huruma ambayo imewageuza wenye dhambi kuwa wenye haki.
Kwa hiyo, kile ambacho Bwana wetu alikizungumza kwa wanafunzi wa Yohana Mbatizaji kuhusu maajabu ambayo alikuwa anayatenda alikuwa na lengo kuwafanya wafahamu kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, Mwokozi wa kweli na Masihi atakayekuja. Baadhi wanaweza kusema kuwa wakati Yohana Mbatizaji alipofungwa, alijaribiwa hadi akawa na mashaka ikiwa Yesu alikuwa ni Masihi atakayekuja, na kwamba hii ndio sababu aliwatuma wanafunzi wake kwenda kwa Yesu. Lakini hii si kweli.
Yohana Mbatizaji alikuwa ni nani? Alikuwa ni mkuu kati ya wote waliozaliwa na wanawake. Alikuwa ni mkuu kuliko mtumishi mwingine yeyote wa Mungu. Kwa maneno mengine, sio kwamba Yohana alikuwa hamwamini Yesu kiasi kuwa akatuma wanafunzi wake kwenda kumuuliza, “Wewe ndiye yule ajaye?” Bali alichokuwa anakifanya ni kuwaelimisha wanafunzi wake ili waweze kufahamu hasa kuwa Yesu ni nani.
Yohana Mbatizaji alikwishaamini na kufahamu kuwa Yesu ni Mwokozi na Mwana wa Mungu; zaidi ya yote, alikuwa amekwishasikia ushuhuda wa Mungu Baba wakati alipombatiza Yesu Kristo katika Mto Yordani (Mathayo 3:17), na pia yeye mwenyewe alikuwa ni shahidi aliyekuwa akimshuhudia Yesu. Yohana Mbatizaji aliwatuma wanafunzi wake kwa Yesu kwa kuwa wanafunzi wake walikuwa hawamfahamu Yesu kikamilifu, na alitaka kuwafundisha kuwa Yesu Kristo ndiye Mwokozi atakayekuja.
 Kwa kweli baada ya Yohana Mbatizaji kufahamu kuwa Yesu Kristo alikuwa ni Masihi atakayekuja, alijaribu kuiondoa huduma yake na kuwapeleka wanafunzi wake kwa Bwana. Ili kumfunua Yesu kwa taifa  la Isareli, Yoahan Mbatizaji alisema kuwa, “Yeye[Yesu] hana budi kuzidi, bali mimi kupungua” (Yohana 3:30).Kwa mfano, Andrea, ndugu wa Simoni Petro, alikuwa ni mwanafunzi wa Yohana, lakini alimfuta Bwana mara baada ya kumsikia Yohana akimshuhudia Yesu (Yohana 1:40).
Hata hivyo, ubishi unaotolewa juu ya Yohana Mbatizaji unaeleza mambo mengi yasiyo na maana hata pale ambapo hawamfahamu Yohana Mbatizaji vizuri, huku wakidai, “Yohana Mbatizaji alikuwa ameshindwa. Aliangukia  katika majaribu na akashindwa kumwamini Yesu. Imani yake ilivurugika baada ya kufungwa.” Lakini ndugu zangu waamini, hampaswi kuiwekea mashaka imani ya Yohana Mbatizaji.
Yohana Mbatizaji na Yesu walikuwa na majukumu yao ambayo walipaswa kuyatimiza pamoja kwa majaliwa ya Mungu Baba. Na majukumu haya yalikuwa ni kubatiza na kubatizwa, huduma ambazo zilikuwa na lengo la kuitimiza haki ya Mungu. Hii ndio sababu Yesu na Yohana Mbatizaji kila mmoja aliishuhudia huduma ya mwenzake.
Mathayo 11:7-9 inasema,  “Na hao walipokwenda zao, Yesu alianza kuwaambia makutano habari za Yohana, Mlitoka kwenda nyikani kutazama nini? Unyasi ukitikiswa na upepo? Lakini mlitoka kwenda kuona nini? Mtu aliyevikwa mavazi mororo? Tazama, watu wavaao mavazi mororo wamo katika nyumba za wafalme. Lakini kwa nini mlitoka? Ni kuona nabii? Naam, nawaambia, na aliye mkuu zaidi ya nabii.”Hapa Yesu alisema, “Kwa nini mlikwenda nyikani? Kumwona nabii? Ikiwa ni hivyo, mpo sahihi. Ninawaambia kuwa Yohana Mbatizaji ni mba mkuu zaidi ya nabii.” Kisha Yesu alimwelezea
Yohana Mbatizaji kwa kunukuu Malaki 3:1 katika Maandiko. Mathayo 11:10 ni kifungu kinachonukuu Malaki 3:1. Katika kifungu hiki, Yesu alisema, “Huyo ndiye aliyeandikiwa haya, Tazama, mimi natuma mjumbe wangu mbele ya uso wako, atakayeingeneza njia yako mbele yako.”Kwa maneno mengine, kwa kunukuu kifungu kilichoandikwa katika Malaki 3:1, Yesu alishuhudia kuwa Yohana  Mbatizaji alikuwa ni mtumishi halisi wa Mungu ambaye ndiye aliyetumwa kumtangulia Yesu Mwenyewe. Mtumishi wa Mungu aliyeandikwa katika Malaki 3:1 ni nani? Si mwingine bali ni Yohana Mbatizaji. Malaki 4:5-6 pia inaonyesha kuwa mtumishi anayetajwa katika Malaki 3:1—“Namtuma mjumbe wangu”—ina maanisha ni Yohana Mbatizaji. Katika Mathayo 11:11, Yesu alisema, “Amin, nawaambieni, hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji; walakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye.”
Kwa nini Bwana alituambia hili? Kwa nini alisema kuwa Yohana Mbatizaji alikuwa ni mkuu kuliko wote waliozaliwa na wanawake? Hapa Yesu anatueleza kuwa Yohana  Mbatizaji alikuwa ni mtumishi halisi wa Mungu aliyekuwa ametabiriwa katika Agano la Kale, na kwamba yeye ni mwakilishi wa wanadamu. Kifungu hiki kinaendelea kwa kueleza sentensi ngumu: “Walakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye.” Waalimu wengi wa uongo wanamhukumu Yohana Mbatizaji kuwa mtu aliyeshindwa kwa kuangalia kifungu hiki. Wanadai “Kwa sababu Yohana alikuwa na mashaka kuhusu Yesu’ kuwa ni Masihi, na kwa sababu hiyo alitathminiwa na Bwana kuwa ni mtu wa mwisho.” Madai haya ni upuuzi mtupu. Ila, kile anachokisema hapa Yesu ni kwamba ingawa Yohana Mbatizaji alikuwa ni mwakilishi wa wanadamu, kwa upande wa kiroho, alikuwa ni mtu wa chini ambaye hakuweza kufananishwa na wale waliokuwa wamefanyika watoto wa Mungu. Kwa maneno mengine, pamoja na kuwa Yohana Mbatizaji alikuwa ni mwakilishi wa wanadamu wote katika mwili, basi yeye hakuweza kufananishwa na walele waliozaliwa tena upya.
Kwa kweli Yohana alikuwa ni mkuu katika mtazamo wa kibinadamu. Yeye alilelewa kama Mnadhiri, na aliishi maisha ya kitawa akiwa nyikani akila nzige na asali ya mwitu. Kutokana na mtazamo wa haki wa kibinadamu, ni kweli kuwa Yohana alikuwa ni mkuu. Lakini hii haki ya kibinadamu haina maana yoyote hasa pale inapolinganishwa na haki ya Mungu ambayo inaweza kutolewa kwa yeyote anayeweza kuingia Ufalme wa Mungu kwa imani. Kwa sababu ya wale waliofanyika kuwa watu wa Ufalme wa Mbinguni kwa kuamini katika injili ya maji na Roho wameipokea haki ya Mungu, basi hao ni wakuu kuliko mtu yeyote anayeitegemea haki yake binafsi. Mtu anaweza kuwa mwakilishi wa wanadamu katika ulimwengu huu katika mwili, lakini yeye ni mdogo kuliko wale waliofanyika watu wa Mungu kwa kuamini katika injili ya maji na Roho.
Hivyo basi, wakati Yesu aliposema, “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni wapatikana kwa nguvu, na wenye nguvu wauteka,”alisema hiyo kwa sababu Yohana Mbatizaji alikuwa amembatiza mara moja na hivyo kuzipitisha dhambi za ulimwengu kwenda kwa Yesu. Kwa hiyo, Yohanan Mbatizaji alikuwa ni Kuhani Mkuu wa wisho na nabii wa mwisho wa Agano la kale, na huduma yake iliisha pale alipombatiza Yesu na akamshuhudia. Kwa maneno mengine, Yesu anatueleza kuwa kila kitu cha Agano la Kale kiliisha kwa kuonekana kwake na kwa kuonekana kwa Yohana Mbatizaji, na kwa huduma ya Yohana Mbatizaji ya kumbatiza Yesu. Kwa lugha nyingine, tangu wakati ambapo Yohana Mbatizaji na Yesu walikuja hapa ulimwenguni, hapo ndipo haki yote ya Mungu ilitimizwa. Kipindi cha Agano Jipya kilifunguliwa wakati Yesu alipokuja hapa duniani na kubatizwa na Yohana Mbatizaji.
 Kipindi hiki cha Agano Jipya ni kipindi cha nguvu ya injili, ni wakati ambapo yeyote anayeamini katika injili ya maji na Roho anaweza kupokea ondoleo la dhambi na kufanyika mwana wa Mungu. Kadri Agano la Kale lilivyodumu hadi siku za Yohana Mbatizaji, wakati Yesu alipokuja hapa duniani, wakati alipozichukua dhambi za mwanadamu kwa ubatizo wake, akaimwaga damu yake, na kuzitoweshea mbali dhambi zetu zote, basi tangu hapo malango ya Mbinguni yamefunguliwa kwa wote wanaoamini katika Ukweli huu.
Wakati Yesu alipozichukua dhambi zote za kila mmoja katika ulimwengu huu kwa kubatizwa, basi hapo ndipo kipindi cha Agano Jipya kilipoanza. Neno lote la unabii la Agano la Kale lilitimizwa kwa kupitia Yohana Mbatizaji na kwa kupitia Yesu Kristo.
Yesu Kristo alizipokea dhambi zote za wanadamu mara moja na kwa wote kwa kubatizwa na Yohana Mbatizaji, kisha akaimwaga damu yake Msalabani, na kwa sababu hiyo amezitoweshea mbali dhambi zote za ulimwengu. Hii ndio sababu Bwana wetu alisema tangu siku za YohanaMbatizaji hata sasa Ufalme wa Mbinguni wapatikana kwa nguvu.
Yeyote anayeamini katika Ukweli huu anaweza kuingia Mbinguni kwa imani kwa kuwa Yesu alizipokea dhambi za ulimwengu kwa kuupokea ubatizo toka kwa Yohana Mbatizaji. Kwa lugha tofauti, Yesu aliweza kuzichukua dhambi zote za wanadamu mara moja na kwa wote kwa kuwa Yohana Mbatizaji alikuwa amezipitisha dhambi zote za mwanadamu kwenda kwa Yesu. Yohana Mbatizaji aliweza kulitimiza jukumu la kuzipitisha dhambi za ulimwengu kwenda kwa Yesu akiwa kama Kuhani Mkuu wa mwisho wa Agano laKale na hii ni kwa sababu Yohana Mbatizaji alikuwa amezaliwa toka katika ukoo wa Haruni Kuhani Mkuu.
Kule kusema kila mtu anayeamini katika Ukweli huu anaweza kuingia Mbinguni kwa imani ni kutokana na ukweli kuwa Yohana Mbatizaji alikuwa amezipitisha dhambi zote za ulimwengu kwenda kwa Yesu kwa kumbatiza, na pia ni kwa sababu Yesu alizichukua dhambi za ulimwengu na ndio maana kipindi cha wokovu kwa mwanadamu kimetufikia. Kwa tukio hili la kihistoria, kipindi cha Agano la Kale kiliisha, na kipindi cha Agano Jipya kilianza.
Yesu aliitimiza huduma yake kama Mwokozi wetu mkamilifu kwa kuzichukua dhambi zetu zote za mwanadamu kwa ubatizo wake, na kwa kuimwaga damu yake, na kwa kufufuka tena toka kwa wafu. Hivyo basi, wakati mpya umefika kwa wale wote wanaoamini katika ubatizo ambao Yohana Mbatizaji aliutoa kwa Yesu, ambapo Ufalme wa Mbinguni unapatikana kwa nguvu.
Ukweli ni kuwa Ufalme wa Mbinguni hauwezi kuchukuliwa kwa nguvu ya kimwili. Sasa, maana ya kiroho ya kifungu hiki ni ipi? Maana yake ni hii: Yesu anatueleza juu ya fumbo la Mbinguni, kwamba mtu yeyote anaweza kuingia Mbinguni kwa kuamini katika injili hii kwa sababu Yesu alizipokea dhambi zote za ulimwengu wakati Yohana Mbatizaji alipombatiza Yeye, na kwa sababu ya kusulubiwa na kuimwaga damu yake na kufufuka tena toka kwa wafu.

Bwana wetu alisema, “Manabii wote na torati walitabiri hadi wakati wa Yohana.”Kwa maneno mengine, unabii wa Agano la Kale ulidumu hadi wakati wa Yohana Mbatizaji. Na kwa kweli ni sahihi kusema kipindi cha Agano la Kale kilidumu hadi kuzaliwa kwa Yesu. Lakini unabii wa Agano la Kale ulitimizwa kiroho wakati Yohana Mbatizaji alipombatiza Yesu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni