Jumatano, 30 Aprili 2014

SHERIA ALIZOTUPATIA MUNGU


Mungu aliweka sheria ulimwenguni kwa sababu zifuatazo;
1. aliwapa wenye dhambi sheria na amri ili waokolewe kwa dhambi zao “ kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria” (Warumi 3:20)
2. Sheria ya pili ni sheria ya imani iokoayo wenye dhambi. “Sheria ya Roho wa uzima” ( Warumi 8:2) inayotoa njia ya wokovu kupitia imani katika Yesu Kristo mwokozi wetu (Warumi 5:1-2).Yesu alishuka ulimwenguni kutimiza hii sheria. Yesu aliweka Sheria ya wokovu ili kuokoa wale wote wenye dhambi ulimwenguni.
Kwa asili kulikuwa na sheria mbili zilizotolewa na Mungu: sheria ya dhambi na mauti na ile sheria ya roho wa uzima. Sheria ya Roho wa uzima ilimwokoa Paulo toka katika sheria ya dhambi na mauti. Hii ilimaanisha kuwa kwa kuamini katika ubatizo wa Yesu na kifo chake msalabani, ambavyo vilichukulia mbali dhambi zake zote, Paulo auliungana na Yesu na kisha akaokolewa toka katika dhambi zake zote. Sisi sote ni lazima tuwe na imani inayotuunganisha na ubatizo wa bwana na kifo chake msalabani. Soma fungu hili; Katika yeye mmetahiriwa kwa tohara isiyofanyika kwa mikono, kwa kuuvua mwili wa nyama, kwa tohara ya Kristo. Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu.( wakolosai:2:11-12)
Mungu aliweka sheria ya imani kwa wale tu wenye kuamini wokovu utokanao kwa maji na roho.  Yeye atakaeokolewa na kuwa mwana wa Mungu yampasa kwanza kuamini sheria hii ya imani ambayo Mungu ameitoa. Ndiyo pekee njia ya kuokoka. Kwa haya, ameruhusu njia ya kwenda Mbinguni kwa wale wenye kuamini kuzaliwa kiroho katika kweli tokana na sheria hii.
Vipo vipengele 613 vya sheria ya Mungu vinavyohusu maisha yetu ya kila siku. Lakini iliyo kuu kati ya hii ni amri kumi ambazo yatupasa kuzifuata mbele ya Mungu. Kupitia amri zilizo andikwa na Mungu tutaweza kutambua ni kwa kiasi gani tumeacha utii kwake. (Warumi 3:19-20).
Sababu ya Mungu kutupatia amri zake ilikuwa ni kutufanya tugundue na kuziona dhambi zetu, kamwe hatutoweza kuzishika amri zote, hivyo yatupasa kunyenyekea kwa kukubali ukweli kwamba sisi ni wenye dhambi na Mungu anajua kwamba kamwe hatutoweza kuishi kwa kufuata sheria yake. Hivyo alishuka ulimwenguni kama mwanadamu, alibatizwa na kuhukumiwa msalabani. Kujaribu kuishi kwa kufuata sheria ya Mungu ni dhambi ya kiburi. Hatupaswi kufanya hivyo.
Ku wapi,basi, kujisifu? Kumefungiwa nje. Kwa sheria ya namna gani? Kwa sheria ya matendo? La ! bali kwa sheria ya imani. Basi, twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria ( Warumi 3:27-28) Pia soma katika (Warumi 4:1-8)

Kuna sehumu imeandikwa imani bila matendo imekufa lakini soma kwa umakini utaona ya kuwa si matendo ya sheria bali matendo ya imani ndiyo yanayo hitajika. Je mwenye Roho Mtakatifu anaweza kutenda dhambi makusudi kwa sababu tu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria? Hapana, maana mtu huyu amempokea Roho Mtakatifu na matunda ya Roho.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni