Sehemu ya pili
Roho Mtakatifu
aliwashukia Wafuasi wa Yesu ghafla toka Mbinguni!
“Hata ilipotimia siku ya
Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja”(Matendo
2:1). Wafuasi wa Yesu walikusanyika
wakisubiri kutimia kwa ahadi ya Mungu kumtuma Roho Mtakatifu. Ndipo Roho
Mtakatifu alipokuja juu yao. “Kukaja ghafla kutoka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo
wa nguvu ukienda kwa kasi ukaijaza nyumba yote waliokuwa wameketi. Kukawatokea
ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliwakalia kila mmoja wao. Wote
wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho
alivyowajalia kutamka” (Matendo 2:2-4).
Roho
Mtakatifu alishuka “ghafla kutoka mbinguni” hapo neno “ghafla” maana yake
kulifanyika si kwa kupitia mapenzi ya Mwanadamu. Kwa nyongeza tafsiri ya “toka
Mbinguni” inaweza kuelezwa mahali Roho Mtakatifu alipotoka, na pia kuondoa
mawazo kwamba ujazo wa Roho Mtakatifu ndani ya mtu hutokana na mapenzi yake au
juhudi. Tafsiri “Toka mbinguni” inatuonyesha kwamba, kusema Roho Mtakatifu
anaweza kupatikana kwa kupitia maombi ni hoja za kitapeli. Kwa maneno mengine,
kusema kwamba Roho Mtakatifu alishuka ghafla toka mbinguni maana yake kuwa na
Roho Mtakatifu ndani hakutokei kwa kupitia namna za kidunia kama vile kunena kwa
lugha au kujitoa nafsi. Wafuasi wa Yesu walinena kwa lugha hapo awali katika
kuhubiri Injili njema kwa watu wa mataifa yote.
Sababu
ya hili ni kuwa aliwawezesha kuhubiri Injili kwa lugha za kigeni toka ile ya Kiyahudi
kwa msaada wake. Watu toka Mataifa yote waliweza kusikia wafuasi hao wakinena
kwa lugha zao ingawa wengi wa wafuasi hawa walitokea Galilaya. “Kukawatokea ndimi
za moto uliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu
wakaanza kusema kwa lugha nyingine kama Roho alivyowajalia kutamka…” (Matendo 2:3-4). Hapa
ni lazima kuwa makini zaidi tunapoona tafsiri, Roho Mtakatifu “kuwakalia kila
mmoja wao”. Wafuasi walisubiri kuja kwa Roho Mtakatifu mahali pamoja wakiwa
tayari wamekwisha kuamini Injili ya kuzaliwa upya mara ya pili katika maji na Roho.
Wakristo wengi nyakati hizi huelewa vibaya
sehemu hii ya kifungu, wakiamini ya kwamba ujio wa Roho Mtakatifu hutokea kwa
sauti kama ya upepo uvumao wanapokuwa kwenye maombi. Hata hivyo hili ni jambo
potofu kuhusiana na Roho Mtakatifu litokanalo na upumbavu na kuchanganyikiwa.
Je, Roho Mtakatifu hufanya sauti pindi anaposhuka juu ya watu? Hapana, hakika
hafanyi.
Kile
watu wanachosikia ni sauti ya shetani afanyayo pale anaposhambulia roho za
watu. Hufanya sauti hizi pale anapofanya mazingaombwe, sauti za kunongoneza na
miujiza ya uongo katika juhudi za kuwaingiza watu katika kuchanganyikiwa kwa
kusingizia kuwa ni Roho Mtakatifu. Watu wengi hupokea kwa kudhani mambo haya
yote ni ishara na ushuhuda wa kushuka kwa Roho Mtakatifu. Pia hudhani kwamba
Roho Mtakatifu huja kwa sauti kama ya “Shwuihhh….” Kama ya upepo mkuu. Wanadanganyika
na mapepo. Kuja kwa Roho Mtakatifu kama ilivyoandikwa katika Matendo alikuja
kwa kupitia imani katika Injili njema tu.
Imani ya Petro (1 Petro 3:21) ilikuwa ni sahihi kumwezesha
kupokea Roho Mtakatifu ndani yake.
Kwa
kuweka bayana tukio la kwanza la Pentekoste katika Matendo
2, Mungu anataka kuweka msisitizo wa ukweli kuwa Roho Mtakatifu alishuka
juu yao kwa sababu walikuwa tayari wamekwisha amini Injili ya maji na Roho.
Lakini watu mara nyingi hudhani Pentekoste ni wakati ule Roho Mtakatifu anaposhuka
toka mbinguni kwa ishara zisizo za kawaida na tafrani za makelele. Na ndiyo
maana nyakati hizi katika mikutano ya uamsho inaaminika kwamba mtu aweza
kupokea Roho Mtakatifu kupitia sala za kurudia rudia, kufunga kula au kuwekewa
mikono. Matukio yasiyo ya kawaida kama vile kuwa na mapepo, kuanguka bila
fahamu, kukosa fahamu kwa siku kadhaa au kutetemeka bila kujizuia hizi si kazi
za Roho Mtakatifu.
Roho
Mtakatifu ni nafsi iliyo na utashi kamili na kamwe haidharau utu wa mwanadamu.
Roho Mtakatifu hana tabia ya kumdhalilisha mtu kwa sababu yeye ni nafsi ya
Mungu aliye na utashi akili na hisia. Huja juu ya watu pale tu wanapoamini maneno
ya Injili ya maji na Roho (Matendo 2:38). Petro
alishuhudia kwamba Roho Mtakatifu alikuja juu ya wafuasi kama ilivyo tabiriwa
na Nabii Joeli. Ilikuwa ni kutimizwa kwa ahadi ya Mungu iliyo sema kwamba Roho Mtakatifu
atawashukia wale wote watakao pokea ondoleo la dhambi. Kwa maneno mengine kuwa
na Roho Mtakatifu ndani huja kwa wale wanaoamini ukweli kuwa Yesu alibatizwa na
Yohana na kusulubiwa ili kuwaokoa wanadamu na dhambi zao. Hotuba ya Petro
ukijumuisha na unabii wa Yoeli, hutuonyesha kwamba yatupasa kujua kwanini Yesu
alibatizwa, na kwa nini imetulazimu kuamini hili. Kwa kujua ukweli huu ndipo
kunako pelekea Wakristo kumpokea Roho Mtakatifu.
Je,
unaamini Injili hii njema ambayo Petro anayoshuhudia? (1
Petro 3:21) au bado wewe unaamini upuuzi na mazingaombwe ya imani zisizo
na umuhimu kinyume na Injili njema? Je, unajaribu kumpokea Roho Mtakatifu kwa
kupitia juhudi zako kwa kuweka kando mpangilio wa Mungu? Hata ikiwa mtu
atamwamini Mungu na kufanya maombi ya toba kwa
matumaini
ya kutakaswa dhambi zake hakuna njia nyingine ya kuweza kumpokea Roho Mtakatifu
zaidi ya kuamini injili ya majina Roho. Je, bado unasubiri kumpata Roho
Mtakatifu ndani yako huku ukiwa huna ufahamu wa injili ya maji na Roho? Je,
wajua maana halisi ya ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani ambayo hupelekea
Roho Mtakatifu kuja ndani ya moyo wako? Ni lazima ujue kwamba Roho Mtakatifu
kuweza kuwa ndani yako kunawezakana ikiwa tu unapoamini injili ya maji na Roho.
Ukweli wa Roho Mtakatifu kuwa ndani yako unawezekana kwa wote wale watakaoamini
Injili ya maji na Roho.
Tunamshukuru
Mungu kwa kutupatia Injili yake ya maji na Roho ambayo ndiyo pekee ituwezeshayo
kumpokea Roho Mtakatifu ndani yetu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni