(Metendo
8:14–24 )
“Na Mitume waliokuwako Yesuramu,
waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu wakawaombea wampokee
Roho Makatifu kwa maana bado hawajawashukia
hata mmoja
wao ila wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu. Ndipo wakaweka mikono yao juu
yao, nao wakampokea Roho Mtakatifu. Hata Simoni alipoona ya kuwa watu wanapewa
Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono ya Mitume akataka kuwapa fedha akisema,
nipeni na mimi uwezo huu ili kila mtu nitakaye mwekea mikono yangu apokee Roho
Mtakatifu. Lakini Petro akamwambia fedha na ipotelee mbali pamoja nawe kwa kuwa
umedhania ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali. Huna fungu wala huna
sehemu katika jambo hili, kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele za Mungu. Basi,
tubia uovu wako huu ukamwombe Bwana ili kama yamkini usamehewe fikira hii ya
moyo wako. Kwa maana nakuona u katika uchungu kama nyongo, na tena u katika
kifungo cha uovu. Simon akajibu akasema, niombeeni ninyi kwa Bwana yasinifike
mambo haya mliosema hata moja.”
Husika na somo kuu katika kifungu hiki,
napenda kuleta ujumbe huu iwapo “mtu anaweza kumpokea Roho Mtakatifu ndani yake
kwa kupitia juhudi binafsi”. Mitume katika nyakati
hizo za Kanisa
la kwanza waliweza kupokea nguvu toka kwa Mungu na kutumwa sehemu kadhaa naye.
Yapo matendo ya miujiza kadhaa katika Kitabu cha Matendo, mojawapo likiwa
kushuka kwa Roho Mtakatifu juu ya
waumini pale Mitume walipowawekea mikono. Biblia inasema “Mitume walipowawekea
mikono wale ambao hawakuwa wamempokea
Roho Mtakatifu ingawa walikwisha mwamini
Yesu, walipokea Roho Mtakatifu.”
Sasa basi, ni
kwa namna gani walimpokea Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono? Kwa wakati huo
maneno ya Mungu bado yalikuwa yakiendelea kuandikwa na hivyo basi kazi ilikuwa
bado haijakamilika hivyo Mungu aliwapa Mitume nguvu za pekee kuweza kufanya
kazi zake. Alikuwa pamoja na Mitume na kuweza kuleta miujiza mingi na maajabu
kupitia kwao. Kilikuwa ni kipindi pekee, wakati Mungu alipofanya maajabu na
miujiza ambayo iliweza kuonekana kwa macho ya wanadamu ili kuweza kuwafanya
watu waweze kumwamini Yesu Kristo kuwa kweli ni mwana wa Mungu na ndiye mwokozi.
Palikuwepo na umuhimu kwa Mungu pamoja na
Mitume kwa nguvu
za ajabu kuweza kuonyesha kazi ya Roho Mtakatifu ili kuthibitisha kwamba Yesu
Kristo ndiye Mungu na kwamba ndiye Mwana wa Mungu Mwokozi. Ikiwa Roho Mtakatifu
asingefanya kazi kupitia miujiza na maajabu kwa nyakati hizo za kanisa la
kwanza hakika pasingekuwepo na yeyote awezaye kumwamini Yesu kuwa ni Mwokozi.
Hata hivyo
hakuna umuhimu tena kwetu sisi leo hii kumpokea Roho Mtakatifu kupitia miujiza
na maajabu ya kuonekana kwa macho ya kawaida kwa sababu Biblia imekamilika.
Badala yake sasa, kuwa na Roho Mtakatifu ndani yetu kunategemea imani zetu
zaidi. Kwa maneno mengine ni kuamini Injili ya kweli. Mungu ametupatia Roho
Mtakatifu awe ndani yetu kwa wale tu watakao kuwa na imani ya Injili ya kweli
mbele ya Mungu. Kuwa na Roho Mtakatifu ndani hutokea kwa wale tu wanao amini
maneno ya Mungu kama ilivyo timia kwa kuja kwake Yesu hapa ulimwenguni na kwa
ubatizo wake na damu yake.
Nyakati hizi
wachungaji wengi hufundisha waumini wao kwamba matendo yasiyo ya kawaida
yawezayo kuonekana kwa macho ndiyo ishara tosha ya kuwa na Roho Mtakatifu.
Hivyo
kuwaongoza
waumini kumpokea Roho Mtakatifu kwa njia hiyo. Huwapotosha watu kwa kuwapa
mafundisho ya uongo kama yale ya kunena kwa lugha kuwa ndiyo ishara ya
kushukiwa na Roho
Mtakatifu.
Wachungaji hawa hujiona kuwa wao ndiyo mitume watendao miujiza na maajabu makuu
na hivyo kuvutia washabiki wa kidini ambao hutaka kumjua Mungu kwa hisia zao.
Ushabiki huu
umeenea kwa Wakristo walio wengi duniani pote na wengi wao hufuata imani hizo
na hatimaye kupatwa na roho za kishetani kwa kupitia njia za nguvu za giza.
Hata leo, watu hao waliokumbwa na ushabiki wa aina hii hudhani kuwa nao
wataweza kuwafanya wenzao kuweza kumpokea Roho Mtakatifu kupitia kuwekewa
mikono.
Hata hivyo kwa
jinsi Simoni alivyo potoka, nao huwa kama wachawi wanaonekana katika kifungu
hicho. Wameharibiwa kwa kujikonga nafsi zao na tamaa ya mwili lakini matendo
yao
yote huleta
tafrani katikati ya watu. Aina hii ya mafundisho ya uongo hupindisha njia ya
kweli katika kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu mbele ya Mungu.
Hata leo, wengi
wa mitume waongo hufanya kazi za ibilisi kupitia mambo yasiyo sahihi ya kidini,
wakijifanya kutenda kazi za Roho Mtakatifu. Wakristo walio wa kweli ni lazima
walishike neno
la Mungu ambalo ndiyo ufahamu pekee wa kuweza kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu
ndani. Wale wote wanaojifanya kuwa ni Wapentekoste, ambao husisitizia mwonekano
wa nje kimwili nilazima waache imani hizi potofu wayarejee maneno ya Mungu na
kuamini ukweli ambao kwa hakika utawaongoza katika kumpokea Roho Mtakatifu
ndani yao.
Simoni alikuwa
mchawi maarufu Samaria katika nyakati hizo. Baada ya kuwaona mitume wa Yesu
wakisababisha watu kumpokea Roho Mtakatifu, alitamani kumnunua Roho Mtakatifu
kwa fedha. Watu wa imani ya aina hii bila shaka huishia kuwa watumwa wa ibilisi
wakitumiwa kutenda kazi zake. Simoni alitaka kumpokea Roho Mtakatifu lakini tama
zake zilikuwa si nyingine bali ni kujipatia kipato binafsi.
Tunaweza kuona
aina hii ya imani siyo yakupelekea kumpokea Roho. Simoni alijaribu kumnunua
Roho Mtakatifu kwa fedha kwasababu ya uchoyo ulio tokana na kutamani nguvu za
Roho Mtakatifu. Alikemewa vikali na mtumishi wa Mungu Petro. Ingawa ilisemekana
kwamba Simoni alikuwa akimwamini Yesu hakuwa ni mtu kamwe aliyekuwa amempokea
Roho Mtakatifu kupitia ondoleo la dhambi. Kwa maneno mengine yeye alidhani
ya kwamba
angeweza kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yake kwa kutoa mali za kidunia
kwa Mungu.
Ingawa muonekano
wake wa nje ulionyesha kwamba alikuwa akimwamini Yesu, mawazo yake halisi ndani
yalikuwa hayawiani na maneno ya Yesu. Badala yake alijawa na tamaa za kimwili.
Petro aliye yagundua mawazo ya Simoni alimkemea kwa kuwa alijaribu kutaka
kumpokea Roho Mtakatifu ambaye ni zawadi ya Mungu kwa fedha. Alimtaadharisha
Simoni kwamba angeweza kuangamia na fedha hizo zake.
Nyakati hizi
mitume waongo walio tawaliwa na roho za ibilisi hunena kwa kuwalaghai watu kwa
kuwafanya kudhani kwamba miujiza na maajabu yote ni kazi za Roho Mtakatifu. Tunaweza
kuona mara nyingi watu wakifurahia aina hizi za nguvu na kuomba kwa dhati nao
waweze kumpokea Roho Mtakatifu. Hata hivyo mtu imempasa kuwa makini kwamba hapana
yeyote utakaye mpokea Roho Mtaktifu ndani yake kupitia maombi yaliyo na tamaa
za kidunia.
Je, wapo pia watu wa uamsho wa vipawa (karismatiki)
kati yako kwa nafasi yoyote? Imekupasa uwe mwangalifu dhidi ya watu wa aina
hii.
Huwafata watu
kwa imani hizi za mashamshamu na kishabiki. Husema kwamba wanaweza
kukemea mapepo na hata kuweza kuwafanya
watu kumpokea Roho Mtakatifu kupitia kuwawekea mikono. Hata hivyo watu hawa
huwa na nguvu ambazo si za Roho Mtakatifu bali ni
nguvu za pepo
wachafu. Wale wanaodai kumpokea Roho Mtakatifu kwa njia ya kuwekewa mikono
hujiongoza wao binafsi na wengie katika kumpokea roho chafu.
Kupokea uwepo wa
Roho Mtakatifu huja kwa sisi wote tu, tunaoamini maneno ya maji na Roho (1 Yohana 5:3-7). Ingawa injili ya maji na Roho
imeandikwa kwa uwazi katika Biblia, bado watu walio wengi hudhani mioyoni mwao
kwamba wataweza jaribu kumfikia Mungu kwa kupitia nguvu za miujiza na kwa hali
za kupumbaza, kunena kwa lugha, maono na kukemea pepo. Na ndiyo maana manabii
waongo wameweza kuwadanganya watu wengi katika kuamini mazingaombwe ya Kikristo
yatokanayo na ibilisi mwovu.
Petro alimkemea
Simoni kwa kumwambia, “Fedha yako na ipotee mbali pamoja nawe, kwa kuwa
umedhania kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali. Huna fungu wala huna sehemu
katika jambo hili. Basi tubia uovu wako huu ukamwombe Bwana ili kama yamkini
usamehewe fikra hii ya moyo wako. Kwa maana nakuona u katika uchungu kama nyongo
na tena u katika kifungo cha uovu.” Yatupasa kujawa na simanzi kwa
sababu leo hii wapo watumishi wa aina hii. Wengi wao ni wale wajiitao
wenye vipawa au wakarismatiki. Hudai fedha kwa makundi yao. Tuwe mbali
sana nao na watu wa imani hizi na tumpokee Roho Mtakatifu ndani yetu kwa
Injili ya kweli katika maji na Roho (Mathayo 3:15, 1 Petro 3:21, Yohana 1:29, Yohana
19:21-23).
1xbet » Free Bet, Bonus, Deposit & Review | Dec 2021
JibuFutaWhat is herzamanindir.com/ 1xbet? — งานออนไลน์ 1xbet is a casino that offers a selection of online ventureberg.com/ casino games, such as slots, 1xbet korean roulette, and poker. There are 토토