Jumamosi, 12 Aprili 2014

MWANADAMU HUTENDA DHAMBI KATIKA MAISHA YAKE YOTE


Katika 1Yohana1:10 inasema  “tukisema kwamba hatukutenda dhambi twamfanya yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo mwetu”.Hapajatokea yeyote ambaye hajatenda dhambi mbele ya Mungu. Hata biblia inasema “bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa duniani ambaye afanyaye mema asifanye dhambi(Mhubiri 7:20).Watu wote hutenda dhambi mbele ya Mungu.
Ikiwa mtu yeyote atasema kwamba hajatenda dhambi basi ni muongo. Watu hutenda dhambi maishani mwao pote hadi saa ya mwishoni kabla ya kufa, na hii ndiyo maana Yesu alibatizwa na Yohana ili kubeba dhambi hizo zote. Ikiwa hatujawahi kutenda dhambi basi tusingelihitaji kumwamini Mungu kuwa ni mwokozi. Bwana anasema “neno langu si neno lako” kwa wale wenye fikra wakidhani kuwa hawajatenda dhambi.
Ikiwa mtu hana imani katika injili njema ya maji na Roho basi anastahili kuangamia. Ikiwa mtu mwenye haki au mwenye dhambi atasema kwamba hajatenda dhambi mbele za Mungu, basi huyo hatastahili kuiamini injili njema.
Bwana amempa kila mmoja zawadi nzuri ya injili njema. Tulikiri dhambi zetu zote nakutubu ilikupokea msamaha kwa injili njema. Tunaweza kuirudia injili hii ambayo Mungu aliyo tupatia kama msamaha wa dhambi zetu na kuiamini ili kuweza kuwa na usharika wa Roho Mtakatifu. Maana ya kweli ya usharika wa Roho mtakatifu ipo katika injili ya maji na Roho, na pia kwa wale tu walio na injili hii ndiyo watakao weza kuwa na ushirika na Mungu.
Wanadamu walikuwa mbali na Mungu kwa sababu ya dhambi walizorithi kwa Adamu na Hawa. Lakini leo hii sisi tuliokuwa tumerithi mbegu ya uovu tunaweza kutarajia kuwa na usharika na Mungu kwa mara nyingine tena. Ili kuweza kufanikisha hayo yote ni lazima tuwe na imani ya injili ya maji na Roho toka kwa Yesu Kristo, na hivyo kuwa na msamaha wa dhambi ambazo zilituweka mbali na Mungu.
Wale wote wenyekuamini injili njema ndiyo watakao okolewa kutokana na dhambi zote, na hapo basi Mungu atawajaza Roho Mtakatifu. Wenye haki wataweza kuwa na ushirika na Mungu kwa kuwa wamempokea Roho Mtakatifu. Kwa wale wote waliowekwa mbali na Mungu kutokana na dhambi zao lazima wairudie injilinjema ya maji na Roho na kuiamini na hapo ndipo watakapoweza kuanza kuwa na ushirika na Mungu.
Kuwa na Roho Mtakatifu ndani huja kutokana na imani katika injili njema. Lazima tujue kwamba kuwa na Roho Mtakatifu ndani yetu huja pale tunapoamini injili ya maji na Roho tu. Kuiamini injili njema ndiko kunako jenga njia mpya kumuelekea Mungu. Bwana amevunja ukuta wa kati ulio kuwa ukitutenganisha naye kwa sababu ya dhambi zote mbili, yaani dhambi tuzitendazo maishani na ile dhambi ya asili, na hivyo tutaruhusiwa kuwa na ushirika na Mungu kwa kupitia imani yetu katika injili njema ya maji na Roho.
Yatupasa kuanzisha upya ushirika na Roho Mtakatifu kwa mara nyingine tena. Usharika wa kweli na Roho Mtakatifu hufanikishwa kwa kupita kuelewa injili ya maji na Roho na kutii kwa imani. Ushirika wa Roho Mtakatifu huja pale tunapokuwa na imani ya kweli na msamaha wa dhambi ambao unatokana na injili njema. Wale wote ambao wahajapokea msamaha wa dhambi kamwe hatoweza kuwa na ushirika wa Roho Mtakatifu.

Kwa maneno mengine hakuna yeyote atakaye weza kuwa na ushirika wa Roho Mtakatifu pasipo kuiamini injili ya maji na Roho. Ikiwa bado ni vigumu kwako kuwa na ushirika wa Roho Mtakatifu basi ni lazima kwanza ukubali kwamba bado hajaamini injili ya maji na Roho na hivyo dhambi zako hazijasafishwa. Je, unatamani kuwa na uhusiano na Roho Mtakatifu? Sasa basi amini injili iliyokamilishwa kwa ubatizo wa Yesu na damu yake. Ndipo hapo tu utaweza kusamehewa dhambi zako zote na thawabu yako itakuwa ni kumpokea Roho Mtakatifu ndani ya moyo wako. Injili hii njema kwa hakika ndiyo inayotuletea ushirika na Roho Mtakatifu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni