.
Somo la kwanza
(Kutoka 25:1-9) “BWANA
akanena na Musa, akamwambia: waambie wana wa Israeli kwamba wanitwalie sadaka;
kila mtu ambaye moyo wake wampa kupenda mtatwaa kwake sadaka yangu. Sadaka
utakayopokea mikononi mwao ni hii: dhahabu, na fedha, na shaba; na nyuzi za
rangi ya bluu (samawiti), na za rangi ya zambarau, na za rangi nyekundu, na
kitani safi, na singa za mbuzi; na ngozi za kondoo waume zilizotiwa rangi
nyekundu, na ngozi za pompoo, na miti ya mshita; na mafuta ya ile taa, na
viungo vya manukato kwa yale mafuta ya kupaka, na kwa ule uvumba wenye harufu
nzuri; na vito vya shohamu, na vito vingine vya kutiwa kwa ile naivera, na kwa
kile kifuko cha kifuani. Nao wanifanyie
patakatifu; ili nipate kukaa kati yao. Sawasawa na haya yote nikuonyeshayo,
mfano wa maskani, na mfano wa vyombo
vyake vyote, ndivyo mtakavyo vifanya.”
Baada ya Mungu
kumpatia Musa amri kumi na sheria 613, kisha mungu akamwita Musa kwenda mlimani
kwa mara nyingine, wakati huu alimwita ili kumwamuru kulijenga Hema takatifu la
kukutania.
Kulikuwa na
lengo mahususi ambalo kwa hilo Mungu alimwambia kuzileta sadaka hizi. Lengo
hilo lilikuwa ni kuijenga hapa duniani nyumba ya Mungu yenye kung’aa, mahali
ambapo hapana dhambi na ambapo Mungu atakaa , ili aweze kukutana na watu wa
Israeli na kuzifanya dhambi zao kutoweka. Hata hivyo, hii haimaanishi kuwa
Mungu aliwaeleza kuleta fedha ili kujenga jumba la kumbukumbu kama yalivyo
makanisa ya leo. Manabii wa uongo wa Ukristo wa leo wanatumia kifungu hiki
vibaya pale wanapotaka kuyajenga makanisa yao ili kuzitimiza tamaa zao binafsi.
Kwa kweli,
sababu iliyomfanya Mungu apokee sadaka hizi ilikuwa ni kwa ajili ya kutukomboa
sisi toka katika dhambi zetu na kutuokoa toka katika hukumu yetu. Pia ilikuwa
kwa ajili ya Mungu ili aweze kukutana nasi, sisi ambao tulikuwa tukiishi maisha
yenye huzuni ya kutisha, ili aweze kuziosha dhambi zetu na kuzifanya zitoweke,
na kutufanya sisi kuwa watu wake mwenyewe.
MAANA
YA KIROHO YA SADAKA AMBAZO MUNGU ALIAMURU ALETEWE
Kabla hatujaenda mbali, hebu tutumie muda kidogo kutafakari juu ya maana
ya kiroho ya sadaka hizi ambazo Mungu aliamuru aletewe. Baada ya kutafakari
tutaichunguza imani yetu kwa mtazamo wa sadaka hizo.
DHAHABU, FEDHA NA SHABA
Kwanza ni lazima
tuchunguze mahali ambapo dhahabu, fedha, na shaba vilitumika. Katika Hema Takatifu
la kukutania, dhahabu ilitumika kwa ajili ya mahali patakatifu, Patakatifu pa
patakatifu, na vifaa vilivyokuwamo ndani ya hizo sehemu takatifu ikiwemo kinara
cha taa, meza ya mkate wa wonyesho, madhabahu ya uvumba, kiti cha rehema, na
snduku la ushuhuda.
Dhahabu inamaanisha neema ya wokovu.
Inatueleza kuwa ni lazima tuwe na imani
inayoamini katika zawadi ya wokovu iliyotolewa bure na kwa ukamilifu na masihi,
na imani ambayo inaamini kuwa Bwana wetu amezichukuwa dhambi zetu zote na
kwamba alihukumiwa kwa ajili yetu.
Kwa upande
mwingine, shaba, ilitumika katika
vitanzi vya nguzo za Hema takatifu la kukutania, katika vigingi vyake, birika
la kunawia, na madhahabu ya sadaka ya kuteketezwa. Vifaa au vyombo vyote vya
shaba vilifunikwa au vilipigiliwa ardhini. Hii inamaanisha juu ya hukumu ya
dhambi za watu, pia shaba inatueleza
kuwa tunahukumiwa adhabu na Mungu kwa kushindwa kuitunza na kuifuata Sheria kwa
sababu ya dhambi zetu.
Je, ni namna ipi
ya kiroho ya dhahabu, fedha, na shaba?
Vitu hivi vinaunda misingi ya imani katika kupokea zawadi ya wokovu iliyotolewa
na Mungu. Biblia inatueleza kuwa sisi sote ni wenye dhambi ambao hatuwezi
kuifuata sheria kikamilifu, na kwamba tunastahili kufa kwa sababu ya dhambi
zetu kwa kufanyika sadaka ya kuteketezwa ya dhambi ambayo ilitolewa katika Hema
takatifu la kukutania.
Ili kutatua
tatizo la dhambi zao, wenye dhambi walileta mnyama asiye na mawaa katika Hema
Takatifu la kukutania, na kwa mujibu wa taratibu wa sadaka ya kuteketezwa,
walipeleka dhambi zao katika mnyama huyo wa sadaka kwa kuiwekea mikono yao juu
ya kichwa chake; kisha sadaka ile ya kuteketezwa ambayo ilizipokea dhambi zao
na kumwaga damu yake na kuuawa. Kwa kufanya hivyo, watu wa Israeli ambao
walikuwa wamefungwa kuzimu (shaba), waliweza kupokea ondoleo la
dhambi zao (fedha), na walikwepa
adhabu ya dhambi zao kwa imani (dhahabu).
NYUZI ZA BLUU (SAMAWITI), ZAMBARAU, NYEKUNDU NA KITANI SAFI
YA KUSOKOTWA.
Hapa kuna vifaa vingine vilivyotumika mara kwa
mara; nyuzi za bluu, zambarau, na
nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa.
Nyuzi hizi zilitumika katika lango la ua wa Hema takatifu la kukutania, lango
la mahali patakatifu, na katika pazia lilotenganisha kati ya mahali patakatifu
na patakatifu pa patakatifu. Nyuzi hizi nne zinatueleza juu ya ukweli kuwa kama
ilivyo tabiriwa katika Mwanzo 3:15, kwamba
Bwana atakuja kama sehemu ya uzao wa mwanamke, na kuwaokoa wenye dhambi toka
katika dhambi zao kwa kubatizwa na kusulibiwa, na kwamba ni mungu mwenyewe
ndiye atakaye tuokoa sisi.
Nyuzi nne
hazikutumika tu kwa ajili ya malango ya Hema Takatifu la kukutania, bali
zilitumika pia katika mavazi ya kuhani mkuu na yalitumika kama kifuniko cha
kwanza cha Hema takatifu la kukutania. Hili lilikuwa ni Agano la mungu kwamba
Yesu Kristo atakuja hapa duniani na kutuokoa toka katika dhambi zetu kwa
kutimiza kazi zake za nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Kwa kweli Bwana
wetu alitekeleza ahadi hii na kwa hakika ametuokoa toka katika dhambi za ulimwengu.
Sehemu ya msingi
katika malango ya Hema takatifu la kukutania ni nyuzi za bluu. Kwanini Yesu Kristo kama masihi alikuja hapa duniani na kufa
msalabani? Ni kwasababu Yesu alibatizwa. Nyuzi za bluu zinatuonyesha juu ya ubatizo wa Yesu, nyuzi za zambarau zinatueleza kuwa Yesu ni mfalme
(Yohana 19:2-3),na nyuzi nyekundu zinatueleza juu ya kusulubiwa
kwake na kumwaga damu yake. Nyuzi hizo zote ni vifaa vya ujenzi, ambavyo ni
muhimu sana kutuonyesha jinsi Yesu alivyokuja hapa duniani na kuchua dhambi
zetu katika mwili wake.
Watu wengi
katika ulimwengu huu wanasisitiza kuwa Yesu ni mwana wa Mungu tu, na kwamba
kimsingi yeye ni Mungu mwenyewe. Lakini anatueleza wazi kupitia Hema takatifu
la kukutania kwamba mafundisho ya jinsi hiyo hayawezi kuwa ndiyo kweli kamili.
Mtume petro
katika 1Petro 3:21, “mfano
wa mambo hayo ni ubatizo, unao waokowa ninyi pia siku hizi; (siyo kuwekea mbali
uchafu wa mwili, bali jibu la dhamira safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake
Yesu Kristo.”
Hii inatuonyesha
sisi kuwa Yesu aliitimiza ahadi ya wokovu na akaweka msingi wa imani mkamilifu
kwa kupokea ubatizo wake, mfano unao tuokoa sisi. Masihi wetu ni nani? Maishi
maana yake ni mwokozi, neno hili linatueleza kuwa Yesu alikuja hapa duniani,
alibatizwa ili kuzichukuwa dhambi zetu
zote na dhambi za ulimwengu katika mwili
wake kwa njia ya ubatizo.
Mungu aliwaeleza
Waisraeli kulijenga lango la ua wa Hema takatifu la kukutania kwa kufuma nyuzi
za bluu, zambarau na nyekundu na kitani
safi ya kusokotwa. Na dhumuni la Bwana wetu, ambaye ndiye mfalme wa wfalme
na Bwana wa mbingu, kuja hapa duniani katika mwili wa mwanadamu ilikuwa ni
kuutimiza ukweli wa nyuzi za bluu,
zambarau, na nyekundu na kitani safi ya
kusokotwa. Bwana wetu alikuja katika mwili wa mwanadamu na akaupokea
ubatizo ambao ungeittimiza haki yote ya Mungu toka kwa Yohana Mbatizaji, ambaye
ni mwakilishi wa wanadamu.
Hii inafanana na
sadaka ya kuteketezwa ya Agano la kale ambayo ilizipokea dhambi za
Waisraeli ambazo zilipitishwa katika
sadaka hiyo kwa kuwekewa mikono na kuhani mkuu katika kichwa chake na kwamba
mnyama huyu wa sadaka alihukumiwa kwa dhambi hizo akiwa mbadala kwa dhambi za
Waisraeli waliokosa. Kwa maneno mengine, kama ilivyo kuwa kwa sadaka ya
kutetezwa ya Agano la kale, Yesu alikuja katika Agano jipya kama sadaka ya
kuteketezwa kwa ajili ya dhambi za wanadamu, alibatizwa, alisulubiwa, na kwa
hiyo alibeba adhabu yote ya dhambi za ulimwengu. Yesu aliutimiza ukweli wa
nyuzi za bluu kwa kubatizwa na Yohana
kama mwana kondoo wa Mungu wa sadaka. Kwa ubatizo huu Yesu alizichukuwa dhambi
za wanadamu katika mwili wake mara moja na kwa wote.
Na nyuzi nyekundu zinamaanisha damu ya Yesu.
Sababu iliyomfanya Yesu Kristo akasulubiwa, akamwaga damu yake, na akafa msalabani
ni kwa sababu dhambi zetu zote zilikuwa zimepelekwa kwake kupitia ubatizo. Ni kwa sababu Yesu alizichukuwa dhambi zetu
kwa ubatizo wake alioupokea toka kwa Yohana Mbatizaji ndipo alipoweza kufa
msalabani, na kwa sababu ya ukweli huu kwamba sadaka ya pale msalabani kwa
ajili yetu haikuishia pasipo maana.
Nyuzi za zambarau zinamaanisha kuwa Yesu Kristo ni
Mungu na mfalme, lakini kama asingebatizwa na Yohana Mbatizaji ambaye ni
mwakilishi wa wanadamu, na kama asingelikuwa amezichukuwa dhambi zetu katika
mwili wake (nyuzi za bluu), Haijalishi ni kwa kiwango gani cha mateso na
maumivu aliyopata (nyuzi nyekundu), kifo chake kingekuwa hakina maana. Kitani safi ya kusokotwa inatueleza sisi kuwa neno la unabii ambalo Mungu
aliliongea katika Agano la kale limetimizwa lote katika Agano jipya.
Soma mwendelezo wa somo hili………………
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni