(Kutoka 30:17-21) “BWANA akanena na Musa, na kumwambia, Fanya na birika la
shaba, na kitako chake cha shaba, ili kuogea; nawe utaliweka kati ya Hema
takatifu la kukutania na madhabahu, nawe utalitia maji. Na Haruni na wanawe
wataosha mikono yao na miguu yao humo; hapo waingipo ndani ya hema takatifu la
kukutania; watajiosha majini, ili wasife; au hapo watakapoikaribia madhabahu
ili watumike, kumtengenezea BWANA sadaka ya moto; basi wataosha mikono yao na
miguu yao ili kwamba wasife; na neno hili litakuwa amri kwao milele, kwake yeye
na kwa wazao wake katika vizazi vyao vyote.”
Birika la kunawia katika Ua wa Hema takatifu la kukutania
Vifaa:
ilitengenezwa kwa shaba, ilikuwa imejazwa na maji wakati wote.
Maana ya kiroho: Shaba ina maanisha hukumu ya dhambi zote za
mwanadamu, Yesu alizichukuwa dhambi za ulimwengu katika mwili wake kwa
kubatizwa na Yohana. Kwa hiyo, maana ya birika la kunawia ni kwamba tunaweza
kuoshwa dhambi zetu zote kwa kuamini kwamba dhambi hizi zote zilpitishwa kwa
Yesu kwa kupitia ubatizo wake.
Makuhani waliohudumu katika Hema
takatifu la kukutania pia waliosha mikono yao na miguu yao katika birika la
kunawia kabla ya kuingia katika Hema Takatifu la kukutania na kwa hiyo
walikiepuka kifo chao. Shaba inamaanisha hukumu ya dhambi, na maji ya kwenye
birika la kunawia yanamaanisha ubatizo ambao Yesu aliopokea toka kwa Yohana na
ambao kwa huo alizichuwa dhambi za ulimwengu katika mwili wake. Kwa maneno
mengine, birika la kunawia linatueleza kuwa Yesu alizipokea dhambi zetu zote zilizopitishwa
kwake na akabeba adhabu ya dhambi hizi. Maji katika birika la kunawia
yanamaanisha, katika Agano la kale, nyuzi za bluu za hemataktifu la kukutania,
na katika Agano jipya, ubatizo ambao Yesu aliopokea toka kwa Yohana (Mathayo 3:15, 1petro 3:21).
Kwa hiyo, birika la kunawia linamaanisha
ubatizo wa Yesu, na ni mahali ambapo tunathibitisha imani yetu katika ukweli
kuwa Yesu alibeba dhambi zetu zote, zikiwemo dhambi zetu halisi, na
akazioshelea mbali zote mara moja kwa kupitia ubatizo alioupokea toka kwa
Yohana Mbatizaji.
Watakatifu ambao wameokolewa toka
katika dhambi zao kwa imani wamevishwa neema ya Mungu kwa kuyaamini maji ya kwenye birika la
kunawia (ubatizo wa Yesu), Shaba (hukumu ya Mungu kwa dhambi zote), na kwamba
Yesu amewakomboa toka katika dhambi zao. Ingawa tuna wingi wa udhaifu na
mapungufu kiasi kwamba hatuwezi kujitambua sisi wenyewe kuwa ni wenye haki, kwa
hakika tunaweza kudhibitisha kwamba sisi ni wenye haki wakamilifu kwa kuiweka
tena na tena imani yetu katika ubatizo wa Yesu (kuzibeba dhambi, maji) na damu
yake iliyomwagwa msalabani (adhabu ya dhambi, shaba). Kwa sababu tunaliamini
Neno la Mungu ambalo limekwisha kutuokoa sisi sote toka katika dhambi zetu na
adhabu ya dhambi hizi, basi tunaweza kufanyika wenye haki wasio na dhambi.
Neno la Mungu tunaloliamini linatueleza
sisi kuwa Yesu alizichukuwa dhambi zetu katika mwili wake kwa kupitia ubatizo
wake alioupokea toka kwa Yohana, akamwaga damu yake msalabani ili kuibeba
adhabu yote ya dhambi badala yetu, na kwa hiyo ametuokoa sisi kikamilifu toka
katika dhambi zetu. Mungu aliliweka birika la kunawia katika ua wa Hema Takatifu
la kukutania ili kwamba tuweze kudhibitisha kwa imani yetu kuwa sisi ndiyo
tuliookolewa kikamilifu toka katika dhambi zetu zote bila kujali hali
inavyoweza kuwa.
Matumizi ya birika la kunawia
Birika la kunawia lilitumika
katika kuosha uchafu wote wa makuhani walipofanya kazi katika Hema Takatifu la
kukutania wakitoa sadaka kwa Mungu. Ilihitajika kuyaosha madoa ambayo makuhani
waliyapata katika kuua mwanasadaka wa kuteketezwa, katika kuikinga damu yake,
na katika kuikata vipande ili kumtolea Mungu sadaka ambayo itawapatanisha watu
wa Israeli na Mungu toka katika dhambi zao. Wakati makuhani walipochafuliwa
walipokuwa wakitoa sadaka, iliwapasa kuoshwa kwa maji, na birika la kunawia
lilikuwa ni mahali ambapo uchafu huu wote ulisafishwa.
Tunapofanya dhambi, kiroho au
kimwili, na kila inapotokea kuwa tumechafuliwa kwa kuzivunja amri za Mungu, ni
lazima tuoshelee mbali uchafu wetu wote katika birika hili la kunawia.
Ilipotokea kuwa miili ya makuhani imegusa kitu chochote kichafu, walipaswa kwa
lazima kuosha sehemu zilizochafuka katika miili yao kwa maji.
Vivyo hivyo, inapotokea kuwa wale
wanaoamini katika Mungu wamegusana na kitu chochote kisicho safi na kichafu,
maji ya birika la kunawia yanatumika kuoshelea mbali huo uchafu wote. Kwa
kifupi, maji ya birika la kunawia yalitolewa ili yatumike katika kuuosha uchafu
wa waliozaliwa upya. Kwa hiyo, birika la kunawia lina rehema za Mungu. Maana ya
birika la kunawia si kitu cha kuchagua ambacho tunaweza kuchagua kuamini au
kutoamini, bali ni kitu cha muhimu na lazima kwa wale wanaomwamini Yesu.
Mungu alitoa vipimo kwa vifaa
vingine vyote katika Hema Takatifu la kukutania, akatoa vipimo maluumu jinsi
ambavyo vitakuwa na dhiraa kadhaa kwa kimo, urefu, na upana. Lakini hakutoa kipimo
cha birika la kunawia. Hii ni tabia ambayo inaapatikana tu katika birika la
kunawia. Hii inadhihirisha upendo usiokoma ambao masihi ametupatia sisi, ambao
tunatenda dhambi halisi kila siku. Katika upendo huu wa masihi kunapatikana ubatizo wake, aina ya kuwekewa
mikono ambayo inaziosha dhambi zetu zote. Kama ambavyo maji mengi yalitumika
wakati makuhani walipokuwa wamechafuka wakati wakitekeleza majukumu yao,
ilikuwa ni lazima birika la kunawia lijazwe maji wakati wote. Kwa hiyo, kipimo
cha birika la kunawia kilitegemeana na hitaji hili. Kwa sababu birika la
kunawia lilitengenezwa kwa shaba, basi kila ilipotokea makuhani wakinawa,
walikuwa wanafikiria juu ya hukumu ya dhambi.
(Waebrania
10:22) inasema “tumeoshwa miili
kwa maji safi”, na (tito3:5) “
kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa mara ya pili na kufanywa upya na Roho mtakatifu.” Kama
Vifungu hivi vinavyoonyesha, Neno la Agano Jipya pia linatueleza sisi kuhusu
kuuosha uchafu kwa maji ya ubatizo.
Ikiwa makuhani waliosha uchafu
wao walioupata katika maisha yao kwa maji ya birika la kunawia, sisi wakristo
wa leo tuliozaliwa upya, tunaweza kuzioshelea mbali dhambi zetu Halisi zote
zilizofanywa katika maisha yetu kwa kuamini ubatizo wa Yesu. Maji ya birika la
kunawia la Agano la kale yanatuonyesha sisi kuwa Masihi alikuja hapa duniani na
amezisafishaia mbali dhambi zote za ulimwengu kwa ubatizo aliopokea toka kwa Yohana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni