Jumatano, 26 Machi 2014

MUNGU ROHO MTAKATIFU


Mungu Roho Mtakatifu sio nguvu tu bali pia anazo tabia
Roho Mtakatifu ni nafsi ya tatu katika utatu. Imani ya Mitume inaweka mkazo katika Roho Mtakatifu, inasema “namwamini Roho Mtakatifu” ni muhimu sana kwa Mitume kujua hakika huyu Roho Mtakatifu na kazi zake ni zipi. Na pia tunapaswa kujua vipawa vya Roho Mtakatifu, ambavyo vitafafanuliwa mbele kidogo ya sura hii. Tunapokiri kumwamini Roho Mtakatifu, kabla hatujatafakari nguvu za ajabu alizo nazo, ni lazima tuzingatie ukweli kuwa tunapokea Roho Mtakatifu pale tunapomwamini Mungu Baba na kazi za Mwanae. WaKristo wengi wana tabia ya kudhani wanaweza kupokea Roho Mtakatifu muda wowote na mara nyingi wanavyoweza. Lakini hili ni kosa kubwa. Lazima tutambue kuwa Roho Mtakatifu sio malaika, ila ni Mungu anayestahili sifa na kuabudiwa. Tunaweza kupokea Roho Mtakatifu tukimwamini Mungu Baba na kazi za Mwanae.
*      Mungu Roho Mtakatifu hufanya nini?
Nini hasa Roho Mtakatifu hufanya? Kwanza Roho Mtakatifu hushiriki katika huduma inayoogozwa na Mungu Baba na Mwana. Roho Mtakatifu alishiriki katika kazi za uumbaji zilizoanzishwa na Mungu Baba. Si hayo tu, pia alishiriki katika kazi za uumbaji zilizoanzishwa na Mungu Baba. Si hayo tu, pia alishiriki katika kazi za ukombozi zilizokamilishwa na Mungu Mwana kwa kuleta ushuhuda. Hii inajionyesha katika huduma ya ukombozi iliyokamilishwa na Yesu na kukamilishwa kwa kila mtume.
*      Tunawezaje kupokea ubatizo wa Roho Mtakatifu?
Ili kuelewa ubatizo na Roho Mtakatifu, kwamba tunapaswa kuelewa kwa nini Yesu alibatizwa na Yohana na kufa msalabani. Katika (warumi 3:23) tunasoma “wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” kila Mwanadamu amezaliwa akiwa na dhambi na hawezi ila kutenda dhambi mbele za Mungu, na kulingana na (warumi 6:23), inayotuambia kuwa “mshahara wa dhambi ni mauti” kila Mwanadamu hawezi kujiepusha na hukumu ya kifo kama mshahara wake wa dhambi. Lakini Mungu Baba anayewapenda wanadamu, ameandaa njia ambayo kwayo, tunaweza pata ondoleo la dhambi, kuhukumiwa kwazo na kuokolewa kutoka dhambini, yote haya kupitia Yesu, Mungu Baba alimtuma Mwanaye mpendwa, Yesu na akaimimina adhabu juu ya Yesu kupitia ubatizo na kusulubiwa msalabani. Badala yetu Yesu akachukua dhambi na kudhihakiwa hadi kufa na Mungu Baba. Licha ya kuwa Yesu alikuwa na haki alikufa na kushinda mauti. Alifufuka na alitoka kuzimu. Ni kwa jinsi gani sasa utimilifu wa ondoleo la dhambi unaunganishwa na wanadamu? Kwa kuamini kazi zake, maana yake ni sisi kupokea ondoleo la dhambi. Yesu aliyebeba dhambi za wanadamu kwa kubatizwa na Yohana katika mto Yordani alipokea adhabu zote pale msalabani ili kutupa ondoleo la dhambi. Tukiamini kuwa Yesu alibatizwa na Yohana na kuugulia kifo kama kujitoa kwa ajili ya dhambi zetu basi hapo tunapata haki ya Mungu, ya kuwa watoto wake, na kupata nafasi ya uzima wa milele (wagalatia 3:27) inasema “kama wengi wenu walivyobatizwa katika Kristo, wamekuwa waKristo.” (Yohana 3:16) inasema, kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe wa pekee ili kila amwaminie asipotee, bali awe na uzima wa milele” mstari huu, tunastahilishwa mara tu tunapoamini kuwa dhambi zetu zimepitishwa kwa Yesu kwa ubatizo aliopokea kwa Yohana na kuamini adhabu ya msalabani. Neno ubatizo linabeba maana nyingi mojawapo ni kutakasa dhambi, na ya pili ni kuunganisha. Ni lazima tutambue kuwa, kubatizwa na Roho Mtakatifu ni kujua na kuamini namna gani Yesu ameondoa matatizo ya maovu ya wakosaji ni kuwa ni kwa imani tunapokea ubatizo wa Roho mtakatifu. Kuwa Roho Mtakatifu amekuja mioyoni mwetu, kukaa ndani yetu na kutunganisha, ina maana tumeamini ubatizo wa Yesu. Huduma hii ya Roho Mtakatifu imeelezwa vizuri katika (Mathayo 3:13-17). Yesu alisema kuwa sababu ya kubatizwa kwake na Yohana ilikuwa kutimiza haki ya Mungu kwa mbinu ya ubatizo wake aliopokea kutoka kwa Yohana. Hivyo kupokea Roho Mtakatifu, ni sharti kwanza tuamini kwamba Yesu alichukua dhambi za wanadamu kwa kubatizwa na Yohana. Hivyo ndivyo tunavyoweza kuunganishwa na Roho Mtakatifu, hata Biblia pia inasema kuwa tunampokea Roho Mtakatifu kwa kuamini neema ya ondoleo na dhambi, kwamba Yesu alisulubiwa na kuimwaga damu yake kwa sababu alizikubali dhambi zote za wanadamu kupitia ubatizo wake. Roho Mtakatifu anakaa ndani ya mioyo yetu na wale waliotakaswa dhambi zao kwa ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani. Hii inaonekana katika mazungumzo kati ya Yesu na Nikodemu. Nikodemu alienda kumwona Yesu, Yesu akamwambia wale waliozaliwa upya wanaweza kuuona ufalme wa Mungu. Kuzaliwa upya maana yake, Roho iliyokufa inahuishwa na kufanywa mpya, na kupata nafasi katika ufalme wa mbinguni. Kusikia ukweli juu ya kuzaliwa upya, Nikodemu hakuelewa maana yake, ndipo akamwuliza Yesu, hayo yanawezekanaje.
Yesu akajibu  “Amini Amini nakuambia, Usipozaliwa kwa maji na kwa Roho huwezi kuingia Ufalme wa Mungu.” (Yohana 3:5) kwa kuamini tu huduma ya Yesu kuwa ndiyo iliyoondoa dhambi zote za dunia na hata mizizi ya dhambi, ndipo tunaweza kuzaliwa upya na kazi hiyo ya ajabu ilitimia Yesu alipobatizwa na kufa msalabani tukiamini, Roho Mtakatifu atakaa ndani yetu. Hakuna juhudi, kazi wala mafanikio, uwezo au tabia ya mtu inayoweza kukufanikisha katika hili. Tunahitaji imani ile inayoamini ukweli kuwa ubatizo wa Yesu na kifo chake msalabani ndivyo vinavyotakasa dhambi za wanadamu. Tunahitaji kuzingatia yale Yesu aliyoendelea kusema katika mazungumzo yake na Nikodemu. Yesu alisisitiza umuhimu kuwa ni sharti tuzaliwe upya kwa maji na Roho. Huduma ya Roho Mtakatifu inayohuisha Roho zetu, kwa ubatizo wa Roho Mtakatifu sio tu ni badiliko la kuanzia ndani ya moyo wa mtu, bali pia ni huduma kubwa inayotendeka. Kwa sababu ya hili, huduma yenyewe haiwezi kuonekana kupitia sababu zetu au ufahamu wetu. Tunaloweza kujua ni kupokea ubatizo wa Roho Mtakatifu pamoja na ondolea la dhambi tulilopokea ndani ya mioyo yetu tulipoamini ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani. Tunatambua kuwa tumekuwa watoto wa Mungu tunapopokea Roho Mtakatifu kama zawadi (Warumi 8:15).
*      Roho Mtakatifu ni nani?
Roho Mtakatifu ni nafsi ya tatu ya Uungu. Imani ya Utatu ndio msingi mkubwa wa imani. Ukweli wote unaweza kufahamika na kueleweka kwa kuamini Injili ya Maji na Roho. Kwa nini? Sababu ni kama zifuatazo.
·         Kwa sababu wenye dhambi ni viumbe wa Mungu, ukweli juu ya utatu hauwezi kujulikana hadi mtu anapopata ondoleo la dhambi kwa kuiamini Injili ya maji na Roho.
·         Kwa sababu ya makosa yetu, mioyo ya wanadamu imetiwa giza na dhambi. Kama vile kioo kisivyoweza kuona kikiwa kimepakwa tope, macho ya mioyo ya wenye dhambi hayawezi kuona yale Mungu wa utatu aliyotenda.
·         Bila nuru ya Roho Mtakatifu, hatuwezi kamwe kujua yaliyo ndani ya Mungu. Kama ilivyo Roho Mtakatifu alivyo shahidi kuwa Neno la Mungu ni kweli (Yohana 16:13), Roho Mtakatifu anatuwezesha sisi kujua ukweli juu ya maji na Roho, kwa kuwa yeye mwenyewe ni Mungu mwenye nafsi kamili na ufahamu, nia na hisia. Anakaa ndani ya wale wanaoamini Neno la Mungu na kulifanyia kazi. Ni sharti tumwabudu yeye, tumwamini na kumtii.

*      Ni zipi kazi kuu za Roho Mtakatifu?
Roho Mtakatifu anafanya kazi ya kutunza Roho za Mitume waliosamehewa dhambi kwa kuamini Injili ya maji na Roho. Roho Mtakatifu anafanya kazi kulingana na imani zetu katika maandiko matakatifu.
·         Anabeba ukweli kuwa Neno la Mungu ni kweli. Roho Mtakatifu anatoa garantii kwa wale walioliamini Neno la ubatizo wa Yesu na msalabani. Yeye anayeihakiki imani yake kuwa ni hakika ni Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu anafanya kazi kati ya wale wanaoliamini Neno. Roho Mtakatifu anahakiki imani ya wale wanaoimini Injili ya maji na Roho. Anatoa garantii, kwa maneno mengine, wale wanaoamini kuwa Yesu alikuja duniani ili kuitakasa dunia na dhambi kwa njia ya ubatizo na damu yake msalabani.
·         Roho Mtakatifu yupo na mwenye haki, na anawafanya waishuhudie injili ya maji na Roho kwa wenye dhambi. Katika Yohana 16:8-9 alisema “akija atauhukumu ulimwengu kwa haki na dhambi kwa sababu hawajamwamini Roho Mtakatifu anaihakiki injili ya maji na Roho katika mioyo ya wenye haki (Yohana 14:26). Anachukua ushuhuda wa yale ambayo Mungu amefanya anatuwezesha kujua kuwa Yesu alikuja duniani, na kuchukua dhambi zetu kwa kubatizwa, kufa msalabani, na anatuwezesha sisi kuyaamini hayo yote.
·         Anafanya tumwamini Mungu, na kuliitia jina lake. Roho Mtakatifu anawafanya wenye haki kuomba. Warumi 8:15 inasema,  “Kwa kuwa hamkupokea tena roho ya utumwa iletayo hofu, bali mlipokea roho ya kufanywa wana. Ambayo kwa hiyo twalia Abba, yaani ‘Baba’”.  Roho Mtakatifu anawawezesha Mitume kumwita Mungu na kumwamini yeye kama “Abba, Baba”.
·         Roho Mtakatifu anatuwezesha kuzifanyia kazi karama alizotupatia. Anatuwezesha kufanya kazi za haki za Mungu kwa uwezo wake 1Wakorintho 15:10 inasema, “kwa neema ya Mungu, nipo kama nilivyo, na neema yake kwangu si bure, nalijitaabisha sana kuliko hao wote, lakini bado si mimi, ila ni neema ya Mungu iliyokuwa pamoja nami.”
·         Roho Mtakatifu anatuongoza mpaka tuingie Mbinguni, Roho Mtakatifu anawawezesha wenye haki kuitunza imani yao mpaka wafike ufalme wa Mungu, na hubaki nao kama mwalimu wao.

*      Kumpokea Roho Mtakatifu ni hatua ya tofauti kwa Mkristo?

Licha ya kuwa Yesu hatoi Roho Mtakatifu kwa wenye dhambi, bado kuna wengi wasio tayari kubadili misimamo yao. Wakati wale wasiojua injili ya maji na Roho wanapopata kiu ya kupokea Roho Mtakatifu, hupokea pepo na kudai na Yesu amewajia na hapo huishia kushikwa na mapepo na nguvu za giza, hivyo, watu wasijaribu kupokea Roho Mtakatifu kwa nguvu zao wenyewe. Ni hatari sana kwa mtu ambaye hajapokea ondoleo la dhambi kuomba apate Roho Mtakatifu. Ni sharti tutambue kuwa, ni upuuzi kuomba jambo lisilowezekana. Biblia inasema, mamlaka ya wale waliopokea ondoleo la dhambi ni kubwa (Yohana 20:23). Yesu alisema  “kama ukisamehe dhambi ya yeyote utasamehewa, ila usiposamehe, hutasamehewa” mamlaka hii wanapewa wale tu, waliopokea ondoleo la dhambi, na kupokea Roho Mtakatifu. Mamlaka kubwa, na majukumu pia ni makubwa. Yesu alimwambia petro, “nimekupa funguo za mbinguni”, hii ni mamlaka waliyopewa wale waliopokea ondoleo la dhambi kwa njia ya Injili ya maji na Roho. Mamlaka ya wale waliopokea ondoleo la dhambi na Roho Mtakatifu mioyoni mwao kwa kuamini injili ya maji na Roho ni ya ajabu sana. Wanayo mamlaka ya kuongoza watu kwenda mbinguni na hata kutupwa kuzimu. Kwa hiyo Mitume hawaenezi Injili ya ondoleo la dhambi kwa wakosaji na kuwaacha jinsi walivyo, hapo itakuwa makosa yapo kwao kwa kuwaacha wakipotea mamlaka ya kusamehe dhambi za watu kutolewa wa Mitume.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni