Somo la pili
Somo hili ni mwendelezo kutoka somo lenye kichwa “MSINGI WA IMANI ULIYOWEKWA NA VIFAA VYA
UJENZI WA HEMA TAKATIFU LA KUKUTANIA”.
Sheria ni kivuli cha mambo mazuri yatakayo kuja, Vifaa vya
ujenzi vya hema takatifu la kukutania vinatuonyesha sisi kuwa Bwana wetu
alikuja hapa duniani katika mwili wa mwanadamu, akazichukuwa dhambi zetu katika
mwili wake, kwa ubatizo wake,akabeba adhabu ya dhambi zetu kwa kusulubiwa
kwake, akafufuka tena toka kwa wafu, na kwa hiyo amefanyika kuwa mwokozi wetu.
(Kutoka 25:1-9) “BWANA akanena na Musa, akamwambia: waambie wana wa Israeli kwamba
wanitwalie sadaka; kila mtu ambaye moyo wake wampa kupenda mtatwaa kwake sadaka
yangu. Sadaka utakayopokea mikononi mwao ni hii: dhahabu, na fedha, na shaba;
na nyuzi za rangi ya bluu (samawiti), na za rangi ya zambarau, na za rangi
nyekundu, na kitani safi, na singa za mbuzi; na ngozi za kondoo waume
zilizotiwa rangi nyekundu, na ngozi za pompoo, na miti ya mshita; na mafuta ya
ile taa, na viungo vya manukato kwa yale mafuta ya kupaka, na kwa ule uvumba
wenye harufu nzuri; na vito vya shohamu, na vito vingine vya kutiwa kwa ile
naivera, na kwa kile kifuko cha kifuani.
Nao wanifanyie patakatifu; ili nipate kukaa kati yao. Sawasawa na haya yote
nikuonyeshayo, mfano wa maskani, na
mfano wa vyombo vyake vyote, ndivyo mtakavyo vifanya.”
MAANA YA KIROHO YA
SINGA ZA MBUZI, NGOZI YA KONDOO DUME ILIYOTIWA RANGI NYEKUNDU, NA NGOZI YA
POMPOO
Vifaa hivi vilitumika katika
kujenga mapaa ya Hema takatifu la kukutania. Paa la kwanza lilifumwa kwa nyuzi
za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa ambapo paa la pili
la singa za mbuzi lililazwa. Kisha lilifunikwa kwa ngozi ya kondoo dume
iliyotiwa rangi nyekundu na mwisho ngozi ya pompoo ililazwa juu yake. Kwa njia
hii aina nne tofauti za tabaka la paa zililifunika hema takatifu la kukutania.
Paa la mwisho ambalo lilifunika Hema
takatifu la kukutania lilikuwa la ngozi za pompoo. Kwa hiyo kilichoonekana
katika uso wa paa la hema takatifu la kukutania lilikuwa ni hizi ngozi nyeusi
za pompoo. Pompoo ni mnyama anayepatikana baharini. Kipimo cha ngozi ya pompoo
ni kama kipimo cha mtu na pengine ni ndogo zaidi kuliko kipimo cha mtu, na aina
hii ya ngozi ilikuwa haipitishi maji. Hii ndiyo sababu ngozi ya pompoo
ilitumika kuezekea paa la Hema takatifu la kukutania. Kwa sababu ya hili, hali
ya nje ya hema takatifu la kukutania Haikuwa ya kuvutia, na bila shaka halikuwa
na mvuto wa kuangalia. Hii ianatueleza sisi kuwa wakati Yesu alipokuwa hapa
duniani kwa ajili yetu, kwa hakika alikuja katika hali ya chini kama ilivyo
kuwa hali ya nje ya hema takatifu la kukutania, hakukuwa na kitu cha
kutamanisha katika mwonekano wake.
Ngozi ya kondoo dume
iliyotiwa rangi nyekundu inatueleza kuwa
Yesu Kristo atakuja hapa duniani na atasulibiwa kwa ajili yetu, ilhali singa za
mbuzi zinatueleza kuwa atatuokoa kwa kubatizwa kama sadaka yetu ya kuteketezwa
na kwa hiyo atazipokea dhambi zetu katika mwili wake kwa kusulubiwa msalabani.
Lakini kwa sababu kuna watu wengi
sana katika ulimwengu huu ambao imani yao haina ufahamu wowote kuhusu ubatizo
wa Yesu, mara nyingi wamezidharau rangi nne za nyuzi zilizotumika katika hema
takatifu la kukutania na badala yake wameyajenga malango yao ya hema takatifu
la kukutania kwa nyuzi mbili tu.
Kwa kufanya hivyo wanawadanganya
watu wengi, ambao tayari hawana uwelewa wa kutosha kuhusu Mungu na ambao
hawajui kabisa neno lake. Hawa wote ni manabii wa uongo. Yesu mwenyewe aliwahi
kuwazungumzia watu wa jinsi hii kwa kuwa ni magugu ambayo shetani aliyapanda
katikati ya ngano (Mathayo 13:25). Kwa maneno
mengine, wamekuwa ni watu ambao wanaeneza uongo kwa kuwacha nyuzi za bluu
katika michoro yao ya ua wa Hema takatifu la kukutania. Hii ndiyo sababu watu
wengi sana wanabakia ni wenye dhambi hata baada ya kuwa wanamwamini Yesu. Pamoja
na imani yao katika Yesu bado wamefungwa katika uharibu kwa sababu ya dhambi
zao.
Msingi wetu wa imani lazima uwe
imara. Kuna uzuri gani kuishi kipindi kirefu cha maisha ya kidini katika nafsi
yako ilhali maisha hayo yapo katika msingi usio wa sheria kiimani? Haijalishi kuwa
nyumba zetu ni nzuri kiasi gani, kutakuwa na uzuri gani ikiwa tunajenga nyumba
hizi katika msingi dhaifu wa kiimani? Bila kujali jinsi ambavyo umemtumikia
Mungu kwa juhudi, ikiwa msingi wako wa imani una dosari, basi utakuwa umejenga
nyumba yako katika mchanga; dhoruba itakapokuja na upepo kuvuma, na mafuriko
yakaja, yataipiga nyumba yako nayo itaanguka chini mara moja.
Je, ni vipi kuhusu imani ya ambao
msingi wao ni imara? Haitaanguka chini kamwe, hata ikitikiswa kiasi gani
haitaanguka chini. Mungu alituambia sisi kuwa nyumba iliyojengwa katika mwamba
wa kweli uliofumwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, nyekundu na kitani safi ya
kusokotwa haitaanguka chini kamwe. Na kwa kweli hivi ndivyo ilivyo. Je, imani
ya mwamba ni nini? Ni imani inayo amini ukweli wa nyuzi za bluu, zambarau,
nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa. Imani ya watu waliojenga nyumba za jinsi
hiyo za kiimani hazitaanguka kamwe. Na hii ndiyo sababu ni muhimu kwa imani
yetu kuwa na msingi imara. Ikiwa hatuamini hata bila ya kufahamu vizuri yale
ambayo Bwana amefanya kwa ajili yetu, basi imani ya jinsi hiyo itageuka kuwa
imani ya kidini za uongo isiyotakiwa na Mungu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni