Kuna nafsi
tatu za utatu mtakatifu, kwa maneno mengine Mungu ni yule yule.
Tuangalie maandiko
yanasema nini kuhusu utatu mtakatifu
Agano la kale.
Ø Kwanza kabisa, katika Agano la kale
tunaona kuwa Mungu ni moja: “Sikiliza ewe Israel, Bwana Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja”(Kumbukumbu la Torati 6:4).
Ø Agano la kale pia linaeleza kuhusu
nafsi mbalimbali (utatu mtakatifu) “Kisha Mungu akasema, ‘tufanye mtu kwa mafano wetu, kwa
sura yetu” (Mwanzo 1:26) “Haya na tushuke
huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao.” (Mwanzo 11:7). Vifungu hivi vinadhihirisha kuwa Mungu
yupo katika nafsi nyingi.
Agano jipya.
Ø Nafsi tatu (utatu mtakatifu)
unajifunua katika ubatizo wa Yesu Kristo ambao ndio mwanzo wa huduma zake. “Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka
majini, na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama
hua, akija juu yake, na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, huyu ni
mwanangu, mpendwa wangu, ninayepenzwa naye” (Mathayo
3:16-17). Kifungu hicho hapo juu
kinaeleza utatu mtakatifu uliofunuliwa katika ubatizo wa Yesu uliofanywa na
Yohana Mbatizaji. Katika kifungu hiki tunajua ya kuwa Yesu ni mwana wa Mungu,
ambaye Roho Mtakatifu anafanya kazi pamoja nae. Ambaye kwa Mungu ni mwanae
mpendwa aliye pendezwa nae. Kupitia ishara hii, utatu mtakatifu wa Mungu
unajifunua. Yesu aliweza kukamilisha haki yote ya Mungu kwa sababu alichukua
dhambi za mwanadamu kupitia ubatizo alioupata kupitia kwa Yohana mbatizaji. Kwa
sababu ya ubatizo ilimpasa Yesu kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu, na hii
ndio “haki ya Mungu” ambayo baba
aliikamilisha kupitia mwanae Yesu. Kwamba Yesu alibeba dhambi zetu kupitia
tendo kuu la ubatizo na hiyo ndiyo haki ya Mungu, na ukweli huu umethibitishwa
na Baba na Roho mtakatifu. Hivyo Baba, Mwana Roho mtakatifu wamejifunua katika
nafsi tofauti, lakini Mungu ni yule yule.
Ø (Mathayo 28:19) “ basi, enendeni mkawafanye, mataifa yote kuwa wanafunzi,
mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho mtakatifu”. Pia
inadhihirisha kwamba Baba, Mwana na Roho mtakatifu kila mmoja ni nafsi
inayojitegemea, lakini kwa wakati huo huo wote ni wa moja kwani ni Mungu yule
yule mmoja. Tunapomwamini Mungu, twamwamini Mungu mmoja aliyeunganishwa na
nafsi tatu. Mungu Baba, Mwana na Roho mtakatifu kama Imani ya Kikristo
inavyokiri ni Mungu aliyepo tofauti kabisa na Miungu wengine. Dini zingine
zinaamini kuwa Yesu ni nafsi moja kati ya manabii wengi, lakini hii sio sahihi.
Ø Kwetu sisi Mungu ni Baba na Mwana na
Roho Mtakatifu. Licha ya ukweli kuwa ukweli huu umetosheleza na kupimwa na
maandiko, kuna wengi ambao bado hawatambui hili. Hii ni kwa sababu wale
wasiojua Injili ya maji na Roho wanadhania utatu mtakatifu kibinadamu ambayo
huwafanya wasielewe. Wale ambao bado hawajazaliwa upya hawawezi kuelewa utatu
na Roho mtakatifu ni Mungu mmoja kwetu, kwake ambaye tunaiweka Imani yetu kwa
uthabiti.
Asili ya Utatu wa Yesu
Kristo:
Yesu Kristo
amekuwepo kabla ya uumbaji na amekuwepo kama Mungu kweli na miele. Japokuwa alikuja
duniani kama mwandamu, ameendelea kuwa Mungu (Yohana
1:1, 14) kama vile (warumi 9:5) inasomeka
“Ambao mababu
ni wao, na katika wao alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili, ndie aliye juu ya
mambo yote, Mungu mwenye kuhimidiwa milele, Amina”. Ukiri wa kanisa la Mungu kuhusu asili ya Yesu
Kristo haujatungwa na wanadamu, umepatikana kutoka ufunuo wa Mungu mwenyewe (Mathayo 16:17) zaidi sana ukweli uliomo katika
Biblia unaelza asili ya ukuu wa Kristo (Isaya
9:6,Mika 5:2). Katika Agano Jipya, ukuu wa kweli wa Kristo mwokozi
umefanuliwa na kuthibitishwa na Kristo mwenyewe. Petro alikiri pia kuwa Yesu “wewe
ni Kristo Mwana wa Mungu aliye hai” (Mathayo 16:16,
Marko 8:29 na Luka 9:20). Zaidi ya hapo, Paulo alisema “ ambaye, yeye
mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu.” (Wafilipi
2:6).Yohana alipokuwa akimtukuza Kristo, naye alikiri. “Nasi twajua ya
kuwa mwana wa Mungu amekwishakuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye
wa kweli nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani ndani ya Mwana wake Yesu
Kristo. Huyu ndiye mwana wa Kweli na uzima wa milele.” (1
Yohana 5:20).
Nabii mkuu
alipomuuliza Yesu “tuambie kama wewe ni Kristo Mwana wa Mungu”Yesu akasema “wewe wasema” (Mathayo 26:63-64, na
Marko 15:2).Katika matukio mengine Yesu alisema yeye na Mungu ni wa -
moja (Yohana 10:30) na kuwa yeye alikuwepo
hata kabla ya Abraham (Yohana 8:58). Kristo
alielezea nafsi yake kama nabii mkuu wa utukufu ambao yeye alishirikiana na
Baba hata kabla ya uumbaji (Yohana 17:5). Pia
tunaona, pale Kristo aliposamehe watu dhambi zao au kuponya magonjwa yao na
pale alipowahimiza wanafunzi wake kumwamini yeye, haya yote yalifungua njia ya
kuufahamu ukuu wa Mungu.
Asili Ya Kibinadamu Ya Yesu
Kristo:
Agano Jipya
pia linaeleza ubinadamu wa Yesu. Mwana wa pekee wa Mungu alizaliwa “kwa mfano wa
Mwanadamu” (Wafilipi 2:7-8) aliitwa “Mwanadamu Yesu Kristo” (1 Timotheo 2:5) licha ya kuwa alikuwa Mungu
mwenyewe, alijinyenyekeza na kuwa kama Mwanadamu na Akakaa kwetu (Yohana 1:14). Matokeo yake alibatizwa na Yohana
mbatizaji. Akakaa kati ya watu kama mtu, na akashiriki furaha yao na huzuni
zao. Pia alikula chakula kile kile kama wanadamu wengine. Yeye alikuwa mtu si
tu kwa mwonekanao, bali tabia yake pia. Kama wengine, yeye pia alikuwa wa uzao
wa Adamu (Luka 3:38) pia alizaliwa na
Mwanamke (Luka 2:6-7) (Mathayo 11:18-25) na (wagalatia 4:4) mojawapo ya mababu zake ni
Abrahamu na Daudi (Mathayo 1:1). Licha
ya kuwa Yesu mwenyewe hakuwa na dhambi alikuja hapa duniani katika mwili wa
nyama ambao Mwanadamu ameudhoofisha kwa dhambi. Kwa maneno mengine Kristo
alikuja kwa namna ya mwili wenye dhambi na kwa kubatizwa na Yohana alitimiza
haki yote ya Mungu (Yohana 19:30). licha ya
kuwa alibeba dhambi zetu mabegani mwake na ubatizo pamoja na mateso aliyopata, hakutofautishwa
na wengine (Isaya 53:2-3). Licha ya kuwa
Kristo alikuwa na asili yetu hakuthubutu kuingia katika majaribu ya kutenda
dhambi kutokana na mwandishi wa kitabu cha Waebrania, Kristo alikuwa kwa namna
nyingi akijaribiwa kutenda dhambi kama sisi, lakini bila kutenda dhambi (Waebrania
4:15). Yesu alichukuwa dhambi za dunia kwa kubatizwa na Yohana na hii
ndio sababu alisulibishwa kwa ajili ya wenye dhambi. Tukirejea kwa Kristo, Waebrania 7:26 inasema, “kwa maana inatupasa sisi tuwe na Kuhani
mkuu wa namna hii aliye mtakatifu, asiye na uovu asiyekuwa na waa lolote,
aliyetengwa na wakosaji”.
Je, Yesu Alikuwa Mungu?
Ndiyo, Yesu
alikuwa Mungu mwenyewe. Yesu ndiye hasa aliyeumba dunia yote kwa neno la kimywa
chake. Kwa hakika dunia hii iliumbwa na Mungu Yohana
1:3 inasema “vitu vyote viliumbwa na yeye, na pasipo yeye hakuna chochote
kilichoumbwa kinaoonekana” Yesu
alikuwa Mungu mwenyewe aliyekuja kuwaokoa wakosaji. Yesu aliumba ulimwengu huu
kwanza. Pale aliposema “na iwe nuru”, mara
ikawa nuru. Aliposema “na liwepo jua”,
mara jua likatokeza. Ilikuwa ni amri tu “na
iwe” vyote majini, miti, bahari, anga, na hata wanadamu wakatokea. Yesu
Kristo aliumba kila kitu hapo
mwanzo (Mwanzo 1:3-15). Alikuwa ndiye Mungu mkuu wa
uumbaji. Yote yalifanyika kwake. Na hakuna chochote kilichokuwepo bila yeye.
Sasa ni kwa nini alikuja kwa mfano wa Mwanadamu? Alikuja kuokoa, wenye dhambi
wote wa dunia hii. Sababu kubwa ya kuja kama Mwanadamu ilikuwa ni kuleta nuru
ya kila mwenye dhambi na hatimaye kuwaokoa na dhambi zao. Yohana 1:9-12 inasema “kulikuweko na nuru halisi, amtiaye nuru
kila mtu, akija katika ulimwengu. Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye
ulimwengu ulipata kuwapo, wala ulimwengu haukumtambua alikuja kwake, wala walio
wake hawakumpokea bali waliompokea waliwapa uwezo kufanyika wana wa Mungu, ndio
wale waliaminio jina lake”. Mungu alikuja kuondoa dhambi za dunia
tulizorithi kutoka kwa Adamu, Baba wa wanadamu, na kuondoa giza kutoka duniani.
Jina lake yeye ni Yesu Kristo na Yesu Kristo ni mtoto wa Mungu Baba.
Utatu wa Mungu
WaKristo wanapaswa
kumjua Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu kama Mungu mmoja, na kukiri imani
kwa nafsi hizo zote? Ndiyo, sababu ni kama ifuatavyo: Mungu Baba, Mwana na Roho
Mtakatifu wote walishiriki huduma ya uumbaji na kumkomboa Mwanadamu. Lakini
Mungu Baba ni Baba wa Mwana mtakatifu. Mwana alitimiza huduma ya ondoleo la
dhambi, kwamba alibatizwa na Yohana, alisulubiwa, ili kumkomboa Mwanadamu
kutoka dhambini. Roho Mtakatifu alichukua nafasi ya kubeba ushuhuda wa wale
wanaoamini ubatizo wa Yesu ushuhuda kwa wale wanaoamini ubatizo wa Yesu na damu
yake msalabani kuwa vimetenda kazi ya kutakasa dhambi. Sisi kuwa watu kamili
kwa Mungu, tunahitaji kumwamini Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu kwa namna
hii. Ni kwa sababu Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu waliumba ulimwengu, na
sisi tuishio humu, na Mungu Mwana kuwaokoa wenye dhambi, ubatizo uliokamilisha
haki ya Mungu na kazi ya kumwaga damu pale msalabani ilihitajika. Kwa kuwa Yesu
alibatizwa na Yohana na hapo akachukua dhambi za dunia, alichukua adhabu ambayo
sisi tulistahili kuibeba na kufa msalabani badala yetu.
Kwa kufanya
hivyo, wenye dhambi hatimaye walipokea ondoleo la dhambi. Ukweli huu
uliandaliwa muda mrefu, na ndio msingi hasa wa huduma ya Injili ya maji na
Roho. Ni pale tunapoutumia ukweli huu ndipo kazi ya Yesu Kristo ya utakaso
inapotimilika kwa ajili yetu, na tunaweza kuokolewa kutoka dhambini kwa kuamini
tu. Kama tusingekuwa na ufahamu juu ya Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu,
hapo tusingeliweza kuujua ulimwengu ulivyoumbwa na nani aliyetupatia uzima, na
kusingekuwa na Mungu Mwana, tusingeweza kujua njia ya wokovu, dhambi zetu
zingepitishwa wapi? Msingi wa wokovu wetu ungekuwa nini. Na kama kusingekuwa na
ushuhuda wa Roho mtakatifu, hapo haijalishi ukubwa na njia ya wokovu
iliyoandaliwa, ukweli ungebaki kama alama tu mawinguni usio na lolote la
kufanya nasi. Kwa hiyo kila tunapokiri imani ya Mitume , ni lazima tumfikiri
Mungu Baba, Mungu Mwana na Roho Mtakatifu aliyetuumba na kutupa uzima na ni
lazima tuwe imara katika imani na kuamini kuwa nafsi hizi tatu ni Mungu pamoja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni