(1Yohana 5:4-7) Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda
ulimwengu; na huku ndiko kushinda
kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu. Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye
aaminiye ya kwamba Yesu ni mwana wa Mungu. Huyu ndiye aliye kuja kwa maji na
damu, Yesu Kristo: si katika maji tu, bali katika maji na katika damu. Naye
Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli.
Yatupasa kuamini kwamba Yesu
alichukua dhambi zetu zote kwa ubatizo wake, alihukumiwa na kufa msalabani kwa
ajili yetu, na akafufuka siku ya tatu, baada ya kifo chake.
Bila imani hii, ukombozi
usingewezekana. Yesu Kristo alikuja kwetu kwa ubatizo, damu na Roho. Alichukuwa
dhambi zote za ulimwengu.
Yapo mambo muhimu matatu yenye
kushuhudia juu ya wokovu wake hapa duniani, Roho, maji na damu.
Kwanza; ‘Roho mtakatifu’
hushuhudia Yesu ni Mungu na alikuja katika mwili.
Pili ; ‘Maji’ hushuhudia
ubatizo wa Yesu katika mto Yordani kwa Yohana Mbatizaji ambaye kupitia kwake
dhambi zetu zote alimtwika Yesu. Dhambi zetu alizibeba Yesu alipobatizwa (Mathayo 3:15).
Tatu; ‘Damu’ inasimama
kama Yesu kukubali kujitoa kwa hukumu ya dhambi zetu. Alikufa kwa hukumu ya Mungu
Baba na alifufuliwa siku ya tatu ili kutupa uhai mpya.
Mungu Baba alimtuma Roho ndani ya
mioyo ya wale wote wenye kuamini ubatizo na damu ya mwana wake ili aweze
kushuhudia ndani, juu ya ukombozi.
Wale wote waliozaliwa upya wana
neno ndani yao lenye kuushinda ulimwengu. Waliokombolewa watamshinda shetani,
uongo wa manabii, walaghai, vikwazo au misukosuko ya ulimwengu ambayo haiachi
kushambulia. Sababu ya kuwa na nguvu hii ni kwamba, tuna ushuhuda wa yale mambo
matatu ndani ya mioyo yetu; maji ya Yesu, Damu yake na Roho.
Haiwezekani kuzaliwa upya au
kuushinda ulimwengu ikiwa huna imani katika ukombozi utokanao na ubatizo wa
Yesu, damu yake na kuamini Yesu ni Mwana wa mungu na mwokozi. Katika (1Yohana 5:8) inasema
“kisha wako watatu washuhudiao duniani, Roho na
Maji na Damu na watatu hawa hupatana kwa habari moja.” Wengi bado
huzungumzia juu ya damu na Roho tu wakiacha maji ya ubatizo wa Yesu. Ikiwa
wataacha habari ya maji, bado wataendelea kudanganywa na shetani. Wanapaswa
kuacha upotovu wao na kutubu na kuamini maji ya ubatizo wa Yesu katika kuzaliwa
upya.
Hakuna yeyote mwenye kuushinda
ulimwengu bila kuamini maji na damu ya Yesu. Nasema tena, hakuna! Yatupasa
kupigana kwa kutumia maji na damu ya Yesu kama silaha nzito na kali za kiroho.
Neno lake ni upanga wa Roho, Nuru.
Wapo wengi wasioamini ubatizo wa
Yesu ulichukua dhambi zetu zote. Wapo wengi wenye kuamini mambo mawili tu.
Hivyo, Yesu anapowaeleza “amka na uangaze”, hawawezi kuangaza kwa vyovyote
vile. Bado wanazo dhambi mioyoni mwao. Ingawa wanamwamini Yesu, lakini bado
watakwenda motoni.
“mfano wa mambo hayo ni ubatizo
unaowaokoa ninyi pia siku hizi” (1Petro 3:21). “watu
wanane wliokoka kwa maji” (1Petro 3:20).
Ni watu wachache ndiyo waliokoka enzi za Nuhu. Je, walikuwa
ni wenye thamani zaidi ya wengine? Hata kidogo! Sisi sote si wenye thamani,
bali tumeokolewa kwa njia nyingine kupitia imani katika maji, damu na Roho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni