Ijumaa, 21 Februari 2014

KUTEMBEA KATIKA HAKI YA MUNNGU


(Warumi 8:12-16)  “Basi, kama ni hivyo, ndugu, tu wadeni, si wa mwili tuishi kwa kufuata mambo ya mwili, kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi. Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu. Kwa kuwa hamkupokea tena roho ya utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba , yaani Baba. Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na Roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu”
Mtume Paulo, kama mtu aliyepokea wokovu toka kwa Mungu alisema kuwa wale waliozaliwa tena upya hawapaswi kuishi kwa jinsi ya mwili bali kwa jinsi ya Roho. Hasahasa Paulo alisema ikiwa sisi ambao tunayo haki ya Mungu tutaishi kwa jinsi ya mwili basi tutakufa, na kwamba kama tutaishi kwa jinsi ya Roho basi tutaishi. Hivyo ni lazima tuamini katika ukweli huu. Je, inakuwaje basi kwa wale wanaoamini katika haki ya Mungu? Je, wanapaswa kuishi kwa mujibu wa haki ya Mungu au kwa tama ya mwili? Ni lazima  watambue kile kilicho sahihi na kisha waiadabishe miili yao na kujitoa kwa kazi za haki ya Mungu.
“ kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndiyo wana wa Mungu(Warumi 8:14) wale wanaoamini katika haki ya Mungu (kuijua haki ya Mungu soma masomo yaliyopita) wanapokea Roho mtakatifu anawaongoza. Hawa ni “wana wa Mungu” wana Roho Mtakatifu anayekaa ndani yao. Kwa hiyo, wale wasio na Roho Mtakatifu ndani yao basi hao si wa Mungu. Mahali pa kuanzia  kumfuata Mungu ni katika kuamini haki yake. Kufanyika mtoto wa Mungu kunaanza kwa kuamini katika neno la injiri ya maji na Roho. Kwa maneno mengine, kufanyika mtoto wa Mungu kunaanza kwa kuamini katika injiri ya haki yake. Hii ina maanisha kuwa unafanyika kuwa mwana familia ya Mungu kwa kuamini katika haki yake na kwamba Mungu ametoa haki yake ili kukuokoa toka katika dhambi.
Yesu alisema kuwa yeye ambaye hajazaliwa kwa maji na Roho hawezi kufahamu maana ya kuzaliwa tena upya. Imani katika ubatizo wa Yesu alioupokea toka kwa Yohana Mbatizaji na damu yake aliyomwaga msalabani inawawezesha wote wanaoamini katika tendo lake la haki kupokea haki ya Mungu.
Hivyo ndugu ninakusihi, jitahidi sana uijue haki ya Mungu iletayo wokovu, soma katika blog hii somo lililo andikwa “ injili ya maji na Roho”


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni