sheria sehemu ya tano
Mtume Paulo alisema kwamba, Mungu ametupatia haki kwa imani
toka mwanzo. Alimpatia Adamu na Hawa, Kaini na Abeli, Sethi na Enoki, Nuhu,
Abrahamu, Isaka na mwisho Yakobo na watoto wake kumi na wawili. Hata pasipo
sheria, walifanywa kuwa wenye haki mbele za Mungu kupitia haki itokanayo na Imani
ya Neno lake; Walibarikiwa na walipata pumziko kupitia imani ya Neno lake.
Muda uliopita wakati uzao wa Yakobo uliishi Misri kama
watumwa kwa miaka 400 kwa sababu ya Yusufu. Ndipo Mungu alipowaongoza kutoka
kupitia Musa kuelekea Kanaani, pamoja na kuwa watumwa kwa miaka 400, walisahau
haki katika Imani.
Ndipo Mungu alipowaongoza kupita kati ya Bahari ya Shamu kwa
muujiza na kuwaongoza jangwani walipofika jangwa la dhambi, akawapa sheria
katika Mlima Sinai. Aliwapa sheria ambazo zilikuwamo Amri kumi na vipengele
613. Mungu aliahidi “Ndimi Bwana Mungu wako, Mungu wa Abraham, Mungu wa Isaka,
Mungu wa Yakobo, Musa apande na kuja katika mlima Sinai na nitawapa sheria”
Ndipo alipowapa Waisraeli Sheria.
Aliwapa Sheria ili waweze “kutambua dhambi” (Warumi 3:20) Ilikuwa ni kuwafahamisha juu ya
anachotaka na asichotaka na kuweka wazi haki yake na utakatifu.Walipokuwa
wakiishi kama watumwa kwa kipindi hicho cha miaka 400, walisahau haki ya Mungu
katika muda huo hawakuweza kuwa na kiongozi. Yakobo na Yusufu walikuwa viongozi
hapo awali. Inaonekana Yusufu alishindwa kuirithisha Imani hiyo kwa watoto wake
wa kiume, Manase na Efraimu.
Hivyo, walihitaji
kumtafuta Mungu tena na kukutana naye kwa kuwa waliisahau haki yake. Tunapaswa
kuweka akilini kwamba Mungu aliwapa haki kwa imani mwanzo na kuwapa sheria
baada ya kuisahau Imani. Aliwapa Sheria ili waweze kumrudia.
Kuiokoa Israeli na kuwafanya kuwa wana wake, aliwaambia
kwamba iliwalazimu kutahiriwa. Nia ya kuwaita ilikuwa ni kuwafanya watambue
kwamba alikuwa kati yao ili kuanzisha Sheria na pili, kufanya watambue walikuwa
ni wenye dhambi mbele zake. Mungu alitaka waje mbele zake na kuwa watu wake kwa
kukombolewa kwa mfumo wa sadaka ambayo aliyokuwa amewapa. Na aliwafanya kuwa
watu wake.
Wana wa Israeli walikombolewa kupitia mfumo wa sadaka wa
Sheria kwa kumwamini Masiya ajaye. Lakini mfumo huu ulipitwa na wakati. Na
tuangalie hii, ilikuwa ni lini. Katika Luka 10:25 mwanasheria mmoja alitajwa kumjaribu
Yesu. Alikuwa ni Mfarisayo. Mafarisayo walikuwa ni wenye kuyashika mafundisho
bila kukubali kubadilika kwa kufanya jitihada zao binafsi kuishi kwa kufuata
neno la Mungu; Walijaribu kuzilinda sheria za nchi kwanza kwa kuishi kadiri ya
maandiko ya sheria. Walikuwa ni “wakereketwa” (kwa lugha ya kisasa) ambao
walihamasisha na kufanya ghasia za kuvunja sheria ili kufanikisha malengo ya
maono yao juu ya uhuru wa Waisraeli toka kwa Warumi.
Kuna baadhi yao hata nyakati hizi wamo kwenye dini
tuzionazo. Huongoza harakati za kijamii kwa usemi kama vile “Okoa
wanaogandamizwa duniani!” Huamini Yesu alikuja kuokoa maskini na
wanaogandamizwa. Hivyo baada ya kujifunza theologia katika seminari, huchukua
nafasi katika mambo ya kisiasa na kujaribu kuwakomboa wanaonyanyaswa katika
kila sehemu ya jamii. Ndiyo wenye kushinikiza kwa kusema “Hebu na tuishi kwa
sheria na rehema ya sheria takatifu. Tuishi kwa sheria, kwa neno la Mungu”
Lakini hawatambui hakika ya ukweli wa Sheria. Hujaribu kuishi kwa sheria iliyoandikwa bila kufahamu na kupata ufunuo
wa Mungu juu ya Sheria hiyo.
Kwa maana hiyo tunaweza kusema kwamba hapakuwepo na manabii,
watumishi wa Mungu katika Israeli kwa kipindi hicho cha miaka 400 kabla ya
Kristo. Kwa sababu hii basi, walikuwa ni kundi la kondoo wasio na Mchungaji.
Hawakuwa na sheria wala Kiongozi wa kweli. Mungu
hakujidhihirisha mwenyewe kwa hao walio kuwa ni viongozi wa dini zao walio
wanafiki. Nchi ilitawaliwa na Dola ya Warumi. Hivyo Yesu aliwaambia watu hawa
wa Israeli walio mfuata jangwani kwamba hawatarudishwa kutoka kwake wakiwa na
njaa. Alijawa na huruma juu yao waliokama kundi la wanakondoo wasio na
Mchungaji kwani wengi wao walikuwa kwenye mateso makubwa.
Wanasheria na wale wengine walio na nafasi za uongozi
walikuwa ndiyo wenyewe tu wenye kunufaika. Mafarisayo walikuwa ni kizazi cha “Judaism”
na walikuwa ni wenye majivuno sana.
Mwanasheria huyu alimwuliza Yesu katika Luka 10:25“nifanye nini niweze kurithi uzima wa milele?” Alionekana
kufikiri kwamba yeye ni bora zaidi kati ya watu wa Israeli. Hivyo mwanasheria
huyu (ambaye hajakombolewa) alimwuliza Yesu kwa kusema “nifanye nini nipate
kuurithi uzima wa milele?”
Mwanasheria huyu anasimama badala yetu leo. Alimwuliza Yesu
swali hili, naye akajibu “imeandikwa nini katika Torati? Wasomaje?” Naye
akajibu “mpende
Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako
zote na akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.” Naye akamjibu umejibu
vema; fanya hivi nawe utaishi.” Alijaribu kumtia changamoto Yesu bila ya
kufahamu yeye alikuwa ni mwenye dhambi, asiyeweza kutenda mema. Hivyo Yesu
alivyomwuliza “imeandikwa nini katika Torati, wasomaje?”
“wasomaje” kwa kifungu hiki Yesu anauliza, ni kwa namna gani
mimi na wewe tunaijua na kuielewa sheria? Kwa jinsi hii wengi wetu nyakati hizi
ndivyo tulivyo. Mwanasheria huyu alifikiri kwamba Mungu alikusudia kuweka
sheria ili zifuatwe. Hivyo alijibu kupitia maandiko “mpende Bwana Mungu wako
kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote na kwa akili
zako zote na jirani yako kama nafsi yako.” Sheria haikuwa na kasoro. Alitupa
sheria iliyo kamilifu. Alituambia tumpende Bwana kwa moyo na kwa roho na kwa
nguvu na akili na kuwapenda majirani zetu kama nafsi zetu. Ni haki tumpende
Mungu kwa moyo wetu wote na kwa nguvu zetu zote, lakini hii ni amri takatifu
isiyoweza kutimizwa kwa nafsi zetu. “Wasomaje?” Hii ina maana sheria ni
kamilifu na sawa lakini je, wewe unaelewa nini juu yake? Mwanasheria alifikiri
kwamba Mungu alileta sheria hii ili aweze kuitii. Ingawa Sheria ya Mungu
imeletwa kwetu ili tuweze kuziona nafsi zetu na upungufu ndani yake kwa
kuukubali udhaifu wetu uliowazi kabisa mbele za Mungu. “Umetenda dhambi, umeua
hali nilikuambia usiue. Kwa nini hukunitii” Ndivyo Mungu akuulizavyo. Sheria
huweka wazi dhambi za watu ndani ya mioyo yao. Hebu na tufikiri kwa mfano
nilipokuwa nikitembea, nikaona tunda zuri na tamu lililoiva katika shamba la
mtu. Mungu amenionya kwa sheria” usichume tunda hilo katika shamba.
Itaniaibisha mimi ukitenda hilo” “Ndiyo Baba” “Shamba hili ni la ndugu fulani,
hivyo usichume” “Ndiyo Baba” Tunaposikia hivyo tusichume, tunahisi msukumo
ndani yetu wa kuchuma. Tunapochukua hatua ya kujizuia inashindikana. Na hii
ndivyo ilivyo katika dhambi za watu. Mungu ametuonya tusitende dhambi. Aweza
kusema hivi kwa kuwa yeye ni mtakatifu, mkamilifu na mwenye uwezo wote.
soma shehemu ya sita " SHERIA NI KWA AJILI YA KUZIFAHAMU DHAMBI"
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni