Jumapili, 23 Februari 2014

WENYE KUJARIBU KUKOMBOLEWA KWA KUPITIA MATENDO YAO BADO NI WENYE DHAMBI.

sehemu ya nne
Hebu na tusome Wagalatia 3:10 na 11“Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana: maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati, ayafanye". Ni dhahiri ya kwamba kwa sababu Mwenye haki ataishi kwa Imani”kuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria; 
Imesemwa “Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati ayafanye “Wale wenye kufikiri kuwa wana mwamini Yesu, hali wakitaka haki kupitia matendo yao, wamelaaniwa. Wapo wapi wenye kujaribu kuwa wenye haki? Wapo chini ya laana ya Mungu.

Kwa nini Mungu ametupa Sheria? Ametupa sheria ili tuweze kuzitambua dhambi zetu (Warumi 3:20). Na pia alitaka tujue kwamba sisi ni wenye dhambi na mwisho wetu ni jehanamu. Amini ubatizo wa Yesu, Mwana wa Mungu na uzaliwe upya kwa maji na kwa Roho. Ndipo utakapo okolewa dhambini, kuwa mwenye haki, kupata uzima wa milele na kwenda mbinguni. Uwe na Imani moyoni mwako.

soma sehemu ya tano "MUNGU AMETUPATIA HAKI KWA IMANI KATIKA SHERIA"

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni