Jumapili, 23 Februari 2014

SHERIA NI KWA AJILI YA KUZIFAHAMU DHAMBI

sheria sehemu ya sita
Katika Warumi 3:20 tunasoma “ Kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria”. Mwanzo kabisa nilichukulia kifungu hiki kuwa ujumbe binafsi kwa Mtume Paulo na kuamini maneno niliyopendelea. Lakini baada ya machozi yangu kukauka hakika sikuweza kuendelea na maisha yangu ya imani ya kidini. Hivyo niliendelea na dhambi na kufikia hatua ya kugundua nina dhambi ndani ya moyo wangu na kushindwa kuishi kwa sheria. Sikuweza kuvumilia ingawa sikuweza kuachana na sheria kwa kuwa niliamini ilikuwepo ili niweze kuitii. Hatima yake nikawa mwanasheria kama walionyeshwa katika maandiko hapo awali. Ikawa ni vigumu kwangu kuendelea na maisha ya imani.
Nilikua na dhambi nyingi hata kufikia kila ninapo soma sheria naanza kugundua dhambi hizo kila ninapozivunja amri 10 ndani ya moyo wangu. Ikumbukwe kuwa na dhambi moyoni ni sawa kutenda dhambi tu! Sikuweza kufahamu kwamba nilikuwa tayari muumini wa sheria.
Nilipofuata sheria nilifarijika. Lakini nilipoanguka nilikua mnyonge, mwenye hasira na huzuni. Na wakati huo nikawa mwenye kukosa matumini kwa yote. Ingeweza kuwa rahisi ikiwa hapo awali ningefundishwa ukweli juu ya sheria kama vile “Hapana, siyo hivi! Ipo maana nyingine ya sheria nayo ni kama taa kuonyesha dhambi zako kama vile wewe unapenda fedha, kupenda jinsia tofauti na vitu vizuri vya kuonekana.Una vitu unavyovipenda kuliko umpendavyo Mungu. Unapenda sana kufuata mambo ya dunia. Sheria iliwekwa kwako si uifuate bali uweze kugundua nafsi yako kama mwenye dhambi aliye na uovu moyoni”.
Ikiwa mtu yoyote angeweza kunifundisha hivi basi nisingeweza kuteseka kwa muda mrefu namna ile. Hivi ndivyo nilivyo weza kuishi kwa sheria kwa miaka mingi kabla ya kuja kugundua hili. Amri ya nne inasema “Ikumbuke siku ya Sabato na uitakase”. Hii ina maana kwamba tusifanye kazi siku ya jumamosi.Tunafundishwa tusifanye kazi, sio kutembea mwendo wa mbali katika safari kwa siku ya Jumamosi.Nilidhani ilikuwa ni sahihi na niheshima kutembea sehemu nilizo hitaji kuhubiri. Hata hivyo nilitaka kuhubiri sheria. Na nilihisi ilinipasa kutenda yale nihubiriyo. Ikawa ni vigumu na kushindwa. Kama ilivyo hapo mwanzo”wasoma je?” sikuelewa swali hili na kuteseka miaka mingi. mwanasheria hakuelewa vema hili.Alifikiri ya kwamba ikiwa ataheshimu sheria na kuishi kwa uangalifu mkubwa atakuwa amebarikiwa na Mungu.
Lakini Yesu alimwambia “wasomaje?”. Naye akajibu kwa imani itokanayo na sheria. Naye akamjibu “umejibu vema, unaichukua kama ilivyoandikwa. Jaribu kuifuata. Utaishi ikiwa utaweza na utakufa ukishindwa.Mshahara wa dhambi ni mauti.Hakika ukishindwa utakufa” ( kinyume cha kuishi ni kufa,sivyo?). lakini mwanasheria huyu hakugundua hili. Mwanasheria ni mfano wetu sisi leo, mimi na wewe. Nilijifunza theologia (elimu ya dini) kwa miaka mingi. Nilijaribu kila namna, kusoma kila kitu na kutenda kila jambo; kufunga kula, kuwa na maono, kunena kwa lugha……. Nilisoma Biblia kwa miaka mingi kwa kutegemea nitahitimisha jambo fulani mbeleni. Lakini kiroho nilikuwa bado kipofu!
Na ndiyo maana mwenye dhambi huitaji mtu fulani atakayefungua macho yake, na huyu ni Bwana wetu Yesu Kristo. Ndipo mtu hugundua “Ahaa! Hatuna uwezo wa kufuata sheria. Haijalishi ni kwa bidii gani tutaweza kujaribu kuifuata tutaishia kufa tukikosa matumaini. Lakini Yesu alikuja kutuokoa kwa maji na kwa Roho! Haleluya!” Kwa maji na kwa Roho tutaweza kukombolewa. Ni neema, zawadi ya Mungu. Na tumsifu Bwana. Nilikuwa mwenye bahati ya pekee kuhitimu toka kwenye njia ya kukosa matumaini katika sheria, naamini wengi huchukua muda mrefu zaidi katika maisha yao kusoma theologia katika njia panda na bila kugundua ukweli hadi umauti. Wengine huamini kwa mioyo mingi, kizazi hadi kizazi na hawazaliwi upya.
Tunahitimu kutokuwa wadhambi pale tu tunapogundua hatuna uwezo wa aina yeyote binafsi wa kufuata sheria na kusimama mbele ya Yesu kwa kukubali kuisikiliza Injili ya maji na Roho. Tunapokutana na Yesu tunahitimu kutoka kwenye hukumu na jehanamu. Sisi ni wenye wingi wa dhambi, lakini tunafanyizwa haki kwa sababu Yesu ametuokoa katika maji na damu yake. Yesu amesema hatuwezi kuishi katika mapenzi yake. Alimwambia mwanasheria, lakini hakuelewa hili. Hivyo alimpa mfano huu.
 “Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang`anyi; wakamvua nguo, wakamtia jeraha wakaenda zao,wakamwacha karibu kufa(Luka 10:30) Yesu alimpa Mwanasheria mfano huu ili kuamsha dhamira yake kwakua huteseka kwa maisha yake yote kama jinsi Mtu yule aliyepigwa na wanyang`anyi karibu kufa.
Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko. Yeriko inawakilisha dunia hii ya sasa, hali Yerusalemu inawakilisha mji wa kidini, mji wa imani uliojawa na majigambo ya sheria. Mfano huu hutuelezea ikiwa tutamwani Kristo kwa njia ya udini tutaangamia.
“ Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko akangukia kati ya wanyang`anyi, wakamvua nguo wakamtia jeraha wakenda zao wakimwacha karibu kufa”. Yerusalemu ulikuwa ni mji mkubwa ukiwa na wakazi wengi. Kulikuwa na Kuhani Mkuu, Jeshi la Makuhani Walawi na wengi wa Wakuu mashuhuri wa dini. Palikuwepo na wengi wenye kuelewa sheria vema. Na walijaribu kuishi kwa sheria, lakini walishindwa na kukimbilia Yeriko wakangukia duniani ( Yeriko ) na kushindwa kuzuia kukutana na wanyang`anyi
Mtu huyu pia alikutana njiani na wanyang`anyi toka Yerusalemu kwenda Yeriko wakamvua nguo. “Kuvuliwa nguo” maana yake kupoteza haki. Ni vigumu kwetu kuishi kwa kufuata sheria, kuishi kwa sheria Mtume Paulo amesema katika Warumi 7:19-20 “Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi, bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo. Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilipendalo si mimi nafsi yangu nilitendalo, bali ni ile dhamiri ikaayo ndani yangu”.
Ningetamani kutenda mema na kuishi katika Neno lake Mungu. Lakini ndani ya moyo wa mwanadamu umefurika mawazo mabaya, uasherati,wivi, uuaji, unzizi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu ( Marko 7: 21-23 ).Kwa kuwa haya ndiyo yaliyomo ndani ya mioyo yetu, basi tunafanya yale tusiyopaswa na hatufanyi yale yatupasayo kufanya. Tunaendelea kurudia maovu haya ndani ya mioyo yetu. Hivyo shetani huitaji kukuhamasisha kwa kiasi kidogo tu ili uweze kutenda dhambi.
Alikutana na nani njiani alipokuwa akienda Yeriko? Alikutana na wanyang’anyi. Yeyote yule asiyetambua na kuishi kwa sheria, maisha yake yanafananishwa na mbwa aliyetelekezwa. Hula na kunywa na kwenda haja mahala popote. Mbwa wa aina hii huamka asubuhi nyingine na kwenda haja na kula tena. Huweza hata kula kinyesi chake.
Ndiyo maana mtu huyu hufananishwa na mbwa. Hula na kunywa na kwenda haja lakini huomba toba asubuhi inayofuata na kurudia yale yale kwa mara zote. Ni sawa na mtu aliyekutana na wanyang’anyi akienda Yeriko. Akaachwa akiwa amejeruhiwa karibu ya kifo. Ina maana kwamba kuna dhambi ndani ya moyo. Na hii ndivyo ilivyo kwa mwanadamu.
Watu humwamini Yesu na kujaribu kuishi kwa sheria katika Yerusalemu, jamii ya dini, lakini wanaachwa na dhambi ndani ya mioyo yao. Kile wanachoweza kuonyesha katika maisha yao ya udini ni majeraha ya dhambi. Wale wenye dhambi mioyoni mwao hakika siku za mwisho watakwenda motoni. Wanajua hili, lakini hawajui lakufanya. Je ni kweli hata wewe upo katika mji huo wa dini? Ndiyo. Hata sisi tulikuwepo.
Mwanasheria aliyeshindwa kuielewa sheria ya Mungu angehangaika maishani pote, lakini angeishia motoni kwa majeraha. Ni sisi kati yetu, mimi na wewe. Yesu pekee aokoa. Wapo watu wengi wenye uerevu kati yetu na kila mara kupayuka wanayoyajua. Wote hawa hujifanya kwa kuishi katika sheria ya Mungu na hawapo kweli nafsini mwao. Hawawezi kuita beleshi kuwa ni beleshi, mara zote huzificha nafsi zao kwa nje ili kuonekana waaminifu.
Kati yao ni wenye dhambi kuelekea Yeriko, wale waliopigwa na waovu na kuachwa karibu kufa. Tunapaswa kuelewa vile tusivyo imara, wepesi wa kuumizwa mbele za Mungu. Yatupasa tukiri mbele zake “Bwana, hakika nitaishia motoni ikiwa hutoniokoa. Naomba uniokoe. Nitakufuata popote, ikiwa ni penye kimbunga au dhoruba, ikiwa tu nitaweza kusikia Injili. Ukiniacha peke yangu, nitakwenda motoni. Nakusihi niokoe!”

Wale wenye kugundua kuwa wapo karibu na jehanamu na kujaribu kutenda matendo ya kujitafutia haki wakiwa wanaambatana na Bwana ndiyo pekee watakaookolewa. Hatuwezi kuokolewa kwa juhudi zetu binafsi. Yatupasa kuelewa kwamba, tutafananishwa na mtu yule aliye angukia katika mikono ya wanyang’anyi.
kumbuka
mwenye haki hatendi dhambi makusudi kwa sababu ana Roho wa mungu soma katika blog hii "injili ya maji na roho."

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni