Baadhi ya
wakristo hawaamini haki ya Mungu na humsifu Bwana wakiimba “Oh, Mungu chukuwa
kilicho changu na ufanye kuwa chako, matendo yangu ya kujitolea mbele yako” kwa
njia hii Mungu hana nafasi ya kufanya chochote kwako.
Wanadamu humchosha
Mungu kwa kujifanya wao ni wa kujitolea matendo yao zaidi. Mungu amechoshwa na
upofu huu wa kujitolea kwa sadaka ya matendo. Wao humsihi Mungu apokee haki zao
za kibinadamu ( ukitaka kujua haki ya Mungu soma “injili
ya maji na roho” katika blog hii). Hudumu waki mlilia Bwana ‘ O, Mungu! Pokea
kujitoa kwetu sadaka” huku wakitenda kazi za kanisa kama vile kufagia, kudeki
sakafu, kufanya maombi, na kuimba mapambio. Itatia dosari kwa wakristo wengi. Siku
hizi wakristo wengi humsihi Yesu kuyajali matendo yao ya kujitolea kimwili huku
hawaijui haki ya Mungu au hata kuiamini. Yatupasa kuacha kujitolea kimwili na
kuanza kuikubali na kuielewa haki ya Mungu ambayo
ndani yake umo ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani.
Tusome
habari ya Kornelio katika kitabu cha Matendo 10, ili ujue namaanisha nini? (Matendo 10:1-6) Palikuwa na mtu kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa
kikosi kilichoitwa kiitalia, mtu mtawa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake
yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu daima. Akaona katika
maono waziwazi, kama saa tisa ya mchana, malaika wa Mungu, akimjia na
kumwambia, Kornelio! Akamtazama sana, akaogopa akasema, kuna nini, Bwana? Akamwambia,
sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu. Sasa basi,
peleka watu Yafa, ukamwite Simoni, aitwaye Petro. Yeye ni mgeni wa mtu mmoja, jina lake Simoni,
mtengenezaji wa ngozi, ambaye nyumba yake iko pwani, atakuambia yakupasayo kutenda”
Neno “atakuambia yakupasayo kutenda” maana yake yale
aliyo kuwa akitenda hayakuwa na msaada wowote kuipata haki ya Mungu (yaani
kupata msamaha wa dhambi), ili kuzaliwa upya na kupokea Roho Mtakatifu. Ni sawa
na mtu masikini na omba omba kumpa tajiri bilionea kila alichonacho na kumba akae katika makazi ya kifahari kwa
fidia ya kile alichotoa. Mungu haitaji
kwetu kujitia sifa ya haki zetu binafsi. Mungu anahitaji tuwe na imani kwa kuamini
ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani.
Tuendelee na
habari hii ya Kornelio katika (Matendo 10:37) Jambo lile ninyi
mmelijua, lililoenea katika Uyahudi wote likianzia galilaya, baada ya ubatizo aliouhubiri Yohana.
Baada ya
kuambiwa na malaika atume watu Yafa wakamwite Simioni, alipofika alianza
kuhubairi habari ya ubatizo. Kwanini Simioni alianzia katika ubatizo?, jibu
unalipata katika kifungu hiki (Matendo10: 43) “huyo manabii wote humshuhudia, ya kwamba kwa jina lake kila
amwaminiye atapata ondoleo la dhambi” ukisha
pokea ondoleo la dhambi nini kinachofuata? (Matendo
10:44) Petro
alipokuwa akisema maneno hayo Roho Mtakatifu akawashukia wote waloisikia lile
neno”
Tunapokea ondoleo
la dhambi ikiwa pale tutakapo amini ubatizo wa Yesu kwa Yohana na damu yake
msalabani( ufafanuzi wa somo hili soma matoleo yaliyopita).Yesu alibatizwa ili
kubeba dhambi zote za dunia na kufa ili ili kuzifuta dhambi hizo mara moja na
kwa wakati wote.
Hivyo mtu anapohubiriwa
kwa usahihi neno la Mungu anapokea ondoleo la dhambi na kupokea Roho Mtakatifu.
Je tusifanye kazi za kujitolea katika makanisa? Hapana. Namaanisha si njia ya
kumpokea Roho Mtakatifu (kuzaliwa mara ya pili).
Tuendelee na
habari ya Kornelio (Matendo10: 47) Ni nani awezaye kuzuia maji, hawa wasibatizwe, watu waliopokea
roho mtakatifu kama sisi?
Utaona kwamba
ubatizo katika maji ni hatuwa ya mwisho, kama ishara ya nje ya kile
ulichokiamini ndani yako, Hivyo Roho Mtakatifu huja kabla ya kwenda katika maji
ya ubatizo.
Hebu tafakari
maandiko haya; (Mathayo 9:13) “lakini nendeni,mkajifunze maana yake maneno haya,
Nataka rehema, wala si sadaka; kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye
dhambi”
(2wakorintho3:12-16)
Basi, kwa
kuwa mna taraja la namna hii, twatumia ujasiri mwingi; nasi si kama musa
alivyotia utaji juu ya uso wake, ili kwamba waisrael wasitazame sana mwisho wa
ile iliyokuwa ikibatilika; ila fikra zao zilitiwa uzito. Kwa maana hata leo
hivi, wakati lisomwapo Agano la kale, utaji uo huo wakaa; yaani, haikufunuliwa
kwamba huondolewa katika Kristo; ila hata leo, torati ya musa isomwapo, utaji
huikalia mioyo yao. Lakini wakati wowote watakapomgeukia Bwana, ule utaji
huondolewa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni