sheria sehemu ya tatu
Sababu ipi Mungu alitupatia Sheria? Ilikuwa ni kutufanya
kuzitambua dhambi zetu na kumrudia kwake kwa toba. Alitupatia vipengele 613 vya
sheria ili tuweze kuzitambua dhambi zetu na kuweza kukombolewa kupitia Yesu
Kristo. Na hii ndiyo maana ya Mungu kutupatia sheria.
Warumi 3:20
inasema “….. kwa maana kutambua
dhambi huja kwa njia ya Sheria”. Hivyo
twajua kwamba sababu ya Mungu kutupatia sheria ilikuwa si kutulazimisha
kuenenda nayo.
Kwa namna hii sasa, tunapata kujua nini juu ya Sheria? Ni
hivi, sisi tu wadhaifu kwa kuitimiza sheria yote na ni wenye dhambi sana.
Tunatambua nini juu ya vipengele hivyo 613 vya Sheria? Tunang’amua mapungufu
yetu na kushindwa kwetu kuifuata Sheria yake.
Tunatambua yakwamba sisi ni viumbe wa Mungu, tulio dhaifu,
na wenye dhambi mbele zake. Ilitupasa sisi sote kutupwa motoni kwa mujibu wa
Sheria ya Mungu. Tunapo tambua dhambi zetu na kushindwa kwetu kuishi kwa
kuzifuata sheria, sasa, na tufanye nini? Je tunajaribu kuishi kwa ukamilifu
wenyewe? Hasha! Yatulazimu kukubali kuwa sisi ni wadhambi, tumwamini Yesu ili
tukombolewe kupitia wokovu wake katika Maji na Roho na kumshukuru yeye.
Sababu ya Mungu kutupa sheria ilikuwa ni kutufanya
tuzitambue dhambi zetu na kujua adhabu yake juu ya dhambi hizo. Hivyo,
itatufanya kuelewa kuwa hakuna njia ya kuokolewa toka motoni pasipo Yesu ikiwa
tutamwamini Yesu kuwa ni Mwokozi, tutakombolewa. Mungu alitupa sheria ili
ituongoze kuelekea kwa Mwokozi Yesu.
Mungu alizifanya sheria ili kutufanya tuweze kutambua ni kwa
namna gani tulivyo wenye dhambi na kuhitaji wokovu wa roho zetu kutoka kwenye
dhambi hizo. Alitupa sheria na kumtuma mwana wake wa pekee, Yesu, kutuokoa kwa
kuzibeba katika ubatizo wake. Kumwamini Yeye kutatufanya tuokolewe.
Sisi ni wadhambi tusio na tumaini lolote, yatulazimu
kumwamini Yesu ili kuwa huru kutoka dhambini, kuwa watoto wa Mungu na
kuurudisha utukufu wake. Yatupasa tuelewe, kufikiri na kuamua kupitia neno lake
kwa kuwa yeye ni asili ya yote. Yatupasa tuikubali kweli ya wokovu kupitia Neno
lake. Hii ni Imani ya Haki na kweli.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni