sheria sehemu ya kwanza
(Marko 7:8-9)“Ninyi
mwaiacha amri ya Mungu na kuyashika mapokeo ya wanadamu. Akawaambia, vema!
Mwaikataa amri ya Mungu mpate kuyashika mapokeo yenu”
(Marko 7:20-23)“Akasema,
kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. Kwa maana ndani ya mioyo ya watu
hutoka mawazo mabaya, uasherati, wivu, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi,
hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu; Haya yote yaliyo maovu
yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi”
Kwanza ningependa kufafanua nini maana ya dhambi. Kuna
dhambi zilizoelezwa na Mungu na nyingine kuelezewa na mwanadamu. Neno dhambi
kwa Kigiriki ‘hamartia’ maana yake ni ‘kukosea katika kulenga shabaha”. Kwa
maneno mengine, ni kufanya jambo pasipo usahihi. Ni dhambi kutotii maelekezo ya
Mungu. Hebu na tuangalie kwa awali maana
ya dhambi kwa mtizamo wa mwanadamu.
Twagundua dhambi zetu kupita dhamira zetu. Ingawa kiwango
cha ubinadamu hutofautiana kulingana na jamii anayotoka, hali ya kimawazo,
katika mazingira na dhamira.
Hivyo, maana ya dhambi inatofautiana kati ya jamii na jamii.
Kitendo cha aina moja chaweza au kisiweze kuchukuliwa kama dhambi endapo kila
jamii itakuwa na aina yake ya vipimo. Ndiyo maana Mungu ametupa vipengele vya
sheria 613 ili vitumike kama vipimo halisi vya dhambi.
Hatupaswi kamwe kuweka viwango vya dhambi kwa kutumia
dhamira iliyowekwa kwa kanuni zetu za kijamii.
Dhambi za dhamira siyo zitokanazo na jinsi ile Mungu
anavyoelezea nini maana ya dhambi. Hivyo tusizisikilize dhamira zetu, bali
tulinganishe viwango vya dhambi zetu na amri za Mungu.
Kila mmoja ana wazo lake juu ya nini maana ya dhambi.
Wengine huchukulia ni udhaifu hali wengine hudhani kwamba ni kutokana na kilema
cha tabia.
Matendo ya kistarabu katika jamii moja yanaweza kuchukuliwa
kwa jamii nyingine kuwa yasiyo ya kistaarabu na kinyama. Ingawa Biblia
inatueleza kwamba dhambi ni kutotii maelekezo ya Mungu. “Ninyi mwaiacha amri ya
Mungu, na kuyashika mapokeo yenu” (Marko 7:8-9). Muonekano wetu wa nje ni
muhimu mbele za Mungu kwa kuwa yeye huangalia kina cha mioyo yetu.
soma sehemu ya pili "KANUNI ZA MTU NI DHAMBI MBELE ZA MUNGU".
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni