Jumanne, 25 Februari 2014

KUPOKEA ROHO MTAKATIFU

Ndugu ninakusihi sana, katika blog hii anza na mafundisho ya awali kama ‘injili ya maji na roho’ ili uweze kumpokea Roho Mtakatifu. Maana bila kumpokea Roho wa Mungu hautoweza kufahamu mafundisho ya ukweli na uwongo. Soma kifungu hichi,  (1wakorintho 2:10-15) lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu. Lakini sisi hatukupokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu. Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni. Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu”
Roho wa Mungu pekee ndiye atakaye kufundisha neno la Mungu kwa usahihi, njia pekee ya kukuwezesha kupokea Roho mtakatifu ni kuwa na imani sahihi katika ubatizo na damu ya Yesu. Tahadhari, usifikiri ubatizo ninaosema ni ule wa maji mengi, hapana. Maji ni ishara ya nje tu ya kile ulicho amini ndani yako, jiulize, kwanini Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizaji?.  (majibu yanapatikana katika masomo yaliyopita).
Wako watu wengi ambao wanajaribu kumpokea Roho mtakatifu kwa kufunga kwa muda mrefu, kujitolea makanisani na mengine mengi, na wengine wakidhani kuwa kila atakaye mwamini Yesu kuwa mwokozi wake basi ataokolewa, lakini ukisoma masomo ya ubatizo utaona kuwa sio sahihi, mfano alikuwapo mtu mmoja aliyeitwa Apolo ambaye Alipoanza kufundisha Efeso kuna mambo hakuyajua kwa usahihi, kama ubatizo wa Yesu, alijua ubatizo wa Yohana tu. Hivyo ilisababisha wale wanafunzi aliowafundisha hawakuweza kumpokea Roho mtakatifu, mpaka pale Paulo alipokuja kuwafundisha kwa usahihi zaidi ndipo wakapokea Roho mtakatifu. (Matendo 19: 24-26) na (Matendo 19:1-6), pia ukisoma habari ya Kornelio (Matendo 10), utaona kuwa Kornelio alikuwa ni mtu wa kujitolea sana, laikini hakuwa na Roho mtakatifu, akapewa maelekezo ya kumwita simioni ili amweleze yampasayo kuyatenda. Ukifika mwisho wa sura hiyo utaona Kornelio kapokea roho mtakatifu kwa sababu ya imani sahihi.
Watu wengi wamekuwa wakidhani kunena kwa lugha, kuombea wagonjwa na kukemea mapepo watakuwa na Roho mtakatifu, lakini nataka nikuambie si kweli. Soma kifungu hiki  ( Luka 10: 20)“lakini, msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa Mbinguni."   Ishara hizi ni moja wapo ya mambo yanayoambatana na aliyeokoka, lakini hata mapepo yanaweza hayo yote. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwajina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitaawambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu nyinyi mtendao maovu. (Mathayo 7:22-23). Mfano katika Agano la kale (kutoka 7) unaweza kuona ni jinsi gani Farao alivyowaita wachawi iliwafanye miujiza na waliweza, japo miujiza yao ilikuwa na mipaka.
Watu wengi wanafanya juhudi za kibinadamu  katika kumpokea Roho mtakatifu, lakini hawaijui “haki ya Mungu” ukisoma masomo yaliyopita katika blog hii kuna somo linalo elezea “haki ya Mungu.”  Inabidi uwamini haki ya Mungu ipatikanayo katika ubatizo na damu ya Yesu ili uweze kumpokea Roho mtakatifu.  Pia soma masomo yaliyopita ujue isemwapo “imani bila matendo imekufa”  je ni matendo ya sheria au matendo ya imani? Pia utajua kwamba Mungu alitupatia sheria aina mbili sheria ya” roho wa uzima” na “sheria ya dhambi na mauti” (Warumi 8:1-4). Hivyo mwanadamu ataokolewa kwa sheria ya roho wa uzima na si kwa sheria ya dhambi na mauti. (Warumi 10:2-4) kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa. Kwa maana, wakiwa hawajui haki ya Mungu, kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki.
Kuna wengine husoma na kudharau, lakini kumbuka bila Roho mtakatifu Biblia utaisoma kama kitabu cha hadithi na shetani atakufunga katika fikira zako. (2 Korintho 4:3-4) “lakini ikiwa Injili yetu imesitirka, imesitirika kwa hao wanaopotea, ambao ndani yao Mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao, isiwazukie nuru ya Injili ya utakatifu wake Kristo aliye sura yake Mungu”
(Warumi 8: 8-9) “wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu. Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili’ bali mwaifuata Roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake”.
Kumbuka mwenye haki hatendi dhambi kwa kukusudia kwa sababu mazingira katika ulimwengu wa Roho yamebadilika, kwamba anaongozwa na Roho wa Mungu, ambaye huingia ndani yake na matunda ya Roho (kama upendo, amani , uvumilivu n.k ).
Agano la kale ni kivuli cha agano jipya,  hivyo kila kitu kina mwenake katika agano jipa kwa agano la kale “tafuteni katika kitabu cha BWANA mkasome hapana katika hao wote atakayekosa kuwapo, hapona mmoja atakayemkosa mwenzake; kwa maana kinywa change kimeamuru na roho yake imekusanya” (Isaya 34:16)


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni