Jumanne, 18 Februari 2014

MAANA YA WOKOVU


Wokovu katika ukristo maana yake ni’ ukombozi toka kwenye nguvu au adhabu ya dhambi .’ tunapokea wokovu pale tunapokiri kwamba hatuna uwezo kujizuia kwenda motoni na kumwamini Yesu ametuokoa sisi sote toka katika dhambi zetu zote kwa kupitia kuzaliwa kwake, ubatizo na damu yake msalabani.
Wale wasio na dhambi kwa kuamini wokovu wa Yesu, ubatizo na damu ya Yesu huitwa “walio okoka” waliozaliwa upya wenye haki.

Tunaweza kutumia neno “wokovu”  kwa wale wote walio okolewa tokana na dhambi zao, pamoja na hatia zile za asili na zile za kila siku, kwa kumwamini Yesu. Kama alivyo mtu aliye jongea kwa Mungu, Yule ajongeaye dhambi za ulimwengu atakuwa ameokolewa kwa kumwamini Yesu kama mwokozi, kwa kuamini ubatizo na damu, maneno ya kweli ya kiroho.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni