Jumanne, 25 Februari 2014

KANUNI ZA MTU NI DHAMBI MBELE ZA MUNGU.

sheri sehemu ya pili

Kushindwa kuishi katika mapenzi ya Mungu ni dhambi. Ni sawa na kutoamini neno lake. Mungu alisema, ni dhambi kuishi kama Wafarisayo ambao walikataa sheria ya Mungu kwa kukazia zaidi msisitizo wa mafundisho ya desturi zao. Yesu aliwachukulia kuwa ni wanafiki.
“Ni Mungu yupi unayemwamini? Je, unaniheshimu na kunitukuza? Unajivunia juu yangu, lakini je unaniheshimu? Mara nyingi watu huangalia umbo la nje na kupuuzia neno la Mungu ndani ya nafsi zao. Je wajua hilo? Matendo ya kuvunja sheria chanzo chake yametokana na udhaifu ambao ni maovu. Makosa tuyafanyayo na upotovu tuutendao kutokana na kutokuwa wakamilifu siyo dhambi kuu ndani yetu bali ni kuanguka katika usahihi. Mungu ametofautisha kati ya dhambi na uovu. Wale wote wenye kulidharau neno lake ni wenye dhambi, hata ikiwa hawana makosa. Ni wenye dhambi zaidi mbele ya Mungu. Na hii ndiyo maana Yesu aliwakemea Mafarisayo.
Katika nyakati za Agano la Kale, kitabu cha mwanzo hadi kumbukumbu la Torati ziliwekwa sheria zilizotaja nini cha kutenda na nini cha kutotenda. Ni maneno ya Mungu Sheria yake. Haitowezekana kwetu kuzitekeleza katika asilimia mia moja, lakini yatubidi kuzikubali kama ni sheria za Mungu. Alitupatia hapo mwanzo na yatupasa kuzikubali kuwa ni Maneno ya Mungu.
“Hapo mwanzo palikuwepo na Neno, naye Neno alikuwepo kwa Mungu, naye Neno alikuwa ni Mungu” Naye alisema “Na uwepo mwanga na ukawepo” Aliumba vyote. Na baadaye, akaiweka Sheria.
“Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu;” (Yohana 1:14). Ni kwa namna gani basi Mungu alijidhihirisha kwetu? Alijidhihirisha kwetu kupitia sheria kwa maana Mungu ni Neno na Roho. Sasa je, Biblia inaitwa nini? Tunaita Neno la Mungu. Imesemwa hapa “Ninyi mwaiacha amri ya Mungu na kuyashika mapokeo ya wanadamu” vipo vipengele 613 katika sheria ya Mungu. Fanya hivi na usifanye vile waheshimu wazazi wako………… nakadhalika. Katika kitabu cha Mambo ya Walawi imetajwa ni kwa namna gani mwanamume na mwanamke wanapaswa kuenenda na nini kifanyike endapo mifugo ikitumbukia shimoni………. Hivi ni baadhi ya vipengele 613 katika sheria.
Kwa kuwa haya si maneno ya mwanadamu, tunapaswa kuyatafakari nyakati zote. Ingawa tutashindwa kutekeleza sheria yote, tunapaswa kwa kiasi Fulani kuzitambua na kumtii Mungu.
Je, kuna kifungu hata kimoja cha maneno ya Mungu yasiyo sahihi? Mafarisayo waliziacha sheria za Mungu na kuzifuata taratibu za mafundisho ya wanadamu dhidi ya sheria ya Mungu. Maneno ya wakuu wao yalichukua nafasi ya uzito wa juu dhidi ya yale ya Mungu.
Yesu alipokuwa duniani, haya ndiyo aliyoshuhudia, na ndicho kilicho umiza moyo wake zaidi kwa kuona Neno la Mungu likipuuziwa na wanadamu. Mungu ametupa vipengele 613 vya sheria ili tuweze kuzitambua dhambi zetu na kutuonyesha kuwa yeye ni mkweli na mtakatifu kwetu. Kwa kuwa sisi sote ni wenye dhambi mbele yake, tunapaswa basi kuenenda kwa imani na kumwamini Yesu kuwa ndiye aliyeletwa na Mungu kwa upendo kwetu. Wenye kuweka neno lake kando na kutoamini watakuwa ni wadhambi. Wenye kushindwa kuenenda katika neno lake pia ni wadhambi, ingawa kuweka kando neno lake ni hatari zaidi. Wenye kutenda dhambi hii wataishia motoni. Kutoamini Neno lake ni dhambi iliyo hatari zaidi mbele za Mungu.
 soma sehemu ya tatu"SABABU YA MUNGU KUTUPATIA SHERIA".

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni