Jumanne, 18 Februari 2014

YESU KUSAFISHA MIGUU YA PETRO (MAANA YA KIROHO)


Maana yake hatuna dhambi tena baada ya kuokoka, hivyo hatupaswi kuomba sala za toba za kila siku.
Katika injiri ya Yohana 13 ipo habari ya Yesu kusafisha miguu ya Petro. Alisafisha miguu ya Petro ili kuonyesha ya kwamba, Petro angetenda dhambi katika kipindi kijacho na kumweleza ya kuwa alikwisha mkomboa kwa dhambi hizo pia, Yesu alijua Petro angetenda dhambi tena katika siku zijazo, hivyo alimimina maji katika karai na kuosha miguu yake.
Petro alijaribu kukataa, lakini yesu alimwambia “nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye.” Kifungu hiki kina maana kwamba “utatenda dhambi tena baadaye” utanikana na kutenda dhambi tena baada ya kuosha dhambi zako zote. Utatenda dhambi hata wakati nitakapo paa kwenda Mbinguni.  Hivyo nasafisha miguu yako ili kumtaadharisha shetani asikutie majaribuni kwa kuwa nimekwisha zichukuwa dhambi zako hata zile zijazo.
Je, unafikiri alisafisha miguu ya Petro ili kutueleza kwamba yatupasa kutubu kila siku? Hapana! Ikiwa tulipaswa kutubu kila siku ili tukombolewe basi ina maana kwamba Yesu isingempasa kuchukuwa dhambi hizo mara moja na kwa wakati wote wa maisha yetu.
Lakini Yesu alisema alitutakasa mara moja na kwa wakati wote ikiwa tungehitajika kutubu kila siku, basi ingekuwa kama vile tumerudi katika kile kipindi cha Agano la kale. Sasa tungeweza kuwa wenye haki? Nani angeweza kukombolewa kwa ukamilifu? Hata kama tulimwani Mungu, ni nani angeweza kuishi bila dhambi?
Hivyo, Yesu alibatizwa mara moja na kujitoa yeye mwenyewe msalabani mara moja ili tuweze kutakaswa mara moja na wakati wote. Je, unaweza kuelewa hili?
Tumekombolewa kutoka dhambini kwa kumwamini Yesu aliyezichukuwa dhambi zetu zote,
“ na kila kuhani kila siku akifanya ibada na kutoa dhabihu zile zile mara nyingi; ambazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi. Lakini huyu alipokwisha kutoa kwa ajiri ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele aliketi mkono wa kuume wa Mungu tangu hapo akingojea hata adui zake wawekwe  kuwa chini ya miguu yake maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa. Na Roho Mtakatifu naye amshuhudia; kwa maana, baada ya kusema hili ni Agano nitakalo agana nao baada ya siku zile anena Bwana, nitatia sheria zangu katika nia zao nitaziandika ndipo anenapo. Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa, basi ondoleo la haya likiwapo, hapana toleo tena kwa ajiri ya dhambi” (waebrania 10:11-18)
Nini maana ya “basi ondoleo la hayo likiwapo” katika mstari wa 18 hapo juu? hii ina maana ya kwamba kila dhambi ilifutwa kabisa bila uchaguzi Mungu alizifuta dhambi zote na kutusamehe.
Nahitimisha kwa kusema kuwa; tuna okolewa bure kwa neema ya Mungu katika imani, lakini neema hiyo haituruhusu kutenda dhambi makusudi, kwa sababu ile nguvu ya kuishinda dhambi tumepewa (Roho Mtakatifu) kwa kuamini katika siri ya Mungu. (kuifahamu siri ya Mungu soma masomo yaliyopita).

“Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi? Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo tulibatizwa katika mauti yake? Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa baba , hivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima  (Warumi 6:1-4)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni